TBC acheni fake news, acheni michezo ya kitoto!

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
10,149
2,000
Inasikitisha kwa TV ya Taifa kutumika kusambaza uongo, kuwa vijana wa Chadema hawataki katiba mpya

Hii michezo yenu ni ya kudanganya umma, mnafanya propaganda za kitoto na mnavunja katiba ya nchi na sheria za utangazaji kwa sababu mnalisha wananchi taarifa za uongo, matukio yaliyo staged.

TBC mnachokifanya ni kinyume cha kanuni za TCRA kwa sababu mnasmbaza taarifa za uongo

Kitu kingine ni kuwa serikali ya Samia nayo inatia aibu, imeanza kuongoza nchi kwa uongouongo. Hizi propaganda za kutengeneza, za kuchukua vijana wengine wa CCM na kuwavisha uniform za Chadema ni utoto.

Jibuni hoja za CHADEMA acheni propaganda mfu na uongo. Ni aibu kwa serikali kudanganya watu wake.

Na kama TISS inahusika, basi hii ni michezo muflisi, jipangeni mje na mipango mizuri kwa ajili ya mustakbali wa Taifa, ni aibu kwa taasisi ya Intelijensia kufinance michezo ya namna hii ya kudanganya na kubraiwash watu.

Please Acheni kudanganya umma, mnavunja sheria, mnavunja katiba kwa kuwalisha watu taarifa za uongo

IMG-20210801-WA0039.jpg
 

The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
7,529
2,000
Halafu huyu aliyeteuliwa kuwa msemaji wao alikosa kabisa "fluency" katika kutoa hiyo taarifa yake.

Ongea yake ni ya kubabaika babaika, ya kutafuta maneno ikiwa ni ishara ya kuonesha kuwa hayo asemayo si yake, amekaririshwa maneno ya kusema na mtu mwingine...

This is too bad kwa vijana hawa. They are ignorantly being used by the power hungry lions inside CCM and the govt.

Mimi nawambia hivi TISS [MATAGA], polisi na CCM na serikali yenu.

Kwamba, lazima mfahamu kuwa kwa sasa tupo katika majira na msimu mwingine mpya kabisa ambao unaongozwa na taratibu na njia mpya vilevile, siyo zile tena.

Inasikitisha sana kuwa hawa TISS [MATAGA], polisi na CCM na serikali yao hawajatambua kuwa nyakati na majira yamebadilika sana.

Kwamba, hawajui kabisa kuwa, ilivyokuwa mazingira ya utawala na ya kisiasa ya miaka 10 nyuma ni tofauti sana na haya ya sasa.

Kwamba, hawajui kabisa kuwa mbinu na propaganda za miaka 10 iliyopita haziwezi kufanya kazi ktk nyakati hizi.

Kwa kifupi, ni kuwa, moto wa mabadiliko haya ya sasa uliokwisha kuwaka hauwezi kuzuilika au kuzimwa kwa kukinga mikono yao unless wanataka kuungua na kuteketea kabisa.

It's either mkubaliane na mahitaji ya wakati na majira haya au muwe kicked out kwa aibu na fedheha kubwa.
 

kichomiz

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
17,716
2,000
TBCCM kama kawaida yao, hakuna mwenye maarifa/upeo hata mmoja ndio maana wanatengeneza cinema za kitoto kama hizo
 

Lutifya

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
1,607
2,000
Naona tunarudi kulekule tulikoishia mwezi wa tatu. Mama ameanza kuupiga mchache. Wahafidhina wameanza kumwingiza chaka kwa Fake News.
 

Bobby

JF-Expert Member
Jan 10, 2008
2,060
2,000
Kitu kingine ni kuwa serikali ya Samia nayo inatia aibu, imeanza kuongoza nchi kwa uongouongo. Hizi propaganda za kutengeneza, za kuchukua vijana wengine wa CCM na kuwavisha uniform za Chadema ni utoto.
All along nilijua huu ujinga nao ulishazikwa. Wanaacha kutoa elimu khs UVICO 19 wanakuja na hizi propaganda za kijinga hivi kwa chombo cha umma kinachoendeshwa kwa kodi zetu. Nimeanza kuelewa ni kwann kuna mtu alisema yy na hayati na kitu kimoja na kweli ni kitu kimoja kwa haya tunayoshuhudia sasa.
 

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
10,149
2,000
They are deceiving people of the united republic of Tanzania, that is crime. Wanavunja sheria za nchi waziwazi kwa kusambaza fake news
 

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
87,253
2,000
Kitu kingine ni kuwa serikali ya Samia nayo inatia aibu, imeanza kuongoza nchi kwa uongouongo. Hizi propaganda za kutengeneza, za kuchukua vijana wengine wa CCM na kuwavisha uniform za Chadema ni utoto.
Uchunguzi unaonyesha kwamba hii ndio serikali duni kabisa kimawazo kwa sasa barani Africa , ikifuatiwa kwa mbaali na Somalia
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom