TBC 3 mlichotufanyia wakati wa mechi ya Simba na Sevilla ni uhuni na ubabaishaji

Bazazi

JF-Expert Member
Aug 18, 2008
2,806
3,476
Tarehe 23/05/2019 mlionesha mechi ya kabumbu baina ya Simba SC Vs Sevilla FC ya Hispania.

Mlichofanya ni uhuni & ubabaishaji. Hakukuwa na jambo lolote linaloendana na mechi ya kabumbu; hakuna matangazo kama mtaionesha, hakuna uchambuzi wala sauti wakati wa mechi. Mechi imeonesha kibubububu tu.

Mkurugenzi mwenye PhD akiwa ni mhadhiri unatia aibu kubwa. Hii mechi mungewaachia tu Azam waioneshe.

TBC ndo sababu hamna waangaliaji kisa ubabaishaji. Mbadilike

Nimesema!
Bazazi
 
Hivi kwa nini haikuonyeshwa Azam TV. Niliiangalia kupitia Tanzania channel ile ya wanyama. Kwa kweli haikuonekana vizuri.
 
Sportpesa ni mchezo wa kamari na Azam huwa wanajinasibu kutofungamana na wacheza kamari kwa sababu hiyo ni dhambi kwa mujibu wa imani yao. Hujagundua tu hata yale mashindano ya kila mwaka ya sportpesa huwa hawaoneshi kupitia channel zao isipokuwa zile tu chache za kwenye decoder zao.
 
Azam Tv na Sportpesa (kampuni za kamari) ni maji na mafuta.
Hawakuwa na copyrights tu mkuu ya kuipeperusha mechi hewani na Sportpesa wanafanya marketing ya kampuni yao bado haijakuwa kubwa sana na haijawafikia wengi.

Wangerusha Azam wasingewafikia watu wenye Startimes, Zuku n.k
Kumbuka mkurugenzi wa sportpesa ni muislamu Abbas Tarimba mtu wa masoko ambaye namkubali sana ni Kelvin Twisa anajua kucheza na hizi mambo
 
Sportpesa ni mchezo wa kamari na Azam huwa wanajinasibu kutofungamana na wacheza kamari kwa sababu hiyo ni dhambi kwa mujibu wa imani yao. Hujagundua tu hata yale mashindano ya kila mwaka ya sportpesa huwa hawaoneshi kupitia channel zao isipokuwa zile tu chache za kwenye decoder zao.
Basi wasingeonesha mechi za simba na yanga
 
Tarehe 23/05/2019 mlionesha mechi ya kabumbu baina ya Simba SC Vs Sevilla FC ya Hispania.

Mlichofanya ni uhuni & ubabaishaji. Hakukuwa na jambo lolote linaloendana na mechi ya kabumbu; hakuna matangazo kama mtaionesha, hakuna uchambuzi wala sauti wakati wa mechi. Mechi imeonesha kibubububu tu.

Mkurugenzi mwenye PhD akiwa ni mhadhiri unatia aibu kubwa. Hii mechi mungewaachia tu Azam waioneshe.

TBC ndo sababu hamna waangaliaji kisa ubabaishaji. Mbadilike

Nimesema!
Bazazi
Kiherehere kilikupeleka TBC? Umekipata ulichokuwa unakitafuta. Wakati unaenda kuwasha chaneli yako ulituambia? Ugulia kimya kimya.
 
Habari naomba kujua kwa wafwatiliaji wa mpira wa miguu Simba na Sevilla Jana kwanini TV Jana haizikuwa na mtangazaji kama game zingine,tumebishana sana leo nawengi bila majibu kupata,wengine wakisema mkataba haukuruhusu mtangazaji kuwepo na mengine mengi, tujuzane kwa wanaojua ASANTE
 
Hawakuwa na copyrights tu mkuu ya kuipeperusha mechi hewani na Sportpesa wanafanya marketing ya kampuni yao bado haijakuwa kubwa sana na haijawafikia wengi.

Wangerusha Azam wasingewafikia watu wenye Startimes, Zuku n.k
Kumbuka mkurugenzi wa sportpesa ni muislamu Abbas Tarimba mtu wa masoko ambaye namkubali sana ni Kelvin Twisa anajua kucheza na hizi mambo
Azam hawawezi kurusha mechi hizo hata mkurugenzi akiwa mtoto wa Bhakresa.
 
Mbona Yanga na Simba na tim zingne znazodhaminiwa na SPORT PESA wanarusha/wanaonyesha tim hizo zikiwa na jezi zimeandikwa Sportpesa sehemu ya tumbon!

Kama sababu ni hiyo kwa Azam wamechemka! Vingnevyo labda kuwe na sababu nyingne
 
Azam hawawezi kurusha mechi hizo hata mkurugenzi akiwa mtoto wa Bhakresa.
Azam wanatafuta hela mkuu usiwe mbishi.
Sportpesa hawajawahi kuwapelekea Tenda Azam, Sportpesa wanarekodi kwa kamera zao.

Ligi ya La liga wanayoirusha timu kibao zinadhaminiwa na kampuni za kamari.
TPL timu nne zinadhaminiwa na kampuni za kamari.

Mkurugenzi wa Azam Tido muhando nadhani si muislamu, mkurugenzi wa idara ya michezo Patrick kihemela si muislamu hapa MAUDINI HAYAPO.

Azam walikuwa wanarusha ndondo cup iliyokuwa ikizaminiwa na mdhamini mkuu M-cheza ni kampuni ya kamari.
Hapa tatizo tenda tu
 
Mi niliangalia kama dk 3 tu nikaona nyama za buchani zinazurura kwa TV nikazima nikaendelea kuangalia kupitiaive stream!
 
Tarehe 23/05/2019 mlionesha mechi ya kabumbu baina ya Simba SC Vs Sevilla FC ya Hispania.

Mlichofanya ni uhuni & ubabaishaji. Hakukuwa na jambo lolote linaloendana na mechi ya kabumbu; hakuna matangazo kama mtaionesha, hakuna uchambuzi wala sauti wakati wa mechi. Mechi imeonesha kibubububu tu.

Mkurugenzi mwenye PhD akiwa ni mhadhiri unatia aibu kubwa. Hii mechi mungewaachia tu Azam waioneshe.

TBC ndo sababu hamna waangaliaji kisa ubabaishaji. Mbadilike

Nimesema!
Bazazi
Mimi nilidhani ni TV yangu!, Kumbe walikuwa wanashindwa kutaja majina ya wachezaji wazungu!.
 
Back
Top Bottom