TBC 1 & Taifa zingatieni haya ili kujiboresha

AKILI TATU

JF-Expert Member
Feb 10, 2016
2,658
2,804
TBC Taifa na TBC 1$ 2 zinakabiliwa na tatizo la kuamini wenye vyeti tu badala ya kuangali pia watu waliosoma na wenye vipaji,hii hali imelifanya shirika hili kuwa na 'staff mizigo' wasio kuwa na nia ya dhati ya kufanya kazi kutoka mioyoni mwao bali wanafanya kazi kwa kutimiza wajibu,hali hii ni mbaya sana ,kwani ninauhakika asilimia kubwa ya watangazaji na waandaa vipindi wa luninga au redio ya taifa wengi wao aidha walikuwa na ndoto nyingine wakajikuta wamesomea fani ya habari wakati wanasoma au huenda wakawa ni aina ya watu waliolazimishwa kusoma fani ya habari ndio maana wao wenyewe binafsi wanashindwa kuwa na msukumo wa uthubutu kutoka ndani ya mioyo yao.

Hilo moja,mbili nadhani imefika hatua kwa TBC hasa uongozi wake ukapeleka ushauri kwa Serikali ya kutka kujiendesha kwa ushindani,hii itasaidia kwanza kutanua wigo wao katika kuwafikia watu wengi zaidi,kwani katika hali hii itapelekea uwepo wa uthubutu wa kiushindani kutoka ktika shirika hilo dhidi ya media nyingine.

Lakini pia TBC ijaribu kuangalia watangazaji wenye vipaji ambao wako katika media nyingine ili kusudi iundwe timu ya watu wenye ushindani.

TBC inatakiwa iwe inatoa motisha pia kwa watangazaji wake ili kuwafanya waone kama wanauhitaji wa wao kufanya makubwa zaidi kutokana na motisha wanazopata
 
Back
Top Bottom