TBA na EWURA CCC kitengo cha walaji zifumuliwe haraka au zifutwe kabisa

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,279
21,396
Naomba niwafahamishe wananchi juu ya mamlaka hizi mbili za serikali;

A). TBA (Tanzania Building agency)

Hawa ni mawakala Wa majengo Tanzania, Hawa jamaa kazi yao kubwa Kushauri Ufanisi katika majengo ya serikali (Consultant), Hawa TBA wana wataalam ambao ni Architect, Quantity surveyor, Engineers n.k ambao hufanya shughuli za kudesign majengo mbalimbali ya serikali na kushauri ubora kwenye majengo mbalimbali ya serikali ie. NHC, etc
kwa lugha rahisi ni kwamba TBA ni washauri/ wasimamizi Wa fundi ili asichakachue!
kwa lugha rahisi TBA siyo Fundi Bali ni mshauri Wa-Fundi.
KWA NINI TBA IFUMULIWE/IFUTWE?
Nina kila sababu za kuomba TBA ifutwe kama ifuatavyo;
  • kwanza kabisa wamejisahau kufanya majukumu yao ya msingi ya kubuni majengo na kusimamia(design & consulting)
  • pili, TBA wamegeuka madalali Wa ufundi, yaani hawana experience na site, hawana Technicians wenye uzoefu na kazi zaidi ya kuokota okota.
  • tatu, TBA, kwasababu ya loop hole ya kujisimamia, tangu waanze kufanya kazi zisizokuwa zao ( yaani wanajenga na kujishauri) hii imetengeneza mwanya Wa upigaji ndani ya hii taasisi, jambo lililochangia ufanisi kupungua.
  • Mfano; hostels za magufuli walipojenga dosari zile walizitetea wao wenyewe,
  • Majengo ya magereza pale Ukonga yamebuma hadi leo hadi raisi kaamua kuwapokonya tends na kuwapa wanajeshi
  • majengo pale magomeni yamebuma n.k
  • Kazi za TBA zinaweza fanywa kwa kuanzisha department tu ndani ya NHC inatosha.
Kuliko kuendeleza hasara TBA IFUMULIWE AU IFUTWE Na kianzishwe kitengo ndani NHC kitakachofanya kazi za kudesign na kushauri. mambo ya ujenzi/Site zitaendelea kuratibiwa chini ya bodi ya wakandarasi FULL STOP

B) EWURA CCC

Katika mamlaka ya Ewura, kuna kitengo kinaitwa Ewura CCC ( Ewura Consumer consultative Councils)
Hiki ni kitengo kinachotutetea wananchi (walaji) kuhakikisha tunapata bidhaa inayostahili; Na inapotokea mtoa huduma hatutendei haki, Ewura CCC wana majaji kutoka mahakama kuu ambao pale pale Ewura kuna mahakama husikiliza pande zote na kutoa hukumu.(FIDIA)

yaani kwa mfano,
  1. kama ni mafuta basi Ewura CCC inahakikisha tunapata mafuta safi na salama.
  2. kama ni maji basi Ewura CCC wanahakikisha tunapata maji safi
  3. kama ni gas basi iwe ni gas salama
  4. kama ni Umeme basi uwe ni Umeme unaokidhi sheria za kimataifa IEE ambao kwa hapa Tanzania tunapaswa kuwa Umeme 220V-240V
  5. Ewura CCC inawajibu wakututetea wananchi kupatiwa huduma bora na kwa wakati katika sekta ya NISHATI
KWANINI HIKI KITENGO NAOMBA KIFUMULIWE AU KIFUTWE?
Bila ubishi Ewura CCC ama kwa makusudi ama kwa kutokujua ama kwa mazoea ya watanzania tuliowengi kufanya kazi za maslahi binafsi tu kitengo hiki kimeelemea upande mmoja tu Wa mafuta na gas!

Ewura CCC wamejitahidi sana kusimamia upande Wa mafuta na gas (sheli za mafuta) ama huenda kwasababu huku kuna hatari zaidi ndiyo maana wameelemea, ama huenda kwenye mafuta kuna bahasha ndiyo maana wameelea huku, lakini yote heri cha msingi upande huo wamejitahidi,
Ewura CCC Wamefeli sana kwenye huduma za usimamizi Wa MAJI NA UMEME
Tukiachilia mbali jambo la kiusalama kwa vifaa vya walaji, ubora Wa maji unatia mashaka makubwa na Ewura CCC wapo wamekaa ofisini wanasubili wapelekewe malalamiko ofisini.
  • Ukiachilia mbali mita inayohesabu hadi upepo, bado ewura yaani wanasubiri hadi mwananchi abebe ndoo ya maji akawaoneshe ofisini kwamba Yale maji ni machafu.
  • Vifaa vingi vinavyotumika hapa Tanzania vina rate ya Umeme 220V-240V, lakini mitaa mingi hususani huku mijini wananchi tunaonunua AC, FRIJI haziwaki kwasababu ya Umeme mdogo, yaani Umeme unasoma 120V,140V-170V jambo linalopelekea hata vifaa vyetu vingi kuungua Ewura CCC wapo maofini wametulia.
  • Umeme unayumba yaani unapanda na kushuka(hauko stable) Lakini hakuna Ewura CCC utawasikia wakifuatilia ubora Wa bidhaa hii ya umeme majumbani inayomgusa kila mtu sasa sijui kwasababu huku kunawanyonge wengi(hakuna bahasha) au wanaogopa kumwajibisha mtoa huduma kwasababu MAMA NA BABA YAO NI MMOJA!
  • Kutambua ubora Wa Umeme na haihitaji hata gharama kubwa kujua, ni kitendo cha Ewura CCC kuamua kwenda mtaa wowote wakapime kiwango cha umeme mdogo uliopo mijini mwetu.
IPO KILA SABABU YA VITENGO HIVI KUSUKWA UPYA AMA KUFUTWA KABISA.

Kama wakala Wa madini TMAA Iliweza kufumuliwa, nakuletea tena na TBA na EWURA CCC Piga Chini wasifanye kazi za mazoea!

NAOMBA KUWASILISHA!!!!

Unaweza kusoma ufafanuzi wa EWURA CCC hapa >>> Ufafanuzi kuhusu Kazi na Majukumu ya Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Nishati na Maji(EWURA CCC) - JamiiForums
 
Kwa kweli umeongea jambo jema kabisa hasa suala la umeme kama huku chanika mimi nina friji inanibidii niamke alfajiri sana na kuwasha friji. Ikifika saa tatu asubuhi inazima yenyewe kwani muda huo matumizi yanakuwa makubwa. Kwa maana wengi watakuwa tayari kazini wamewasha vyombo mbalimbali hivyo tunanyang'anyana hiyo huduma.
 
Mimi kwangu huku SALASALA AC nikiwasha haiwaki nilimwita fundi akaniambia Umeme ni mdogo, kwahiyo AC zimebaki pambo tu zinanyewa na popo!
 
Kwa kweli umeongea jambo jema kabisa hasa suala la umeme kama huku chanika mimi nina friji inanibidii niamke alfajiri sana na kuwasha friji. Ikifika saa tatu asubuhi inazima yenyewe kwani muda huo matumizi yanakuwa makubwa. Kwa maana wengi watakuwa tayari kazini wamewasha vyombo mbalimbali hivyo tunanyang'anyana hiyo huduma.
jamaa kanifumbua macho sana, hivi kumbe kuna mamlaka za kufuatilia haya wamenyamaza! Tanzania yetu tunawatu Wa ajabu sana
 
Kwa TBA Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania, Amesema Jana Dawa Imeshacheka Ni TBA Kunyweshwa Muda Wowote Tu.
EWURA Nao Wajipange Waache Sababu
Muda Umekwisha Zamani
 
Kuhusu TBA kutokufanya kazi kwa wakati na bajeti ni suala lililotegemewa kutokea tu, kwa wajuzi wa mambo tulijua hilo kitambo sana.

Ilianzia kwenye hostel za UDSM ambapo mradi wa bil. 50+ , TBA walidai wameujenga kwa bil. 10, na watu waliokuwa wanatia mashaka juu ya hiyo bei kazodolewa na kuitwa wapiga dili.

TBA wamekuwa wakifanya kazi kisiasa badala ya kitaalam, wanataja kufanya miradi kwa bei ndogo, matokeo yake wanatumia hela za miradi mingine kukamilisha miradi yenye uharaka. Pia wanashindwa wakiwa field kutokana na gharama halisi kuwa kubwa tofauti na bei waliyotoa na kupewa.

Jambo jingine TBA kwa mujibu wa structure yake ilikuwa taasisi ya Kusimamia tu majengo ya serikali(Consultant/ Client representative) katika awamu iliyopita hata majengo yaliyokuwa chini ya milki yao yalijengwa na wakandarasi wengine, lakini baada ya awamu ya rais Magufuli kuingia madarakani wakapewa kazi ya kujenga majengo yote ya serikali na taasisi zake nchi nzima. Hali hiyo imewafanya wawe na mzigo mkubwa juu ya uwezo wao wa kiuendeshaji. Kazi ya ujenzi ni ngumu na inahitaji umakini mkubwa na uangalifu sana.

Serikali inachotakiwa kufanya ni kuwapa kazi wakandarasi kwa njia ya zabuni kama ilivyokuwa zamani, iachane na kuzipendelea taasisi zake au kufanya kwa Force account maana hilo nalo ni janga jingine huko mbeleni. TBA ibaki kama msimamizi kwa niaba ya serikali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kweli kabisa
 
TBA...kuna nyumba zaidi ya 3500 kule Bunju B mabwepande..walizijenga bila kumalizia ndani...walitakiwa kuziuza...sasa yamekuwa magofu....serikali iingilie kati...zile nyumba zimaliziwe ndani na kuuzwa kwa mtanzania yeyote mwenye uwezo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom