TB Joshua hakuwahi kubatizwa wala kumpokea Yesu! Nimeshangaa sana

Kusema mimi ni muumini ni sawa na kusema mtu aliyenyoa kipara kasuka nywele mtindo wa kipara.
Hahahaha!
Huwezi sema Mungu hayupo bila kuthibitisha. +ve na -ve zote ni chaji. Ni bora ukakaa kimya paka pale itakapothibitika yupo au hayupo.
 
Mtu akisema ndani Kuna kikombe na mwingine akasema ndani Hakuna kikombe, Nani kati ya hao wawili anapaswa kuthibitisha uwepo wa kikombe ndani?

Kwanini uwepo wa mungu mnataka wasioamini uwepo wake ndio wathibitishe na sio Nyie mnaosema Mungu yupo?

Wote wanaweza kuthibitisha.

Kwanini waamini Mungu hayupo bila uthibitisho? Na kwanini wasikae kimya tu paka pale itakapothibitika?

_Hawakai kimya sababu wao pia ni waumini wanaoamini Mungu hayupo.
 
View attachment 1813227



Ubatizo wa maji ni udhihirisho wa nje kwamba umempokea Kristo!

Wapo waliompokea Kristo pasipo udhihirisho huo wa nje na kuokolewa!

Ref: Mwizi msalabani aliye mkiri Kristo na kuokolewa pasipo ubatizo wa maji.
Mwizi Msalabani hakubatizwa kwa sababu hakupewa nafasi au muda wa kuishi.Na hii hutokea kwa watu ambao muda mfupi ameongozwa sala ya Toba harafu akafa! Mtu wa jinsi hiyo Toba yake inatosha kumwokoa.
Lakini akipewa nafasi ya kuishi ni LAZIMA kubatizwa ili kukamilisha Wokovu baada ya Toba kama Kristo alivyoagiza,
Marko16:15-17,Matendo 2:38
Kama TB alikataa kubatizwa kwa Maji tele kwa visingizio vyake,huyo hesabu alikuwa akipita Njia pana na Mlango Mpana,(Mathayo7:13-14)
Kama alienda na sababu zake huenda alipewa Majibu kama haya,
(Mathayo7:22-23)
 
Wote wanaweza kuthibitisha.

Kwanini waamini Mungu hayupo bila uthibitisho? Na kwanini wasikae kimya tu paka pale itakapothibitika?

_Hawakai kimya sababu wao pia ni waumini wanaoamini Mungu hayupo.
Mtu anaesema kikombe kipo atathibitishaje?
 
View attachment 1813227



Ubatizo wa maji ni udhihirisho wa nje kwamba umempokea Kristo!

Wapo waliompokea Kristo pasipo udhihirisho huo wa nje na kuokolewa!

Ref: Mwizi msalabani aliye mkiri Kristo na kuokolewa pasipo ubatizo wa maji.
Sawa kabisa. Ila kumbuka huyo mwizi alikufa palepale hakuwahi kutumika au kumtumikia Mungu. Ubatizo wa maji ni takwa kuu la utumishi na sio wokovu. Kama mtumishi lazima ubatizwe tena ubatizo wa maji mengi mtoni kama Kristo Yesu. Sauti haikutoka mbinguni mpaka alipozamishwa na kuibuka ndio mbingu zikasema "huyu ni mwanangu mpendwa niliyependezwa naye".
 
Hahahaha!
Huwezi sema Mungu hayupo bila kuthibitisha. +ve na -ve zote ni chaji. Ni bora ukakaa kimya paka pale itakapothibitika yupo au hayupo.
Naweza kuthibitisha Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.

Using proof by contradiction.

Kama ninavyoweza kuthibitisha 10 si square root ya 2,

Using proof by contradiction.
 
Unaposema kitu kipo au hakipo bila sababu au bila uthibitisho ndio maana ya imani. Unakosoa wanaoamini yupo akati na wewe unaamini hayupo.
Nimekuuliza swali naomba unijibu.

Kama kikombe kipo ndani na mtu akasema kikombe kipo, atathibitishaje kuwa kipo ?
 
Nijuavyo kiasilia TB Joshua katokea madhehebu ya Anglican kabla hajaanzisha huduma yake. Kama alikuzwa huko hizo doubt si za msingi.

Yesu aliamuru mitume nendeni ulimwenguni kote mkafanye wote wanafunzi wangu mkiwabatiza kwa jina la baba, mwana na Roho Mtakatifu. Hayo mambo ya kumpokea Yesu kwa kusema sala fupi wanavyofanya walokole leo haijawahi kuwa njia iliyotumika hata na mitume.

Huwezi kukuta nukuu yoyote kwenye biblia mtu akiendeshwa zile sala eti ndio aokoke! Mbaya zaidi wengine tayari ni wabatizwa! Sasa mlokole akianguka dhambini anaokoka tena? Kuna tofauti gani na mbatizwa ambaye hajasema ile sala? Mkristo hata uwe safi kiasi gani, unajua neno kiasi gani bila kwenda kwenye makanisa ya kiroho kusema ile sala eti hujaokoka!!

Niliwahi kusikia hadi Gwajima akifundisha kuwa madhehebu kama Katoliki, Lutheran, Anglican hawajaokoka ingawa ni wakristo!
 
Nimekuuliza swali naomba unijibu.

Kama kikombe kipo ndani na mtu akasema kikombe kipo, atathibitishaje kuwa kipo ?
Kuna mambo mengi ambayo mwanzo hayakuthibitika lakini baadae yakathibitika kwamba yapo. Kama umesoma comments zangu toka mwanzo nimetoa mfano.

_Kama kitu hakijathibitishwa haimaanishi hakipo, kikithibitishwa kinaweza kuwepo au kisiwepo. Kusema kipo au hakipo bila uthibitisho ni imani.
 
Nimekuwa nikifuatilia kifo cha gwiji huyu wa gospo tangu kilipotokea.

Jana nilishangaa hoja ambazo Jumuia ya makanisa ya kikristo ya Nigeria na Jumuia ya makanisa ya kipentekoste kumkataa kabisa TB Joshua kama Mkristo mwenzao.

Alipoulizwa sababu ya kumkataa, mwenyekiti mmoja wa jumuia hiyo aliwahi kusema.

TB hajawahi kubatizwa, au kuonyesha alimpokea Yesu lini na wapi na kwa pastor yupi. Hawakubaliani na agenda yake kuwa yeye Yesu alimalizana naye tangu akiwa tumboni mwa mama yake mimba ambayo ilikaa miezi 15.

Kwa kanuni za kikristo na Kibiblia mtu akiwa na akili timamu ndio anatakiwa amchague Yesu sio tumboni. Lakini pia kwa wengine akiwa mtoto hubatizwa. Lkn sio tumboni na angalau aonyeshe ushahidi wao hawatapata shida kabisa.

Huyu ndiye Gwiji wa injili aliyekuza sekta ya utalii nigeria kwa njia ya injili. Kuna mwaka ulifika ndege ikitua na wazungu 10 nigeria zaidi ya sita wote walikuwa wanaenda SCOAN kulamba upako.
Kama waliona hivyo kwa nini hawakuchukua hatua ya kumwongoza Sala ya toba???
 
Siyo tu Mungu huyu hawezi kuthibitishwa kuwepo, bali pia uwepo wake unakuwa contradicted na hali halisi kwa namna ambayo inaonesha hayupo.

Unaambiwa Mungu ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote.

Aliweza kuumba dunia isiyo na kifo, mabaya, magonjwa, etc.

Lakini hakuumba hiyo, akaumba hii ya ma pandemic na matetemekonya ardhi na ma tsunami.

Kwa nini Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote awe mkatili hivyo kwa viumbe wake?
Uwepo wa dunia na the whole universe and every living thing in it ni uthibitisho tosha kuwa MUNGU yupo. Kazi aliyoifanya ya uumbaji inathibitisha uwepo wake.

MUNGU aliumba dunia iliyokuwa nzuri, yaani it was a perfect creation. Hakukuwa na udhaifu wa aina yoyote, wala majanga (natural disasters) ya aina yoyote ile.

Isipokuwa, MUNGU siyo dicteta na wala hakuumba machines, bali alimuumba kiumbe ambaye anauwezo wa kuchagua, kufikiri na kutenda kwa uhuru. Kiumbe huyu ni Mwanadamu ambaye ndiye aliyekabidhiwa dunia yote iwe chini ya utawala wake. Katika viumbe vyote vyenye mwili ni Mwanadamu peke yake aliyepewa akili, ufahamu, hekima, busara na maarifa, na uhuru wa kuamua, free will. Hii ilikuwa ni hatua ya kwanza ya uumbwaji ya mwanadamu.

Baada ya uumbaji MUNGU alimweka huyu Mwanadamu katika dunia iliyokuwa perfect kabisa lakini MUNGU alimpa maagizo kisha akamwacha huyu Mwanadamu aamue mwenyewe, kufuata maagizo aliyopewa ili aendelee kuishi katika dunia njema au akiuke maagizo na kujitenga na MUNGU na kuingia kwenye dunia ya matatizo.
Ndiyo maana ya tunda la uzima au tunda la mema na mabaya.

Mwanadamu kwa ukaidi alichagua tunda la mema na mabaya na kuacha tunda la uzima. Matokeo yake ndiyo hayo kwamba leo hii dunia imejaa mambo mabaya na mambo mazuri, utajiri na umaskini, ugonjwa na afya, furaha na huzuni, ujana na uzee, uhai na mwisho kifo.
Hayo yote yapo kwasababu Mwanadamu wa kwanza alichagua mwenyewe.

Kwanini MUNGU aliruhusu iwe hivyo?
Kwanza kabla ya kujibu hilo swali, tunapaswa kujua ni nini lilikuwa dhumuni la MUNGU kumuumba Mwanadamu ?
Kwa kifupi sana ni kwamba MUNGU alimuumba Mwanadamu ili huyu Mwanadamu kwa kupitia utiifu wake ambao ni wa hiari akamilike awe kama MUNGU. Kwa lugha rahisi MUNGU aliwaumba Wanadamu ili hawa Wanadamu wawe Miungu yaani tuwe watoto wake, tukifanana naye kitabia kama yeye alivyo.

Baada ya Mwanadamu kuumbwa utaona alikuwa bado hajakamilika. Ili akamilike ilimpasa kwanza kwa hiari yake awe "mtiifu" kwa MUNGU. Na ndiyo maana utaona katika Biblia imeandikwa kuwa baada ya MUNGU kumuumba Adamu na kumuweka ndani ya bustani iliyokuwa timilifu alimpa maagizo; kwanza, kuitunza bustani, pili, kutawala kila kitu ndani ya bustani hiyo, tatu, azaliane aongezeke na nne, asile matunda ya mti uliokuwa katikati ya bustani.

Utaona kwa maagizo hayo Adamu alikuwa anaandaliwa kuwa "mtiifu" ,ili akifaulu basi aingie hatua ya pili ya uumbwaji yaani akamilishwe kuwa kama MUNGU. (hii nitaielezea hapo mbele).
Unfortunately Adam alishindwa kuwa "mtiifu", badala yake akawa "mkaidi".

In every action there are consequences. Kwenye "utiifu" kuna consequences zake na kwenye "ukaidi" kuna consequences zake. Kwenye utiifi utapata uzima na mema yote. Kwenye ukaidi utapata mema kidogo, mabaya mengi na mwisho kifo.
Dunia tunayoishi sasa hivi ni sababu ya UKAIDI wa Adam.

Je, malengo au dhumuni la MUNGU lilipotea baada ya Adamu kukaidi?
Jibu ni hapana. Dhumuni la MUNGU bado liko pale pale, kumfanya Mwanadamu kuwa kama Mungu. Hivyo basi baada ya Mwanadamu kukaidi, MUNGU hakutaka kumwangamiza kabisa Mwanadamu badala yake akaruhusu kipindi cha mpito, yaani kipindi cha shida, mateso, mahangaiko, magonjwa, na kifo ili miongoni mwa Wanadamu hawa wapatikane wale watakaochagua kuwa "watiifu" ili awakamilishe katika uumbaji wake. Na ndiyo maana utaona MUNGU ameweka kanuni na taratibu za kufuata na maagizo ya nini kifanyike ili Mwanadamu akamilishwe. Maagizo hayo, na taratibu hizo na kanuni hizo ni pamoja na kumwani YESU KRISTO kama BWANA na Mwokozi.
Ukizishika kanuni hizo, na taratibu hizo na maagizo hayo basi unakamilishwa kwa kujazwa ROHO WA MUNGU. Ukishajazwa huyo ROHO MTAKATIFU basi wewe umbwaji wako unakuwa umekamilika na hapo unakuwa mtoto wa MUNGU nawe utaishi milele kama MUNGU katika dunia mpya yenye mema pekee.

Adamu baada ya kuumbwa, uumbaji wake ulikuwa haujakamilika sababu hakuwa amejazwa ROHO MTAKATIFU.

Uumbwaji wa Adamu ulikuwa ni phase one, yaani ile ilikuwa ni hatua ya kwanza ya uumbwaji. Ili aingie phase two ya uumbwaji ilikuwa ni lazima kwanza afaulu kuwa "mtiifu" sababu kwa kanuni za MUNGU, mtu akiwa mkaidi hawezi kuingia phase two ya uumbwaji. Yaani hii ROHO YA MUNGU haiwezi kukaa ndani ya mtu "mkaidi".

Nitakupa mfano mdogo sana. Mwili wa Binadamu ni kama vessel, yaani chombo kinachoweza kuhifadhi kitu ndani yake. Na ROHO WA MUNGU ni kama "moto". Sasa basi Mwanadamu akiwa "mtiifu" kwa MUNGU, mwili wake unakuwa imara na utaweza kujazwa hiyo ROHO YA MUNGU ambayo ni sawa na "moto". Lakini Mwanadamu akiwa "mkaidi" kwa MUNGU, mwili wake unakuwa dhaifu hivyo huyo ROHO WA MUNGU hawezi kukaa ndani ya chombo dhaifu sababu chombo hichi dhaifu kikiwekewa "moto", kitateketea na kuungua.

Hivyo basi ndiyo maana utaona kuwa MUNGU alihitaji kwanza Mwanadamu awe MTIIFU ili akamilishwe kiuumbaji.

Ndugu yangu Kiranga nafikiri kwa maelezo hayo utakuwa umeelewa kuwa MUNGU yupo na kwanini dunia ipo kama ilivyo na ni nini mpango wa MUNGU kwako.
Ni rahisi sana, uwe mtiifu uingie phase two ya uumbwaji na uishi milele kwa raha mustarehe au;
Uwe "mkaidi" na ufe kifo cha milele.

Uamuzi ni wako, kifo au uzima.
 
Kuna mambo mengi ambayo mwanzo hayakuthibitika lakini baadae yakathibitika kwamba yapo. Kama umesoma comments zangu toka mwanzo nimetoa mfano.

_Kama kitu hakijathibitishwa haimaanishi hakipo, kikithibitishwa kinaweza kuwepo au kisiwepo. Kusema kipo au hakipo bila uthibitisho ni imani.
Mkuu mbona unashindwa kujibu swali ninalokuuliza ?
 
Kifalsafa hii hoja ni " A Priori fallacy".

Umeanza na jibu la uongo. Halafu mzigo wa kuthibitisha unawapa wengine.

Ni sawa na mimi nikuambie hapa unajibizana na Jeff Bezos tajiri mkubwa, bilionea wa Kimarekani. Mimi ni Jeff Bezos.

Ukibisha kosa si langu, kosa ni lako uliyeshindwa kuthibitisha mimi ni Jeff Bezos bilionea wa Kimarekani.

Yani nasema kitu cha uongo ambacho hakiwezi kuthibitishika, halafu mzigo wa kuthibitisha nakupa wewe.
Hata wewe huwa unatupa Sisi mzigo wa kuthibitisha yupo.
 
Back
Top Bottom