TB Joshua hakuwahi kubatizwa wala kumpokea Yesu! Nimeshangaa sana

Kwa nini unaweka umuhimu kwenye kuamini, ikiwa mtu yeyote anaweza kuamini lolote, la ukweli au uongo?

Mimi sitaki kuamini, nataka kujua na kuelewa.
Ukitaka kupata ukwel wa haya mambo ya kiiman usiegemee kitabu kimoja tu Cha din usichokielewa kutoka kwenye biblia utaelewa Zaid ukisoma Quran vtabu vya kiyahudi , kihindi , kichana na Iman nyingne Kama umesoma vyote unayo haki ya kutoamn uwepo wa Mungu , vitabu vyote vina dhumun moja Ila vinakuwa kamili vinapokuwa vyote kwa pamoja
 
Mkuu, mimi nimesoma mpaka na ma Buddhist Monks walikuwa wanaoeleka watu South Africa, akaenda rafikinyangu Mshana Jr. Mimi monk alitaka kunipeleka ama Thailamd ama Malaysia.

Nimesoma na ma Jehovah Witness makao makuu yao New York City miaka miwili. Biblia kwetu nibkama maji tunasoma kika siku.

Hivyo vitabu hakuna kitabu cha dini kubwa ambacho sijasoma.

Nimesoma Rig Veda, Bhagavad Gita, Dhammapada, The Uppanishads, The Tibetan Book if The Dead, The Rgyptian Book if The Dead, Quran, Agamas, Tanakh, Talmud, Dao De Jing, The Philosoohy of Religion : An Anthology" et cetera, et cetera.

Kwa hilo la kusoma vitabu vingi huwezi kunilaumu.

Kuna wakati najadiliana na watu hapa JF kwa level ndogo ya Biblia na Quran kwa sababu sijaona wengi wa kujadiliana nao Bhagavad Gita.

Na kote huko, hakuna aliyeweza kuhakikisha uwepo wa Mungu.
 
Ndugu mm din yangu Ni Astra Boyd projection (high level of meditation) din hii imenidhibitishaia viumbe vingi nisvyoweza ona kwa macho na uwezo mkubwa ulio fichwa ndan ya miil yetu(gereza) jarbu kufuatilia nakutekeleza, hutakuja kutaka kudhbitshwa Bal utatoa ushuhuda mwenyewe , sema jamii yetu haijui mengi kuhusu haya , ndo maana nilikuomba usome vtabu vya din za Asia chna Japan na Hindi) then ufanyie Kaz utagundua tu
 
Nakwambia nishasoma Bhagavad Gita, the Vedas, Upannishads, Dhammapada,Tripitaka etc.

Tangu 1990s.

Viumbe tusivyoweza ona kwa macho mbona hata kwenye ndoto tunaviona?

Je, hilo linafanya viwepo kweli?
 
Kwani mimi nimekataa huyo mtu hana mzazi? Sijakataa huyo mtu hana mzazi.

Nimekataa mtu wa miaka 60 kuwa na mzazi binti wa miaka 5.

Mimi sijakataa kwamba ulimwengu una mwanzo.

Nimekataa kwamba Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote ndiye chanzo cha ulimwengu.

Sababu ile ile inayonifanya niseme mtoto binti wa miaka 5 hawezi kuwa mama wa mwanamme wa miaka 60, ndiyo ile ile inayonifanya niseme Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hawezi kuwepo na kuwa muumba wa ulimwengu huu.

Sababu hiyo ni logical inconsistency na inherrent contradiction.

Ukikubali Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote yupo, ni sawa na umekubali binti mtoto wa miaka 5 ni mama wa mwanamme wa miaka 60.
Sijaandika kuwa umekataa kwamba huyo hana mzazi.

Nami pia nakatataa mtu wa miaka 60 kuwa na mzazi binti wa miaka 5.

Hata nami sikatai kwamba ulimwengu una mwanzo.

Wewe unakataa kwamba Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote ndiye chanzo cha ulimwengu. Na hiyo ndiyo tofauti yetu kubwa.

Umetumia mfano wa mtoto binti wa miaka 5 kwamba hawezi kuwa mama wa mwanaume wa miaka 60 ili kuhalalisha kuwa Mungu sio
chanzo cha ulimwengu. Sijui kama unamaanisha kuwa Mungu ni sawa mtoto binti wa miaka 5, na ulimwengu sawa na mwanaume wa miaka 60! Hata hivyo siamini kabisa kama Mungu ni mdogo wa umri kuliko ulimwengu.
Hiyo ndiyo sababu halisi inayokuaminisha kuwa Mungu sio chanzo cha ulimwengu, na unaamini pia kuwa hiyo ndiyo sababu ya kutofautiana kimantiki na utata wa asili.

Mfano wako wa mtoto binti wa miaka 5, kuzaa mwanaume wa miaka 60, una mfumo wa sayansi ya kibaolojia. Katika mfumo wa kibaolojia, mzazi ni lazima awe na umri mkubwa na sio vinginevyo.

Tofauti na mfumo wa kibaolojia, pia kuna mfumo wa sayansi ya kiufundi. Mfumo wa kiufundi unahitaji ukubwa wa maarifa na uwezo ili kutengeneza kitu kikubwa kwa kipimo hata kuliko fundi mwenyewe. Huo ndiyo mfumo wa uumbaji. Mungu alitumia mfumo wa kiufundi kutengeneza ulimwengu.

Kwa kuzingatia mifumo hiyo miwili, mfano wako hauna uwiano na uumbaji wa ulimwengu. Mtaji wa mfano wako ni umri, na mtaji sayansi ya kiufundi uwezo na maarifa.
 
Kama vile hoja ya mtoto wa miaka 5 kuwa mama mzazi wa mwanamme wa miaka 60 ilivyo na contradiction, kwamba mama mzazi wa mwanamme wa miaka 60 ni lazima awe mkubwa kuliko huyo mwanamme, ndivyo hoja ya kuwapo Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote ambaye kaumba ulimwengu wenye kuweza kuwa na mabaya, licha ya kuweza kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani ilivyo na contradiction.

Contradiction hii pande zote mbili, kwa mtoto wa miaka 5 ambaye pia ni mama mzazi wa mwanamme wa miaka 60, na kwa Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote ambaye kaumba ulimwengu ambao mabaya yanaweza kutokea, inaonesha habari hizi ni dhana tupu, hazipo katika ukweli.

Na zaidi, uwepo wa ulimwengu unaoruhusu mabaya kutokea ni mutually exclusive na uwepo wa Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote.

Hivyo.

1. Inawezekana awepo Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote, bila ya kuwepo ulimwengu unaoruhusu mabaya kutendeka.

2. Inawezekana ukawepo ulimwengu unaoruhusu mabaya kuwepo, bila ya kuwepo Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote.

3. Haiwezekani viwili hivi, Mungu huyo mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote na ulimwengu huo unaoruhusu mabaya, vyote kuwepo.

4. Kwa uzoefu wetu wa maisha, tunaona ulimwengu unaoruhusu mabaya upo. Ni huu tunaoishi ndani yake kika siku.

5. Hivyo, Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.
 
Back
Top Bottom