TB Joshua hakuwahi kubatizwa wala kumpokea Yesu! Nimeshangaa sana

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
3,385
2,000
Nimekuwa nikifuatilia kifo cha gwiji huyu wa gospo tangu kilipotokea.

Jana nilishangaa hoja ambazo Jumuia ya makanisa ya kikristo ya Nigeria na Jumuia ya makanisa ya kipentekoste kumkataa kabisa TB Joshua kama Mkristo mwenzao.

Alipoulizwa sababu ya kumkataa, mwenyekiti mmoja wa jumuia hiyo aliwahi kusema.

TB hajawahi kubatizwa, au kuonyesha alimpokea Yesu lini na wapi na kwa pastor yupi. Hawakubaliani na agenda yake kuwa yeye Yesu alimalizana naye tangu akiwa tumboni mwa mama yake mimba ambayo ilikaa miezi 15.

Kwa kanuni za kikristo na Kibiblia mtu akiwa na akili timamu ndio anatakiwa amchague Yesu sio tumboni. Lakini pia kwa wengine akiwa mtoto hubatizwa. Lkn sio tumboni na angalau aonyeshe ushahidi wao hawatapata shida kabisa.

Huyu ndiye Gwiji wa injili aliyekuza sekta ya utalii nigeria kwa njia ya injili. Kuna mwaka ulifika ndege ikitua na wazungu 10 nigeria zaidi ya sita wote walikuwa wanaenda SCOAN kulamba upako.
 

capitalpool

JF-Expert Member
Sep 18, 2017
22,254
2,000
screenshot-www.bible.com-2021.06.09-12_46_06.png
Ubatizo wa maji ni udhihirisho wa nje kwamba umempokea Kristo!

Wapo waliompokea Kristo pasipo udhihirisho huo wa nje na kuokolewa!

Ref: Mwizi msalabani aliye mkiri Kristo na kuokolewa pasipo ubatizo wa maji.
 

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
3,385
2,000
Ukipata muda naomba umchunguze na baba askofu gwajima Kama amempokea yesu na kubatizwa ili nijue sadaka yangu jumapil naipeleka kwake au nitombeee tu

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Hahahaha.
Huwa siwafuatilii hadi wawe kwenye headline. Simuamini hivyo kufuatilia habari zake hadi liwepo tukio. Sadaka we toa tu ila amini umempa Mungu kupitia watu wake. Ukigundua ni wasanii pelekea hata yatima au Bibi kijijini asogeze siku uchote na baraka.
View attachment 1813227Ubatizo wa maji ni udhihirisho wa nje kwamba umempokea Kristo!

Wapo waliompokea Kristo pasipo udhihirisho huo wa nje na kuokolewa!

Ref: Mwizi msalabani aliye mkiri Kristo na kuokolewa pasipo ubatizo wa maji.
Mwizi tunajua, ila yeye jamaa wanasema hawajui wala hajasema. Ya tumboni akiwa zygote hiyo wanagoma. Hahaha
 

ujoka

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
2,468
2,000
View attachment 1813227Ubatizo wa maji ni udhihirisho wa nje kwamba umempokea Kristo!

Wapo waliompokea Kristo pasipo udhihirisho huo wa nje na kuokolewa!

Ref: Mwizi msalabani aliye mkiri Kristo na kuokolewa pasipo ubatizo wa maji.
"Enendeni mahali pote mkawafanye mataifa wote kua wanafunzi wangu ,mkiwabatiza kwajina la Baba na Mwana na la Roho Mtakatifu"

"Ukiamini na kubatizwa utaokoka"
Hayo ni maneno ya Yesu Kristo

ila mtake msitake hatujapewa ruhusa ya kujaji ila tumeruhusiwa kuyachunguza maandiko
 

Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
58,302
2,000
Je! vyote visivyoweza kuthibitishwa havipo?
Si vyote visivyoweza kuthibitisha havipo.

Lakini wewe unajuaje hiki hakiwezi kuthibitishwa kwa sababu hakipo na hiki hakiwezi kuthibitishwa lakini kipo?

Mathalani, unajuaje Mungu yupo, hawezi kuthibitishwa tu?

Umeshawahi kufikiri kwamba pengine Mungu hawezi kuthibitishwa kwa sababu hayupo, ni hadithi za kutungwa na watu tu?

Siyo tu Mungu huyu hawezi kuthibitishwa kuwepo, bali pia uwepo wake unakuwa contradicted na hali halisi kwa namna ambayo inaonesha hayupo.

Unaambiwa Mungu ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote.

Aliweza kuumba dunia isiyo na kifo, mabaya, magonjwa, etc.

Lakini hakuumba hiyo, akaumba hii ya ma pandemic na matetemekonya ardhi na ma tsunami.

Kwa nini Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote awe mkatili hivyo kwa viumbe wake?
 

Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
58,302
2,000
La uongo sawa. La kutokuwepo Mungu kisha hajathibitishwa kosa sio la Mungu kosa ni la ukosefu wa wadhibitishaji
Kifalsafa hii hoja ni " A Priori fallacy".

Umeanza na jibu la uongo. Halafu mzigo wa kuthibitisha unawapa wengine.

Ni sawa na mimi nikuambie hapa unajibizana na Jeff Bezos tajiri mkubwa, bilionea wa Kimarekani. Mimi ni Jeff Bezos.

Ukibisha kosa si langu, kosa ni lako uliyeshindwa kuthibitisha mimi ni Jeff Bezos bilionea wa Kimarekani.

Yani nasema kitu cha uongo ambacho hakiwezi kuthibitishika, halafu mzigo wa kuthibitisha nakupa wewe.
 

mazojms

JF-Expert Member
Sep 22, 2017
1,505
2,000
Si vyote visivyoweza kuthibitisha havipo.

Lakini wewe unajuaje hiki hakiwezi kuthibitishwa kwa sababu hakipo na hiki hakiwezi kuthibitishwa lakini kipo?...

Katika karne ya 19 Alfred Wegner alitoa wazo la continental drift, lakini kulingana technologia duni ya wakati huo jumuiya ya wanasayansi duniani ilimcheka na kutupilia mbali wazo lake, But guess what! Katika karne ya 20 his idea was not only proven but also accepted.

Huo ni mfano wa idea ambayo ilikua karibu na uwezo wetu kibinadamu na ilichukua karne moja kuthibitishwa. Now! Think of an idea that is greater than any one of us could ever imagine, the idea that cannot be proven yet, Idea ya uwepo wa Mungu.

Bila uthibitisho inamaanisha Mungu yupo na Mungu hayupo at the same time, na hapa ndipo dini/imani inapo anzia. Kuamini uwepo wa Mungu ni imani, na kuamini kutokuwepo kwa Mungu ni imani pia maana huna uthibitisho wa kutokuwepo kwa Mungu. Je! Ni nani anajidanganya?

Ni bora uamini yupo usimkute kuliko uamini hayupo umkute.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom