TB Joshua: Afungiwa akaunti ya Youtube kwa 'kuwaponya watu wa mapenzi ya jinsia moja'

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,314
33,108
_118080632_73928d32-9c7b-45a4-b34d-29d5295a6404.jpg

Akaunti yake ya YouTube ilikuwa na wafuasi milioni 1.8.
YouTube imesimamisha akaunti ya mhubiri maarufu wa Televisheni wa Nigeria TB Joshua juu ya madai ya matamshi ya chuki.
Shirika moja la kutetea haki liliwasilisha lalamikoa baada ya kukagua video zisizopungua saba zikimuonesha mhubiri huyo akifanya maombi ya "kuwaponya" watu wa mapenzi ya jinsia moja.

Facebook pia imeondoa moja ya machapisho ambayo yanaonesha mwanamke akipigwa kofi wakati TB Joshua akimuombea na kusema anatoa "roho ya pepo".

Mhubiri huyo alisema alikuwa akikata rufaa dhidi ya uamuzi wa YouTube. Akaunti yake ya YouTube ilikuwa na wafuasi milioni 1.8.
TB Joshua ni mmoja wa wainjilisti wenye ushawishi mkubwa barani Afrika, na wanasiasa wakuu kutoka bara zima ni miongoni mwa wafuasi wake.

Kwanini akaunti yake imefungwa ?
Shirika la Open Democracy lenye makao yake nchini Uingereza liliwasilisha malalamiko baada ya kukagua video saba zilizochapishwa kwenye idhaa ya YouTube ya TB Joshua Ministries kati ya 2016 na 2020, ambayo inaonysha kuwa mhubiri huyo anafanya maombi "kuponya" watu wa mapenzi ya jinsia moja.

Msemaji wa YouTube aliambia OpenDemocracy kwamba akaunti hiyo ilifungwa kwa sababu sera yake "inakataza maudhui ambayo yanadai kwamba mtu ni mgonjwa wa kiakili, anaugua, au ni duni kwa sababu ya ushirika wao katika kikundi kinacholindwa pamoja na mwelekeo wa kijinsia".

Ujumbe kwenye akaunti ya Facebook ya TB Joshua Ministries uilisema: "Tumekuwa na uhusiano mrefu na wenye mafanikio na YouTube na tunaamini uamuzi huu umefanywa kwa haraka."

Video hiyo inaonyesha nini?​

Video hiyo ni ya kipindi cha maombi cha mwanamke anayeitwa Okoye, iliyopeperushwa kwanza mnamo 2018. Ndani yake TB Joshua anampiga makofi na kumsukuma Okoye na mwanamke asiyejulikana kama mara 16 hivi na kumwambia Okoye: "Kuna roho inakusumbua imejipandikiza ndani yako. Ni roho ya mwanamke," openDemocracy inaripoti.

Video hiyo ambayo ilitazamwa zaidi ya mara milioni 1.5 kabla ya akaunti ya YouTube kuishusha, baadaye inamuonesha akishuhudia mbele ya mkutano kwamba "roho ya mwanamke" ilikuwa ikiharibu maisha yake lakini alikuwa ameponywa baada ya maombi ya muhubiri huyo. Anatangaza kwamba alikuwa ameacha kuwa na "mapenzi" kwa wanawake na "sasa nina mapenzi kwa wanaume".

TB Joshua ni Nani?​

Ni Mwanzilishi wa kanisa la Synagogue, Church of All Nations na mmoja wa wahubiri maarufu wa Nigeria.
Makumi ya maelfu ya watu wanahudhuria huduma zake za kila wiki katika jiji la Lagos, Nigeria.

_118084310_fa918928-c417-49d8-b8fc-9e895ae917bb.jpg

Kupanda kwa umaarufu wake mwishoni mwa miaka ya 1990 kuliwiana na mlipuko wa vipindi vya "miujiza" vilivyofanywa kwenye Runinga ya kitaifa na wachungaji mbali mbali.

TB Joshua wakati mwingine hukejeliwa kwa kukosa 'umahiri' wenzake katika vikao vya 'uponyaji' -hafla za maombi makali ya kuondoa 'pepo'.

Huduma yake ya injili inadai kuweza kutibu kila aina ya matatizo yakiwemo maradhi kama vile ya Ukimwi na huwavutia watu wengi kutoka sehemu mbali mbali za dunia.

Anajulikana kama "Nabii" kwa wafuasi wake na Bwana Joshua anaendesha kituo cha runinga cha Kikristo Emmanuel TV na mara nyingi huzuru Afrika, Marekani, Uingereza na Amerika Kusini.

Mnamo 2014, kanisa lake moja lilianguka, na kuua watu wasiopungua 116, wakiwemo Waafrika Kusini wengi. Mahakama moja ya Lagos ilisema "kanisa lake lilikuwa na hatia kwa sababu ya utepetevu na jinai " lakini hakuwahi kufunguliwa mashtaka yoyote.

Je ni mara ya kwanza anapigwa marufuku?
Mnamo Mei 2004 Tume ya Kitaifa ya Utangazaji ilipiga marufuku vituo vya Televisheni kuonesha vipindi vya wachungaji wakifanya miujiza kwenye runinga isipokuwa ikiwa imeidhinishwa.

Kulikuwa na madai kwamba baadhi ya miujiza hiyo ilikuwa bandia na ilifanywa na waigizaji. Vituo vya Televisheni viliondoa programu za wachungaji hao ili kuepuka leseni zao kufutwa au kupigwa faini na NBC.

Lakini wakati vifaa vya kurusha matangazo bila kulipia(Ving'amuzi) viliposhuka gharama na watu wengi Nigeria kumudu kuvinunua ,Wahubiri hao walianzisha vituo vya kuendelea kupeperusha vipindi vyao vya 'miujiza'.

Wanatangaza na vifaa vya kisasa na wana vituo maalum vya watoa huduma kupitia runinga ya satelaiti barani Afrika, wakionesha shughuli za makanisa na wachungaji mfululizo . Ingawa bado vipo chini ya usimamizi wa NBC, vituo hivyo viliruhusiwa kuendelea kupeperusha matangazo hayo.

Chanzo. BBC SWAHILI
 
Kawaida ya wazungu.wakishaona maslahi yao yanatibuliwa watafanya juu chini wakukomeshe.
Hiyo iwe open kwamba ni taasisi ya kutetea mashoga na wasagaji
YouTube kumejaa video kibao wanaume kwa wanaume wakioana
Wanawake kwa wanawake wanaoana.
Kwanini wakereke wakiponywa??

Nlishawahi shuhudia mkaka mmoja shoga kutoka Tanzania akipona na kurudiwa na fahamu zake na kuanza kushuhudia alivokuja anafanya ushoga n kujutia.alikuwa maarufu DSM na arusha

Shetani hawezi mshinda Mungu!!
 
zitto junior
Njoo huku kuna watu wanawasema wazungu.
Unajua waafrika tuache kulia lia ile ni kampuni binafsi na ina virtues zake kwanini na sisi tusije na social media zetu kama wachina tu!!

Chanjo tuwalalamikie, Youtube tuwalalamikie na matusi juu kwani kama msimamo wao hakuna anayejua? Hili ni funzo kwamba ni lazima tuwe na vitu vyenyewe tuache kulalama kwa vitu visivyo vya kwetu.

Funny enough tunapokea misaada zinazotokana na kodi za mashoga, tunapokea madawa kutoka nchi inayosupport ushoga, na hata biblia za kiingereza KJV zimetafsiriwa kwa amri ya mfalme James aliyekua shoga. NIV bible (inayotumika zaidi) imetafsiriwa na Harper Collins/Zondervan taasisi inayosupport ushoga, premier league wanavaa armband za ku support ushoga ila sijaona watu wakisusa kuangalia.

Ni hivi waafrika tuanzishe vitu vyetu wenyewe ilo tujiwekee masharti yetu kulia lia na kejeli hku kesho mnachukua misaada yao haiwezi badili kitu. Tuwe kama wachina tu ndio suluhu
 
Haya mashirika ya kutetea haki za binaadamu yanavuka mipaka, hao waliokua wanaombewa kwa TB Joshua walikwenda wenyewe bila kulazimishwa, na walikwenda kwa sababu za kiimani na sio kwa sababu za kisiasa or whatsoever

Mimi nadhani ifike mahali haya mashirika yatambue kwamba moja ya haki za binaadamu ni dini/imani au uhuru wa kuamua, mtu yupo huru kuchagua anachokitaka

Hao mashoga wamekaa kwenye ushoga na imefika mahali hawaoni faida ya ushoga wana haki ya kutafuta solution ya kutoka kwenye ushoga,

Ina maana hayo mashirika hayataki watu waache uovu? Hata kama hawataki lakini wana haki ya kuamua aina ya maisha wanayoyataka
 
Unajua waafrika tuache kulia lia ile ni kampuni binafsi na ina virtues zake kwanini na sisi tusije na social media zetu kama wachina tu!!

Chanjo tuwalalamikie, Youtube tuwalalamikie na matusi juu kwani kama msimamo wao hakuna anayejua? Hili ni funzo kwamba ni lazima tuwe na vitu vyenyewe tuache kulalama kwa vitu visivyo vya kwetu.

Funny enough tunapokea misaada zinazotokana na kodi za mashoga, tunapokea madawa kutoka nchi inayosupport ushoga, na hata biblia za kiingereza KJV zimetafsiriwa kwa amri ya mfalme James aliyekua shoga. NIV bible (inayotumika zaidi) imetafsiriwa na Harper Collins/Zondervan taasisi inayosupport ushoga, premier league wanavaa armband za ku support ushoga ila sijaona watu wakisusa kuangalia.

Ni hivi waafrika tuanzishe vitu vyetu wenyewe ilo tujiwekee masharti yetu kulia lia na kejeli hku kesho mnachukua misaada yao haiwezi badili kitu. Tuwe kama wachina tu ndio suluhu
Watu hawalalamika kwa sababu hao ni wazungu bali wanalalamikia hayo baadhi ya matendo hata kama yangekuwa yanafanywa na Wahindi.
 
Watu hawalalamika kwa sababu hao ni wazungu bali wanalalamikia hayo baadhi ya matendo hata kama yangekuwa yanafanywa na Wahindi.
The point is lawama zimekua nyingi kwa kila kitu cha mzungu si muanzishe chenu!!

Utaskia wazungu wanaangalia maslahi yao cjui wanatulazimisha ushoga n.k it is simple anzisha chako achana na vya wazungu kuanzia mpira mpaka misaada hadi media zao.

Kingine si kweli mnapinga vitendo sio wazungu!! Brazil inaongoza kwa watu kuingiliana Kinyume na maumbile for both girls and men ila umewahi ona thread humu.

Thailand inaongoza kwa mashoga duniani na transsexuals ambao ni almost 10% ya wananchi wote ila umewahi ona thread humu kuwakosoa?

Huyo TB Joshua kma ana jeuri asiombe radhi na afute akaunti zote kwenye social media za mabeberu anything less than that ni mnafiki tu kama wana JF
 
Mkuu hata afrika mashoga wapo hatutoi lawama kwa wazungu kwa sababu tu kuna mashoga, kama Thailand wangekuwa wanafanya kama wazungu ungeona lawama pia.
 
Mkuu hata afrika mashoga wapo hatutoi lawama kwa wazungu kwa sababu tu kuna mashoga, kama Thailand wangekuwa wanafanya kama wazungu ungeona lawama pia.
Hivi unafahamu Thailand wanaingiza mabillion kila mwaka sababu ya sex tourism yaani watu wanatoka mataifa mengi kwenda kujivinjari na mashoga/Kathoeys wa Thailand.

Ila sijawahi ona mkitoa povu kwa wa Asia ila comments zenu humu mtadhani wazungu ndio mashetani kuliko race zote.

Hata kubadili jinsia ni bei rahisi zaidi Asia kuliko Ulaya au marekani!! Kwahiyo kma kuna watu wachafu basi ni South East Asia na sio wazungu!!

Tuache chuki zisizo na tija
 
Bado upo mbali sana na wanachokilalamikia watu humu, hiki walichofanya wazungu wako kwa TB Joshua si sawa na hicho unachokiongelea.
 
Bado upo mbali sana na wanachokilalamikia watu humu, hiki walichofanya wazungu wako kwa TB Joshua si sawa na hicho unachokiongelea.
Mada za wazungu JF zimezidi kila lawama wazungu.... embu tuache conspirancy theories na inferiority complex.

China wana social media zao huko hta FB inapigwa pini tu na maisha yanasonga..... Wana chanjo zao, wana simu zao n.k sasa lini wataanza kulalamika kufungiwa akaunti na mabeberu?

Wazungu misimamo yao inafahamika ya haki sawa kwa wote mpaka mbwa ana haki sawa na ww so kelele za nini. Usipost content ya kudhalilisha mnyama au shoga au mtoto n.k they take it serious.

Kama huwezi anzisha social media yako... Nakumbuka kuna lecture za bure zilitolewa na vyuo vya US yaani koz nzima unasoma bure online. Ila kiziwi mmoja alidai inawabagua sababu hazina subtitles kwa chini. Zile kozi zilifungiwa na kulikua navideo zaidi yaelfu 10.

So wenzetu wapo assertive sana na haki sio ushoga tu kama mnavyotaka watu waamini humu.
 
Ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha wazungu manina zao..... Huwa wana mambo ya kichoko.

Humo online kuna mavideo ya hovyo huwa hawahangaiki nayo ila sio wasikie unawazingua mashoga.

Sasa jamaa amewaponya wao wanakataa nini!

Sent using Jamii Forums mobile app
Wanaharakati wapo wapi wampiganie TB Joshua. Nilidhani uhuru wa vyombo vya habari na kutoa maoni hauna mipaka.
 
Mada za wazungu JF zimezidi kila lawama wazungu.... embu tuache conspirancy theories na inferiority complex.

China wana social media zao huko hta FB inapigwa pini tu na maisha yanasonga..... Wana chanjo zao, wana simu zao n.k sasa lini wataanza kulalamika kufungiwa akaunti na mabeberu?

Wazungu misimamo yao inafahamika ya haki sawa kwa wote mpaka mbwa ana haki sawa na ww so kelele za nini. Usipost content ya kudhalilisha mnyama au shoga au mtoto n.k they take it serious.

Kama huwezi anzisha social media yako... Nakumbuka kuna lecture za bure zilitolewa na vyuo vya US yaani koz nzima unasoma bure online. Ila kiziwi mmoja alidai inawabagua sababu hazina subtitles kwa chini. Zile kozi zilifungiwa na kulikua navideo zaidi yaelfu 10.

So wenzetu wapo assertive sana na haki sio ushoga tu kama mnavyotaka watu waamini humu.
Mkuu wazungu hakuna wasipolalamikiwa hata huyo mchina anasumbuana nao hata muarabu huko nae ana ya kuongea kuhusu huyu mzungu hivyo ni ngumu sana kuwatetea hawa watu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom