TAZARA yazidi kudorora kwa huduma mbovu za treni

Not_Yet_Uhuru

JF-Expert Member
Oct 11, 2010
1,304
431
Wadau wana JF!

Nchi yetu kila pahala ni rojo..hata mashirika ya ubia na nchi jirani tumeishia kuvuruga tu, uongozi mbovy!

Habari zinazovunjika (breaking news) toka kwa wasafiri watumiao reli ya TAZARA ni kuwa, treni ya Tazara imefanyia watu uhuni, abiria wanalalamika wamelala sakafuni toka saa 5 asubuhi waliporipoti, treni ilitakiwa kuondoka toka saa 7 mchana, haikusafiri, uongozi ukakatoa udhuru kuwa safari ni saa 11, abiria wavumilie tu, napo saa 11 jioni haikusafiri, wakaweka matangazo tena na udhuru kuwa safari ni saa 3usiku haikusafiri, hadi sasa 4.35usiku, watoto na wamama wamechoka wamelala sakafuni wanalalama

Source: Mdau wangu aliyepo safari hiyo na watoto, toka saa 5asubuhi.

Hiyo ndiyo maisha bora chini ya Magamba, Ma-CCM yaliyofilisika!
 
station gani hiyo? Tazara ni majanga, utakuta kichwa hakina mafuta hapo.. Kuna siku tulikaa masaa 8 nilipo uliza nikaambiwa mafuta hakuna walikuwa wanasubiri makusanyo wakanunue kurasin baada ya kampun kugoma kuweka mafuta....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom