Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,141
- 18,769
Nawashangaa sana watu wa TAZARA. Wanakubali kufiwa na shirika mikononi na siku zote kuwa na mikakati midogo sana ya kuifufua kampuni (mediocre strategies). TAZARA wanahitaji kufikiria kikubwa - think big - ikiwa wanataka kuendelea kuwapo.
Kwa mfano, umbali wa reli ya TAZARA toka Dar hadi Mbeya ni km 860. Treni za kasi za kampuni ya DB ya Germany zinazosafiri kati ya nchi ya Germany, Ufaransa, Belgium na Uswisi, spidi yake ya wastani ni km 250/hr, lakini zinaweza kwenda hadi spidi ya 300km/hr.
Kwa hiyo ikiwa reli ya TAZARA ambayo ni "heavy gauge" ikiboreshwa kutumia umeme na kuondoa kona kali, TAZARA watakuwa na uwezo wa kufanya safari kati ya Dar es Salaam na Mbeya kwa muda wa saa 3, kutia ndani na kusimama vituo vikubwa vya Ifakara na Makambako.
Gharama ya maboresho hayo ya TAZARA kufikia kiwango hicho hayawezi kufikia gharama ya kujenga SGR kati ya Dar na Morogoro. Yatafanya soko la TAZARA likue sana. Na nikweli safari za ndege Dar - Mbeya zitakosa soko, lakini si ajabu. Pia TAZARA wakifanya hivyo itapunguza sana utitiri wa mabasi njia ya Dar-es-Salaam hadi Mbeya. Watu wa Dar - Iringa au Dar- Songea wanaweza kuwa wanapanda mabasi toka Makambako.
Inawezekana, suala ni mipango tu, labda ubia na wachina kwa mradi kama huu ili kuinusuru TAZARA ambayo bila mkakati mzito itakufa. Think big TAZARA, acheni mipango ya maboresho ya kipwagu na pwaguzi, haitawapeleka popote. TAZARA wanaweza pia kufikiria kuendeleza reli hii kwenda Kyela na Malawi toka pale Vyawa (Mbozi) - ukifikiria suala la kupatikana mafuta ndani ya ziwa Nyasa.