Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,272
- 21,448
Labda Wakuu mna jibu. Kuna msisimko sana na Tanzania kujenga reli ya kati kuwa standard gauge kwa gharama kubwa na kudhani kwamba itakuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo. Labda kweli. Lakini swali ninalojiuliza ni kwamba, TAZARA ilijengwa kama standard gauge na kufunguliwa mwaka 1975. Hata hivyo kila siku tunasikia juu ya matatizo ya TAZARA, pamoja na kuwa standard gauge. Kumbuka TAZARA ni reli ambayo unaweza kuunganisha hadi South Afrika (ndio maana kuna treni ya utalii inakuja Dar toka Cape Town), lakini bado imefeli. Kufeli kwa TAZARA kunatia ndani;
- wasafirishaji wa mizigo kwenda Mbeya, Malawi, Zambia na DRC bado kupendelea usafiri wa malori badala ya TAZARA
- Abiria wa mikoa ya kusini, hususa Mbeya, bado wanapendelea kupanda mabasi badala ya treni