TAZARA nako hakujatulia ufisadi kila kona | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TAZARA nako hakujatulia ufisadi kila kona

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ochu, Sep 5, 2008.

 1. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #1
  Sep 5, 2008
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Vigogo TAZARA wasimamishwa kwa tuhuma...

  2008-09-05 09:18:17
  Na Thobias Mwanakatwe, PST, Mbeya

  Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara), Clement Muya na msaidizi wake, Magreth Banyikwa na Meneja Masoko, Pondani Mwanza, wamesimamishwa kazi kwa tuhuma za ubadhirifu lililosababishia hasara kubwa shirika hilo.

  Hatua hiyo imechukuliwa na bodi ya Tazara iliyokutana hivi karibuni kujadili uendeshaji wa shirika hilo.

  Katika mabadiliko hayo bodi imemteua, Henry Chipeo, kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji.

  Akizungumza na wafanyakazi wa Tawi la Mbeya jana, Chipeo alisema kazi inayofanyika sasa ni kuchunguza viongozi waliosimamishwa ili kuanza hatua za kuwafikisha mahakamani.

  ``Kitakachofanyika sasa ni uchunguzi wa kina kwa tuhuma zinazowakabili wote waliohusika na wizi huo ili wachukuliwe hatua za kisheria,``alisema
  Akifafanua Chipeo alisema kutokana na ubadhirifu wa mabilioni ya Shilingi , hivi sasa Tazara ipo katika hali mbaya na inashindwa kujiendesha, huku treni nyingi zikiegeshwa juu ya mawe.

  ``Utakuta kwa mfano mteja analipia fedha Sh.milioni 800 kama gharama za kusafirishiwa mizigo. Lakini badala yake fedha hizo zinaishia mifukoni mwa wakubwa na kufanya mizigo ya watu kurundikana stesheni,``alisema.

  Alibainisha kwamba ubadhilifu wa fedha katika manunuzi ya mafuta ya treni umetia fora Tazara, ambapo wafanyakazi wa kawaida wamekuwa wakishirikiana na viongozi kuiba mafuta kwenye mabehewa.

  Alisema ubadhirifu mwingine unafanyika baada ya viongozi kugushi tiketi na kusafirisha mizigo ya baadhi ya wafanyabiashara na malipo kuchukua wao.

  Chipeo alitaja mbinu nyingine ya ubadhirifu kwamba ilikuwa ni maafisa hao kuwatoza kiasi kidogo wafanyabiashara wanaosafirisha mizigo, kisha kupokea malipo binafsi kwa mlango wa nyuma, hali ambayo imeshusha mapato ya Shirika.

  Alisema inasikitisha kuona Treni zinajaa mizigo na abiria, lakini pesa hazionekani.

  Chipeo alisema viongozi waliofanya ubadhilifu huo arobaini zao zimefika na bodi imekusudia kuwafikisha mbele ya sheria kwa lengo la kuwafilisi.

  Hata hivyo, alisema baada ya vinara wa tuhuma hizo kuondolewa, uongozi umeziba mianya iliyowekwa ya watu kuchota fedha kirahisi.

  Chipeo alisema wafanyakazi ambao walikuwa na mazoea ya kuiba kwa kushirikiana na viongozi sasa wabadilike vinginevyo nao wataenda na maji.

  Alisema kutokana na wizi huo, Tazara inadaiwa Sh 900 milioni, ambazo ni fedha zilizotolewa na wafanyabiashara kwa ajili ya kusafirisha mizigo, lakini zikaishia mifukoni mwa vigogo.

  Pia alisema Shirika limeshindwa kuwalipa wafanyakazi wake mishahara tangu mwezi Julai.

  Alisema wafanyabiashara wamegoma kuikopesha Tazara mafuta, kutokana na madeni yao kutolipwa.

  * SOURCE: Nipashe
   
 2. M

  Masatu JF-Expert Member

  #2
  Sep 5, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wawape wenyewe wachina waiendeshe sie ishatushinda hiyo
   
 3. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #3

 4. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #4
  Sep 5, 2008
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Mkulima kala mbegu....
   
Loading...