TAZARA ipo katika hali mbaya, yashindwa kujiendesha...!

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,222
1,670
Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara) imeshindwa kujiendesha kutokana na mizigo mingi mizito kusafirishwa kwa njia ya barabara.

Baada ya kubaini tatizo hilo, serikali ya Tanzania na Zambia zimekubaliana kuwalipa malimbikizo ya mishahara wafanyakazi wa Tazara na kuweka mikakati ya kuendelea kulipa mishahara ya Mei na Juni, mwaka huu.

Katika makubaliano hayo, serikali ya Tanzania imetoa Sh. milioni 140 kwa ajili ya kulipa malimbikizo ya mshahara wa Februari, mwaka huu, huku serikali ya Zambia italipa mshahara wa Machi, mwaka huu.

Afisa kutoka Dawati la Serikali, Muttarson Magayane, alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.

Alisema pia serikali ya Tanzania imetoa Sh. bilioni 1.5 kwa ajili ya kulipa mshahara wa Aprili, mwaka huu, huku ikiendelea kujipanga kulipa mishahara ya miezi ijayo.

"Tazara ipo katika hali mbaya kwa kuwa mizingo yote ambayo inashushwa katika Bandari ya Dar es Salaam, asilimia 80 inapaswa kusafirishwa kwa njia ya reli, lakini hali ilivyo sasa ni asilimia 5.2 pekee ya mizingo inasafirishwa na reli na kiasi kikubwa kusafirishwa kwa barabara," alisema.

Magayane alisema kutokana na hali hiyo itakuwa ndoto kwa Tazara kujiendesha yenyewe, hivyo serikali zote mbili zimekubali kuinusuru mamlaka hiyo.

Alisema Tazara ilipaswa kusafirisha tani 60,000 kwa mwezi ili kujiendesha, lakini kuanzia Januari, mwaka huu, imesafirisha tani 4,000 pekee kutoka tani 23,000 za Julai, mwaka jana.

Alisema kuporomoka kwa biashara kwa Tazara pia kumechangiwa na ukosefu wa uaminifu ambao unasababisha baadhi ya wateja kulalamika mizigo yao kupotea.

Hata hivyo, pamoja na jitihada hizo, wafanyakazi wa Tazara kwa kauli moja wamesema hawatarejea kazini hadi watakapopata malipo yote ya mishahara yao, lakini pia kuhakikishiwa upatikanaji wa mishahara ya miezi ijayo ukiwamo Mei kwa wakati.

SOURCE: NIPASHE
 
nina mashaka na hii BRT ndani ya miaka kumi na tano itakuwa mabasi yao yoote yameshakufa, mtaambiwa kila mwanachi mwenye basi lenye siti 60 aingize kwenye mwendo kasi
 
halafu katika nnch hiyo wazir wake anataka akae first class kwenye ndege,akiambiwa upande daraja jengne anahairisha safar,wengne wanadai lak 3,aziwatosh,polen sana watanzania wenzangu serekal sikivu inaitaj kusafishwa masikio,maana miez mi4 bila mshahara ni hatar hata kwa mwananch mpandaj wa tren kwan dereva anaweza litupa train lenyewe kwa mawazo ya majukumu
 
BOSI TRAWU KORTINI: Tazara yamfikisha kortini Katibu Mkuu Trawu, E. Kihwele leo kwa kuanzisha mgomo haramu, kuuchochea licha ya wao kuahidi kulipa wafanyakazi.
 
Nataka kukodisha ofice kwenye majengo yao yaliyo wazi bila watumishi.
Wahusika nipeni taratibu za kufuata.
 
Back
Top Bottom