Tazama yanayowakuta watu wa Bukoba kisa Wameelimika na wamechagua Upinzani

instanbul

JF-Expert Member
Jun 26, 2016
11,359
14,089
Siku zote siku zote CCM huwanasa watu wasio na elimu yoyote.

Hebu niwape historia ya Bukoba Kwa ufupi.

Tangu kuanzishwa Kwa mji wa Bukoba mwaka 1890 na Wajerumani wakiongozwa na Emin pasha mji huu ulikuwa vizr Tu kama miji mingi tz Hadi mwaka 1919 walipoondoka.

1920-1961 mji uliendelea kukua Tu huku ukiwa mji wa pili Kwa ukubwa baada ya jiji la mwanza na ukiwa na bandari mbili custom na kemondo na meli kama mv Victoria ,kishimba, Serengeti na baadae MV bukoba .

Kimsingi bukoba vijijin na mjini Yote kulikuwa na maendeleo at least maana watu walizalisha kahawa na ndizi Kwa wingi hivyo wakauza na kupeleka watoto wao shule.Mpaka mkoa wa ziwa magharibi ( kagera) ulikuwa wa pili tz Kwa maendeleo hadi 1979.

Baada ya CCM kushika nchi Kwa sababu wanazozijua wao udororaji wa kiuchumi wa bukoba na mji wenyew wa bukoba umeyumba na kufanya bukoba ibaki vilevile mji mkongwe mpaka Leo.

2000 wanabukoba wakaamua wamchague upinzani kweli bukoba at least ilisonga kidogo kama kuwa na barabara za lami mji mzima ingawa Kwa vikwazo vingi kutoka serikali.

2005 Jimbo likarudi CCM chini ya MH kagasheki . Bukoba ilibaki vilevile tena na bandari ikafungwa kabisa huku wakirumbana wao Kwa wao CCM mpaka billion 18 zilizotolewa na world Bank kujenga mji wa Bukoba hasa stendi ,soko kuu,kashai market na barabara za mji kuziboresha ikaamishiwa miji mingine.

2015 wananchi wa bukoba wakaona hebu wajaribu upinzani ili walao wawaache CCM na migogoro Yao maam wakampa MH Rwakatale. Ni kweli huyu alifaa na nilimuona Sana akilalamika Sana bungeni kuhusu bukoba hasa stendi na soko lake lakin hakusikilizwa Kwa kuwa mpinzani mwishowe amekata tamaa na hagombei tena.

2020 sasa bukoba mjini imebaki na stendi mbovu ,soko bovu na barabara mbovu kuliko zote tz hakuna hata mradi wa UGLSP wala sijui TARURA mji Una mifoleni ya ajabu.

Watu binafsi( wahaya) ndo wanajitahi di kujenga mahoteli nyumba shule nk mpaka sasa mkoa huu Una hospital 2 Tu za serikali nyingine 17 ni za kanisa na watu binafsi.

Mwaka huu wakazi wa mji huu hawajui wachague nini maana CCM na upinzani wametawala bukoba lakin mji unazidi kuchakaa

mgomo%2B%255Bic.jpeg
images%20(14).jpeg
images%20(15).jpeg
images%20(16).jpeg
images%20(17).jpeg
images%20(18).jpeg
FB_IMG_15961743299218063.jpeg
 
Tazameni stendi kuu ya mji mkongwe na mkubwa wa Bukoba.


Cha ajabu na wajumbe wa CCM hutumia hii stendi
FB_IMG_15961743299218063.jpeg
images%20(18).jpeg
images%20(17).jpeg
images%20(16).jpeg
images%20(15).jpeg
images%20(14).jpeg
mgomo%2B%255Bic.jpeg
 
Hivi Mkoa huu ratio ya Christians and Muslims ni ngapi kwa ngapi? Tuanzie hapo Kiongozi......data muhimu kabla ya hukumu
Wakristu ni wengi zaidi zaidi ya 90% huku 75%wakiwa wakatoliki Sana.


Wilaya za wahaya ndo zinawakatoliki wengi Sana ( muleba, Bukoba na misenyi)

Wilaya za wanyambo zina walutheri wengi.


Waislamu hupatikana kata chache kama kamachumu,nshamba,katoro na bukoba mjini( waarabu)
 
Tushawachoka nyie mnadhani maendeleo ni stendi tu mbona ubungo stendi chafu imejaa madimbwi na vyoo vichafu havina maji tuache kukalili/ ...Ubunge kama kawaida tunawapa Chadema tena Chief maana kuanzia 2015-2020 Chadema wamejenga bandari ya custom ya kisasa na mabarabara kibao bila kusahau daraja la Bukoba club , Bukoba ndani ya chadema imesonga sana ubunge tunampa Chief. tena instanbul
 
Tushawachoka nyie mnadhani maendeleo ni stendi tu mbona ubungo stendi chafu imejaa madimbwi na vyoo vichafu havina maji tuache kukalili/ ...Ubunge kama kawaida tunawapa Chadema tena Chief maana kuanzia 2015-2020 Chadema wamejenga bandari ya custom ya kisasa na mabarabara kibao bila kusahau daraja la Bukoba club , Bukoba ndani ya chadema imesonga sana ubunge tunampa Chief. tena instanbul
Lakin walau Dar wanajenga stendi mpya pale mbezi.


Bukoba hata dalili hakuna
 
Kwani wewe unataka tuwape kura CCM, kagasheki kakaa hapo bungeni miaka 10 stendi imemshinda pia sisi maisha sio stendi tu CCM acheni chokochoko ubunge tunampa chief Kalumuna
 
Bukoba kuko vizuri tatizo ni stendi tu....ccm acheni chokochoko.
Kuko vzr wapi.
Tazama barabara za katikati ya mji ni chafu, taa haziwaki, hakuna traffic lights, soko bado la mabati. Daladala zilistopishwa nk.


Halafu Mimi sina chama chochote Mimi nataka kuona Bukoba ikibadilika
 
Ndugu Zangu Mjifunze Kuchagua
Kosea Kuoa Ila Siyo Kuchagua
Ukikosea Kuoa Mke Mnaweza Kuachana Muda Huo Huo
Lakini Ukikosea Kuchagua Hadi Miaka 5
Kupanga Ni Kuchagua
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
 
Kuko vzr wapi.
Tazama barabara za katikati ya mji ni chafu, taa haziwaki, hakuna traffic lights, soko bado la mabati. Daladala zilistopishwa nk.


Halafu Mimi sina chama chochote Mimi nataka kuona Bukoba ikibadilika


We tulia tu Bukoba pazuri tu, huwezi fananisha na miji mingine kama mikoani.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom