Tazama yanayowakuta watu wa Bukoba kisa Wameelimika na wamechagua Upinzani

Siku zote siku zote CCM huwanasa watu wasio na elimu yoyote.

Hebu niwape historia ya Bukoba Kwa ufupi.

Tangu kuanzishwa Kwa mji wa Bukoba mwaka 1890 na Wajerumani wakiongozwa na Emin pasha mji huu ulikuwa vizr Tu kama miji mingi tz Hadi mwaka 1919 walipoondoka.

1920-1961 mji uliendelea kukua Tu huku ukiwa mji wa pili Kwa ukubwa baada ya jiji la mwanza na ukiwa na bandari mbili custom na kemondo na meli kama mv Victoria ,kishimba, Serengeti na baadae MV bukoba .

Kimsingi bukoba vijijin na mjini Yote kulikuwa na maendeleo at least maana watu walizalisha kahawa na ndizi Kwa wingi hivyo wakauza na kupeleka watoto wao shule.Mpaka mkoa wa ziwa magharibi ( kagera) ulikuwa wa pili tz Kwa maendeleo hadi 1979.

Baada ya CCM kushika nchi Kwa sababu wanazozijua wao udororaji wa kiuchumi wa bukoba na mji wenyew wa bukoba umeyumba na kufanya bukoba ibaki vilevile mji mkongwe mpaka Leo.

2000 wanabukoba wakaamua wamchague upinzani kweli bukoba at least ilisonga kidogo kama kuwa na barabara za lami mji mzima ingawa Kwa vikwazo vingi kutoka serikali.

2005 Jimbo likarudi CCM chini ya MH kagasheki . Bukoba ilibaki vilevile tena na bandari ikafungwa kabisa huku wakirumbana wao Kwa wao CCM mpaka billion 18 zilizotolewa na world Bank kujenga mji wa Bukoba hasa stendi ,soko kuu,kashai market na barabara za mji kuziboresha ikaamishiwa miji mingine.

2015 wananchi wa bukoba wakaona hebu wajaribu upinzani ili walao wawaache CCM na migogoro Yao maam wakampa MH Rwakatale. Ni kweli huyu alifaa na nilimuona Sana akilalamika Sana bungeni kuhusu bukoba hasa stendi na soko lake lakin hakusikilizwa Kwa kuwa mpinzani mwishowe amekata tamaa na hagombei tena.

2020 sasa bukoba mjini imebaki na stendi mbovu ,soko bovu na barabara mbovu kuliko zote tz hakuna hata mradi wa UGLSP wala sijui TARURA mji Una mifoleni ya ajabu.

Watu binafsi( wahaya) ndo wanajitahi di kujenga mahoteli nyumba shule nk mpaka sasa mkoa huu Una hospital 2 Tu za serikali nyingine 17 ni za kanisa na watu binafsi.

Mwaka huu wakazi wa mji huu hawajui wachague nini maana CCM na upinzani wametawala bukoba lakin mji unazidi kuchakaa

View attachment 1522239View attachment 1522240View attachment 1522241View attachment 1522242View attachment 1522245View attachment 1522246View attachment 1522247
Haka kamanispaa ndio kanalinganishwa na Moshi kweli????

BTW mkulu hana hoja hiyo hoja nyepesi sana ua kuihukumu CDM

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom