TAzama unavyoweza kuwa tajiri kwa muda mfupi.

Sitachoka

JF-Expert Member
Nov 17, 2011
3,030
1,303
Habari wanajamii!

Nawatafuta watu wenye mitaji ya kuanzia kama milioni 3 hivi tufanye nao biashara.

Biashara yenyewe iko namna hii ni kuzalisha umeme kwa kutumia machine ya kusaga itakayobadilishwa na kuwa ya kufua umeme kwa kufungiwa moter, nipo eneo moja Mkoani mwanza pembezoni mwa mji ni sehemu iliyo na watu wengi sana kutoka sehemu mbalimbali za nchi wakiwa wamekuja kutafuta eneo hili, kwa bahati mbaya eneo hili hakuna umeme usambazwao na shirika letu la umeme la Tanesco bado haujafika, ingawa kuna mtu mmoja yupo sehemu hii ikijaribu kutoa huduma hii maeneo haya kwa kutumia machine ya kusaga yenye piston moja ambayo imeelemewa mzigo kwa mahitaji ya wateja kuwa makubwa hivyo kufanya watu kuendelea kukaa gizani


hizi ndizo gharama anazozitoza huyu bwana kwa wateja wake kwa siku

1. Ukihitaji umeme nyumbani kwako balbu moja tsh. 500/=@siku

2. Kwa mwenye salon maeneo haya kama anahitaji hudumu yake anatozwa 3000/=@siku

3. Kwa wenye kumbi labda za kuonyesha video tsh.5000/=@siku

3. Kwa wenye maduka tsh.5000/=@siku kama ana charge na simu

4. Kwa wenye mabaa tsh. 4000/=@siku huruhusiwa kutumia friji kuepusha mashine kuzimika kwa ukubwa wa mzigo

kwa kifupi mahitaji bado ni mengi mno na hudumu iliyopo sasa inalegalega sana kama utalizika na maono yangu ya kufanya nawe mfanyabiasha biashara hii katika eneo ili tafadhari tuwasiliane kwa kuniPM
 
mkuu mwea, hebu jaribu kuwekka technical details n nn kinahitajika, na approximate mtaji unaohitajika n kiasi gani, mashine itafanyaje kazi. unategemea kuzalisha watts ngapi tokana na huo uwekezaji.
 
Umefanyia utafiti wa kutosha khs ufanisi (efficiency) wa hiyo mashine?
 
Kutokana na post yako inaonekana kinachokusukuma (driving force) ni tamaa ya kuwa tajiri haraka. Hiyo siyo attitude ya ujasiriamali. Driving force yako inapaswa kuwa utoaji wa huduma bora mbadala. Utajiri yatakuwa ni matokeo. Fanya uchunguzi wa kina (yakinifu) badala ya ku-copy na ku-paste biashara za wenzako.
 
cha muhimu hapo unatakiwa utoe detail kama umepata kibali toka mamlaka husika cause unaweza fungua leo kesho mamlaka husika wakuja juu halafu tayari umeshawekeza pesa zako. utashika kichwa mpaka basi!!!!!!
 
good business ila una kibali cha kuendesha hiyo biashara ukizingatia hili shirika la usambazaji umeme ni monopoly economy
 
Back
Top Bottom