Tazama tembo wetu wanavyo angamia!! Watanzania tuungane kulaani!!!

Earthmover

JF-Expert Member
Sep 28, 2012
22,492
19,561
Kumbukeni Wantanzania wanyapori ni kiporo chetu cha mwisho kilicho baki bila kujali udini wetu, ukabila wetu, umasikini wetu, itikadi zetu na hata upagani wetu mkikubali na hiki wakiangamize basi KIZAZI CHETU KIMEANGAMIA, bila kujali udini wetu, ukabila wetu, umasikini wetu, itikadi zetu na hata upagani wetu !!!
Wamefagia madini sasa wanafagia hifadhi wakitoka hifadhini watakuja kwako!! UTUMWA WA FIKRA HURITHISHA TAIFA UMASIKINI NA UMASIKINI HURITHISHA UTUMWA WA FIKRA KWA TAIFA!! Tafakari chukua hatua!!!
 
Attachments

  • tanzania_elephants1-14545e465b1a57b62849fda2b985de5216b4e730-s2.jpg
    tanzania_elephants1-14545e465b1a57b62849fda2b985de5216b4e730-s2.jpg
    22.1 KB · Views: 233
Bora hao majangili ni watanzania wenzetu wanajitafutia liziki kuliko wale WAARABU wanaopandisha kwenye ndege TWIGA wetu wazima wazima....SIUNGI MKONO HOJA.
 
Kinana na CCM wanamaliza hawa wanyama kila kukicha na sisi tunapewa t.shirt, kanga na wali tunashangilia kama wehu.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
kati ya watu wajinga kabisa duniani ni WATANZANIA. Wanasiasa wamefanya kila aina ya uchafu tunawaangalia tu.Wanatuchezea,wanafanya wanacho taka,wameiba kila walichokitaka.wazo langu ni kuwa wasomi wote kwa ujumla wetu tujiandikishe tupate idadi kamili ya watu wanaochukia uovu halafu tutangaze mgogoro na serikali na hasa wanasiasa tuwaondoe madarakani.haiwezekani mtu ahusike katika kuiba nyara za serikali anaachwa hivihivi!!
 
Huu ndio mzigo uliokamatwa China, kutoka Tanzania, alafu waziri anaenda kuomba uuzwe ili fedha zitumike kupambana na majangili. Uzumbukuku mwanzo mwisho.
images
 
hapo nimekubali mkuu meno yote hayo sasa hawa askari wanyama poli nao wanakazi gani, du tumekwisha
 
hapo nimekubali mkuu meno yote hayo sasa hawa askari wanyama poli nao wanakazi gani, du tumekwisha
Mkuu, usikubali kwamba tumekwisha, hebu chukua hatua ya kizalendo maana hili ni Taifa letu wote ila kuna wachache wamejaliwa tumbo na tamaa zisizojali utu wala uzalendo....!
 
Kinana na CCM wanamaliza hawa wanyama kila kukicha na sisi tunapewa t.shirt, kanga na wali tunashangilia kama wehu.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

Hili la Kinana limekaaje! Eti anasema yeye sio mtendaji wa moja kwa moja wa kampuni yake, naomba kuuliza "Hivi kama bunduki yangu ikitumiwa na majambazi utasemaje kwamba mimi sihusiki moja kwa moja na kadhia hiyo ya ujambazi?" Jamani tumwogope Mungu, siku si nyingi mtaumbuka Mungu sio mzee.
 
Bora hao majangili ni watanzania wenzetu wanajitafutia liziki kuliko wale WAARABU wanaopandisha kwenye ndege TWIGA wetu wazima wazima....SIUNGI MKONO HOJA.
Watanzania wenzetu wapi wewe??
Yule ni msomali aliejivika utanzania.
 
Huu ndio mzigo uliokamatwa China, kutoka Tanzania, alafu waziri anaenda kuomba uuzwe ili fedha zitumike kupambana na majangili. Uzumbukuku mwanzo mwisho.
images

Ni sawa na Tembo wangapi??
Ifikapo 2020 kutakua hakuna mnyama aitwae Tembo hapa Tanzania
 
Hayo ndiyo marupurupu ya kuiweka ccm madarakani! Hayo yote watanzania mnayataka wenyewe!!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom