Tazama nimegundua njia ya kuacha kutumia nishati ya petroli kuendesha gari...

Johnny Sack

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
8,813
18,793
Hapo tumeweka sumaku kwenye gari kwa mbele huku sumaku nyingine ikiwa kwa mbele hapo kuivuta hilo gari
Gari inakuwa inajivuta yenyewe...wadau mnasemaje?

1078554
 
Mkuu, hapo gari haisogei
Ukitaka kuhakikisha hilo kajaribishe kwenye kigari cha kuchezea watoto

Sijui namna gani rahisi ya kukuelewesha ila
Kuna kanuni moja ya Newton inasema body will remain at rest or in motion if there is no EXTERNAL force actin on it

Kitu kitabaki kimesimama au katika mwendo endapo hakuna kani kutoka nje inayokilazimisha kisogee au kisimame

Hapo kati ya hizo sumaku kuna kani ya uvutano ila hilo gari halitasogea kwa sababu sumaku zote zipo ndani ya hilo gari, yaani kuna force ila sio EXTERNAL force, zote zipo within hilo gari....

Labda lingesogea endapo sumaku moja ingekuwa nje ya gari kabisa, labda kwenye gari jingine au ukutani, hapo force ingekuwa ni external na gari lingesogea kama sumaku zingekua na nguvu ya kutosha
 
View attachment 1078554
Petrol lazima itumike kwa gari itakayokuwa mbele ikiwa na sumaku A kwa ajili ya kuvuta hii ya nyuma yenye sumaku B.

Sumaku zote zikisetiwa katika gari moja lilelile haziwezi kujivuta kwa kuisogeza mbele.

Hata gari zikiwa mbili zilizowekewa sumaku A na nyingine B pia uwezekano wa kusafiri hata kwa umbali wa mita100 ni ngumu.

Aidha zitavutana na kugongana ama magnetic field itapungua kutokana na movement ya gari la mbele jinsi itakavyoendelea kusonga mbele.

Kifupi hiyo nadharia haiwezekani mkuu.
 
Hiyo gari haita sogea hata hatua moja mkuu. Njia bora kabisa ya kufanikisha zoezi unalotaka ni kuchukua fisi wawili wakubwa uwafunge mbele ya gari. Kisha ning'iniza mguu wa mbuzi choma mbele ya hao fisi kwa kutumia mti mrefu. Hakikisha fisi hawaufikii huo mguu kwahiyo watakua wanaukimbiza kwa kasi ya 180 km/h.
 
Hhehee
 
Mkuu, hapo gari haisogei
Ukitaka kuhakikisha hilo kajaribishe kwenye kigari cha kuchezea watoto

Sijui namna gani rahisi ya kukuelewesha ila
Kuna kanuni moja ya Newton inasema body will remain at rest or in motion if there is no EXTERNAL force actin on it

Kitu kitabaki kimesimama au katika mwendo endapo hakuna kani kutoka nje inayokilazimisha kisogee au kisimame

Hapo kati ya hizo sumaku kuna kani ya uvutano ila hilo gari halitasogea kwa sababu sumaku zote zipo ndani ya hilo gari, yaani kuna force ila sio EXTERNAL force, zote zipo within hilo gari....

Labda lingesogea endapo sumaku moja ingekuwa nje ya gari kabisa, labda kwenye gari jingine au ukutani, hapo force ingekuwa ni external na gari lingesogea kama sumaku zingekua na nguvu ya kutosha
Tutaendesha na hayo mawinch?
 
Back
Top Bottom