Mahojiano ya Diamond katika kipindi cha leo tena, amkubali mtoto wa Hamisa kuwa wake

Socw

JF-Expert Member
Aug 27, 2016
1,304
2,582




saa 10:30
washaintroduce kuwa leo watakuwa na diamond. na inaonekana hii interview inasubiriwa sana kwa sababu wamesema wanaungana na clouds tv. sasa hivi zinapigwa ngoma katika kusogeza sogeza muda. now linapigwa dude la young killer ft harmonize.

saa 10:45
inapigwa ngoma ya ben pol..kidume.

saa 10:47
inapigwa ngoma ya joh makini ft. davido. tuendelee kusubiri

saa 10:51
inapigwa nyimbo ya Nandi sijui inaitwaje...nasikia tu moyooo moyoooo...tundelee kuwa wavumilivu wapenda ubuyu wenzangu.

saa 11:03
mahojiano ndo yameanza..

saa 11:03
diamond: ni mimi ndiye huposti kwenye account yangu ya instagram. sijawa maarufu kiasi cha kuajiri mtu kwa ajili ya konipostia.

saa 11:13
anaaanza kutoa maelezo..lakini ameanza kwa kusisitiza kuwa kuwa mtoto siyo wake. na anaanza kama ifuatavyo

saa 11:15
daimond: hamisa tumefahamiana naye kuanzia 2010 na tukawa na mahusiano lakini tukaachana. ilikuwa ni kabla ya kuanza mahusiano na wema.

sasa 11:23
katikati aliingia shetani lakini nikamwambia kuwa nina familia. haya tuliyofaya tubaki siri yetu mimi na wewe. nikampigia nikamuuliza lakini akasema yeye hahusiki. lakini baadaye akaniambia kuwa ana ujauzito wangu. na nikaanza kuilea lakini nikamwambia ninailea kwa sababu kama baba. zari alikuwa akiniuliza nikawa namwambia ni uzushi.

saa 11:28
nilimwambia kuwa mimi kwa namna yoyote siwezi kuachana na zari.

mama yake alinifuata akaniuliza kwa nini siongei na mwanae mimi nikamwambia kuwa mwanao anachukua karibu laki tano kwa wiki, nimemnunulia rav 4 na nimemwambia kuwa atafute mradi mimi nikamsadia.

nilitoka London na nilipofika nikalala na mwanangu

(tunapata breaaaaaaak kidogo)

tunarudi tena....

saa 11:49
diamond: katika maisha hivi vitu vinatokea ila kama mwanaume unatakiwa ujue una solve vipi hayo.

======

Mwanamuziki Diamond Platnumz amemkubali mtoto aliyezaa na na Hamisa Mobeto na amesema jina alilotaka apewe mtoto huyo ni Dylan lakini kwa sababu za kutafuta umaarufu mwanamke huyo alimwita Abdul Nassib.

Amesema Hamisa alimwita mtoto huyo Abdul ambalo ni jina la baba yake mzazi ili iwe rahisi watu kufahamu kuwa mtoto huyo ni wa kwake baada ya kukubaliana kufanya uhusiano wao kuwa wa siri.
"Tulikubaliana na Hamisa Mobeto kuwa ujauzito huo usitangazwe kuwa ni wa kwangu, na alikubali lakini akawa anatangaza.

"Mpaka Mobeto anajifungua, nilikuwa nampa 70k kila wiki, nilimnunulia RAV4 na kabla hajajifungua nilimpa Tsh 7m ya kununua vitu.

"Sio kweli kwamba nilimkataa mtoto kama Hamisa anavyodai, bali alikuwa anatuma watu ili niseme sijamkataa watu wajue kuwa ni wangu.

"Zari anajua kuhusu mtoto wangu na Mobeto na hana tatizo, ila Mobeto anatengeneza mazingira nigombane na Zari kitu ambacho sitafanya.

"Wakati anajifungua nilimpa $3,500, nikamtafutia hospitali binafsi na baada ya kujifungua, nilimuomba mama yangu akamuone mjukuu

"Siku Hamisa Mobeto anajifungua sikuwepo Tanzania na niliporudi nilikwenda kumuona mwanangu na kulala naye hadi asubuhi.

“Mimi jina ninalolitambua ni Dylan hata niliposikia wamemwita Abdul nilisema poa tu lakini akija kwangu nitamwita ninalolitaka mimi kwa sababu nataka aitwe DD (D Square).”Amesema Diamond

Amesema alisikitishwa pia na kitendo cha mwanamke huyo kumualika baba yake katika sherehe ya kutimiza siku arobaini ya mtoto huyo akimdanganya kuwa angekuwepo.

“Walimwalika mzee Abdul na nguo wakampelekea ili ahudhurie, yote hiyo ili mradi tu wapate cha kuzungumziwa mitandaoni,” amesema.

Chanzo: Mpekuzi

===

Mitandao mingine imeandika...

Hatimaye msanii mkubwa wa Bongo Fleva nchini Diamond Platinumz ameamua kusema ukweli kuhusu tetesi zilikuwa kuwa zikisambaa mitandaoni kuhusu ujauzito wa mwanadada video queen maarufu nchini Hamisa Mobeto.Diamond amesema ukweli baada ya kuenea kwa picha na video clips nyingi mitandaoni zikimuonyesha akiwa kitandani na mwanadada .

akiongea katika kipindi cha leo tena Cha clouds tv, Diamond amekiri kuwepo na mahusiano kati yake na Hamisa kipindi cha nyuma na hapo katikati walirudiana ilhali mrembo huyo akijua kuwa Diamond ana familia .

“Mimi na Hamisa tulikutana tangu mwaka 2010, tukawa na mahusiano lakini mahusiano yetu hayakudumu, kipindi icho nilikuwa sijakutana na Wema wala Zari.” akiri diamond “kipindi nipo na zari alianza kunirequest turudiane lakini nilimwambia mimi nina familia tayari,tukaendelea..baada kama ya siku tatu habari zikaanza kusambaa mitandaoni Diamond anatembea na hamisa” amesimulia.

‘Baada kama ya miezi alinipigia simu kuwa ana ujauzito wangu, basi nikamuuliza yeye ameamuaje, nikamwambia sawa ila mimi nina familia yangu , nilikubali na nikaanza kulea ujauzito wangu” amekiri diamond

“Mpaka mimba inakuwa , kila siku alikuwa anapokea si chini ya elfu sabini kwa siku,na hata mimba ilikuwa kubwa nilimnunulia Rav4, na tushakubaliana tukae kimya ,sikuwa tayari kuzungumzia swala ilo kwenye media”

Baada ya kuona maneno yanazidi katika mitandao Diamond aliamua kumwambia ukweli mzazi mwenzie zari na kukiri kosa lakini alimwambia hamisa hana haja aya kumtukana zari na watoto wake maana watoto watachukiana wakati wote ni wake.

Diamond anasema kuwa alikuwa akimuhudumia hamisa, na hata alipoenda kujifungua aliacha zaidi ya mil7 kwa ajili ya shopping ya mtoto na bado akampa ela kwa ajili ya kujifungua, anakiri kuwa ni ujinga wake ndo ulifanya yote yakatokea “familia yangu imetukanwa kwa sababu ya ujinga wangu.. nilitoka uingereza usiku nikaenda kulala na mtoto wangu ”

Diamond anakiri kuwa alikuwa karibu na Hamisa kwa sababu alikuwa anaamini kuwa mtu anapokuwa na tumbo(ujauzito) hapaswi kujisikia vibaya.hata hivyo Diamond ameomba radhi kwa familia yake, watoto wake na mama mzazi wa watoto wake Zari.
 
nipo hapa mbele Kabisa na popcorn zangu......



clouds tunaomba mje mbalance story Kama mlivyotaka kufanya ktk ile story ya Gwajima mpaka bashite akawavamia.... .na hamisa ahojiwe ili aeleze upande wake.. maana kwa Maelezo ya dai hamisa ni shetani wa mguu mmoja ilihali yeye Diamond ni mkosaji tu wa kawaida
 
Ndo kipindi kinaanza....inapigwa nngoma ya eneka.

Update nyingine kufuata.

Ikitokea wasikilizaji tukapewa muda wa kupiga Simu na kumuuliza ' Ndomo ' swali nikipata tu line nitamuuliza hivi ni kweli kwamba ana ' Mkuyenge ' bamia kama ambavyo inasemekana au tunaaminishwa na hasa wale wanaomjua ' Kindakindaki ' na pengine aliowabandua?
 
Kama atathibitisha kuzaa na Hamisa nadhani ndio utakuwa mwanzo wa kuanza kuporomoka kisanii. Watu wengi sana wameumizwa na hili suala. Na wengi sana walimpenda Diamond alivyokuwa na msimamo juu ya Zari. Lakini kuzaa na Hamisa ni kama kumtusi Zari. Binafsi nitakuwa hater wa Diamond endapo atathibitisha kuzaa na Hamisa.
 
Kama atathibitisha kuzaa na Hamisa nadhani ndio utakuwa mwanzo wa kuanza kuporomoka kisanii. Watu wengi sana wameumizwa na hili suala. Na wengi sana walimpenda Diamond alivyokuwa na msimamo juu ya Zari. Lakini kuzaa na Hamisa ni kama kumtusi Zari. Binafsi nitakuwa hater wa Diamond endapo atathibitisha kuzaa na Hamisa.
Then start now. Wamezaa
 
Ikitokea wasikilizaji tukapewa muda wa kupiga Simu na kumuuliza ' Ndomo ' swali nikipata tu line nitamuuliza hivi ni kweli kwamba ana ' Mkuyenge ' bamia kama ambavyo inasemekana au tunaaminishwa na hasa wale wanaomjua ' Kindakindaki ' na pengine aliowabandua?
Haha siamn uyu jamaa inaonekana ana mkuyenge wa maana,,...si kwa kugonga huku na mitoto anayopiga kumlilia aisee huyu dogo anatumia mcongo si kawaida
 
Kama atathibitisha kuzaa na Hamisa nadhani ndio utakuwa mwanzo wa kuanza kuporomoka kisanii. Watu wengi sana wameumizwa na hili suala. Na wengi sana walimpenda Diamond alivyokuwa na msimamo juu ya Zari. Lakini kuzaa na Hamisa ni kama kumtusi Zari. Binafsi nitakuwa hater wa Diamond endapo atathibitisha kuzaa na Hamisa.
Yaani mtu amkatae mwanae kisa tu apendwe na wewe!? Mbona babako hakukukataa wewe ili awafurahishe walimwengu ambao hawakupenda kuzaliwa kwako
 
True I stand with Kiba haumizwi na skendo za mahusiano hata akiachana na madem zake wala huoni mapovu wala kashfa kimya kimya kama jokate pamoja na kuwa wameachana ila bado alimsapoti alipotoa nyimbo yake
Seduce me haijahitaji kiki kufika 5M views ndani ya 18 days, kwakweli kiba na mama yake wanabusara sana sio bi Sandra kila mkwe ye anampokea anakuwa upande wake, domo anapotea so far nyimbo zake week tu zinazima
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom