Tazama Maisha na mali zinavyomuijilia kila mtu duniani kabla ya kufilisika

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,252
21,345
KILA MTU ANAFUNGU LAKE LA UTAJILI KWA WAKATI WAKE

Maisha ni fursa, Maisha ni safari, ili ufike unakokwenda lazima uchague njia sahihi ya kukufikisha.

Maisha huongozwa kwa matamanio!
Utajili na Umasikini vimetenganishwa na Matamanio!
Ili uwe tajiri ni lazima ujuwe kupangilia Matamanio yako!
Utofauti wa mali kati ya mtu na mtu huchangiwa na kufeli kwa mipangilio yenye matamanio( KIPAUMBELE)

kwa mfano:
Watu watatu marafiki waliokuwa na ndoto za utajili baada ya kumaliza shule yao, waliajiliwa pamoja katika ofisi moja kwa mshahara sawa, baada ya mda kutokana na pesa walizochuma /kopa walikuwa huru kila mmoja kufanya MATAMANIO YAKE!

wa kwanza akanunua gari nzuri kwa ajili ya kuwahi kazini kutokana na changamoto ya usafiri,ndoto yake ni kumiliki Gari zuri ikiwa kama sehemu ya mafanikio yake!
wa pili akanunua kiwanja na akaanza kusimamisha mjengo haraka kwa sababu alisikia ushauri kuwa wenye akili wanajenga kwanza!

Watatu yeye kwasababu mama yake alimsomesha kwa kuuza chakula, Alitamani kuboresha biashara iliyomsomesha akaamua kuboresha biashara na mama ake na kufungua duka la vinywaji vya jumla na rejareja huku baadhi ya pesa kidogo akanunua mifugo huko kijijini!
Wote watatu hawa walitimiza Azimio la matamanio yao katika kuufikia utajili!

NINI KILIFUATA BAADA YA HAPO?
Kutokana na mikopo yao! wa kwanza aliyenunua gari alitembelea mwaka mmoja tu akaamua kupaki maana aliandamwa na deni la mkopo huku pesa aliyokuwa akiipokea ikiishia kulipa bima, service, mafuta,parking,kodi na faini za barabarani HADI ile furaha aliyotarajia ikaanza kuyeyuka!

Wa pili aliyenunua kiwanja alifanikiwa kujenga boma lote na bahati mbaya pesa ilimwishia punde baada ya kuweka mbao za kenchi zikalala zikipigwa jua na mvua bila bati!

wa tatu alifanya biashara akapata faida kiasi cha kununua kiwanja na kujenga taratibu kwa faida iliyotokana na biashara iliyosimamiwa na mama yake!

KILICHOENDELEA BAADA YA HAPO
Kwa bahati mbaya sana Bodi na taasisi yao baada ya kuonekana haina faida katika nchi IKAFUTWA NA RAIS WA NCHI HIYO!

KWA MFANO HUU
Ninachotaka kusema ni hivi!

Maisha ni vile unavyotanguliza KIPAUMBELE,
  • Mafanikio huja kama mvua za msimu,
  • Mafanikio ya mtu nayanafananisha na tairi lenye tundu linalozunguka ambapo kila binadamu mwenye mkuki anatakiwa kuchoma tundu lile ili afanikiwe, kwahiyo ukibahatika kulenga tundu choma kwelikweli, maana ukichomoa hutachomeka tena kwasababu tundu litakuwa limehamia kwa mwingine!
  • Kila mwanadamu kaumbwa na fursa yake, ukikosea tu ndo basi tena;
HISTORIA KWA WALIOTUTANGULIA
Mtakubaliana na mimi kwamba;
Ukiuliza wazee maskini wengi waliojilani yako watakwambia kauli kama hizi;
  • Mwaka fulani nilipata pesa nyingi sana lakini kwa wakati huo sikufikilia kufanya chochote hadi zikaisha.
  • Mimi enzi za usichana wangu ningeolewa na (Jina la Mkubwa) lakini sikuhitaji Mme kwa wakati huo.
  • Mwaka fulani tulivuna mazao mengi sana sema hatukuwaza kujipanga kuwekeza!
Kwa mifano hiyo ya wazee ni dhahili kila binadamu anakutana na nafasi ya utajili Mara moja katika uhai wake, Tatizo ni vile tu tunafeli kutokana na Vipaumbele vya matamanio yetu.

  • Wapo waliowahikupata pesa wakakimbilia kuoa na pesa ikakata.
  • wapo waliopata pesa wakajenga nyumba wakitalajia watapata zingine wanunue gari lakini hawajapata hadi leo,
  • wapo walionunua magari wakitalajia mirija itaendelea wajenge lakini wameshindwa hadi leo wamepanga.
  • wapo waliopata pesa za madini wakazichezea wanachimba had I Leo.
  • wapo waliokuwa wakuu wakafukuzwa kazi n.k
Ni Changamoto sana kujua kuitumia Fursa;
FURSA HUJA MARA MOJA TU IKIJIRUDIA NI ZARI;
Golden Chance Never comes Twice
 
Tunashukuru sana mkuu kwa uzi mzuri kabisa ila hivi karibuni kumekuwa na thread nyingi sana zikielezea namna kama hii yako! Au ni njia mpya ya kutaka kuanzisha semina za utajiri na mafanikio kama zile zilizokuwa zinaratibiwa na kina Ngoma?
Maana walimu wengi wa semina hizi huwa hawana ule utajiri wanaotufundisha sie akina pangu pakavu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ujue tatizo ni kwamba Huwezi kumiliki bila kuishinda vita, Vita ni changamoto,sifa na matamanio ambavyo vyote vinahitaji Uvumilivu unaochochewa na KIPAUMBELE
 
Uzi bora saana cha kuongezea tuu kuna mahali nilisoma palikuwa pameandikwa hivi ;
Huwe na maamuzi yaliyo sahihi katika matumizi!!
 
Si kweli kuwa fursa huja mara moja tu maishani. Fursa zipo nyingi zinatuzunguka, sema wengi wetu hatuzioni.

Na ukiharibu fursa ya kwanza haimaanishi huwezi kufanikisha kupata fursa nyingine na ukaitumia vyema.

Muhimu ni kujifunza tu je, nini kilisababisha ukashindwa itumia vilivyo fursa ya kwanza?
 
Si kweli kuwa fursa huja mara moja tu maishani. Fursa zipo nyingi zinatuzunguka, sema wengi wetu hatuzioni.

Na ukiharibu fursa ya kwanza haimaanishi huwezi kufanikisha kupata fursa nyingine na ukaitumia vyema.

Muhimu ni kujifunza tu je, nini kilisababisha ukashindwa itumia vilivyo fursa ya kwanza?
 
KILA MTU ANAFUNGU LAKE LA UTAJILI KWA WAKATI WAKE

Maisha ni fursa, Maisha ni safari, ili ufike unakokwenda lazima uchague njia sahihi ya kukufikisha.

Maisha huongozwa kwa matamanio!
Utajili na Umasikini vimetenganishwa na Matamanio!
Ili uwe tajiri ni lazima ujuwe kupangilia Matamanio yako!
Utofauti wa mali kati ya mtu na mtu huchangiwa na kufeli kwa mipangilio yenye matamanio( KIPAUMBELE)

kwa mfano:
Watu watatu marafiki waliokuwa na ndoto za utajili baada ya kumaliza shule yao, waliajiliwa pamoja katika ofisi moja kwa mshahara sawa, baada ya mda kutokana na pesa walizochuma /kopa walikuwa huru kila mmoja kufanya MATAMANIO YAKE!

wa kwanza akanunua gari nzuri kwa ajili ya kuwahi kazini kutokana na changamoto ya usafiri,ndoto yake ni kumiliki Gari zuri ikiwa kama sehemu ya mafanikio yake!
wa pili akanunua kiwanja na akaanza kusimamisha mjengo haraka kwa sababu alisikia ushauri kuwa wenye akili wanajenga kwanza!

Watatu yeye kwasababu mama yake alimsomesha kwa kuuza chakula, Alitamani kuboresha biashara iliyomsomesha akaamua kuboresha biashara na mama ake na kufungua duka la vinywaji vya jumla na rejareja huku baadhi ya pesa kidogo akanunua mifugo huko kijijini!
Wote watatu hawa walitimiza Azimio la matamanio yao katika kuufikia utajili!

NINI KILIFUATA BAADA YA HAPO?
Kutokana na mikopo yao! wa kwanza aliyenunua gari alitembelea mwaka mmoja tu akaamua kupaki maana aliandamwa na deni la mkopo huku pesa aliyokuwa akiipokea ikiishia kulipa bima, service, mafuta,parking,kodi na faini za barabarani HADI ile furaha aliyotarajia ikaanza kuyeyuka!

Wa pili aliyenunua kiwanja alifanikiwa kujenga boma lote na bahati mbaya pesa ilimwishia punde baada ya kuweka mbao za kenchi zikalala zikipigwa jua na mvua bila bati!

wa tatu alifanya biashara akapata faida kiasi cha kununua kiwanja na kujenga taratibu kwa faida iliyotokana na biashara iliyosimamiwa na mama yake!

KILICHOENDELEA BAADA YA HAPO
Kwa bahati mbaya sana Bodi na taasisi yao baada ya kuonekana haina faida katika nchi IKAFUTWA NA RAIS WA NCHI HIYO!

KWA MFANO HUU
Ninachotaka kusema ni hivi!

Maisha ni vile unavyotanguliza KIPAUMBELE,
  • Mafanikio huja kama mvua za msimu,
  • Mafanikio ya mtu nayanafananisha na tairi lenye tundu linalozunguka ambapo kila binadamu mwenye mkuki anatakiwa kuchoma tundu lile ili afanikiwe, kwahiyo ukibahatika kulenga tundu choma kwelikweli, maana ukichomoa hutachomeka tena kwasababu tundu litakuwa limehamia kwa mwingine!
  • Kila mwanadamu kaumbwa na fursa yake, ukikosea tu ndo basi tena;
HISTORIA KWA WALIOTUTANGULIA
Mtakubaliana na mimi kwamba;
Ukiuliza wazee maskini wengi waliojilani yako watakwambia kauli kama hizi;
  • Mwaka fulani nilipata pesa nyingi sana lakini kwa wakati huo sikufikilia kufanya chochote hadi zikaisha.
  • Mimi enzi za ufichana wangu ningeolewa na (Jina Mkubwa) lakini sikuhitaji Mme kwa wakati huo.
  • Mwaka fulani tulivuna mazao mengi sana sema hatukuwaza kujipanga kuwekeza!
Kwa mifano hiyo ya wazee ni dhahili kila binadamu anakutana na nafasi ya utajili Mara moja katika uhai wake, Tatizo ni vile tu tunafeli kutokana na Vipaumbele vya matamanio yetu.

  • Wapo waliowahikupata pesa wakakimbilia kuoa na pesa ikakata.
  • wapo waliopata pesa wakajenga nyumba wakitalajia watapata zingine wanunue gari lakini hawajapata hadi leo,
  • wapo walionunua magari wakitalajia mirija itaendelea wajenge lakini wameshindwa hadi leo wamepanga.
  • wapo waliopata pesa za madini wakazichezea wanachimba had I Leo.
  • wapo waliokuwa wakuu wakafukuzwa kazi n.k
Ni Changamoto sana kujua kuitumia Fursa;
FURSA HUJA MARA MOJA TU IKIJIRUDIA NI ZARI;
Golden Chance Never comes Twice
True

And if the chance come twice grab it with both hands of yours

Sent using Jamii Forums mobile app
 
24 Reactions
Reply
Back
Top Bottom