Tarehe 15 ndiyo leo na makato mapya ya miamala ya simu. Tumewekewa makato ya Vodacom tumeona tigo pia makato yao

Bado kuna mitandao mingine hawajaweka wazi makato yao (hata kama wameweka basi wadau hawajatupandishia bango humu)

Ingawaje zantel leo wamenitumia ujumbe kuhusu makato mapya ila bango lao sijaliona bado

Kupitia uzi huu naomba tuanikiwe mabango yote ya makato ya miamala ya simu kwa mitandao yote hapa Tanzania ili tujue tunakimbilia wapi

Pole, naona umewahi kweli ili uone mtandao wa kukimbilia mapema. Mimi ni kama wewe tu tuungane kusubiri

Vodacom
Halotel
Zantel
Airtel
Tigo
TTCL

JamiiForums1108062210.jpg
View attachment 1854963View attachment 1854964View attachment 1854961View attachment 1854962View attachment 1854965
 
KWA KWELI HII NI AHABU SANA KWA WATUMIAJI WA MITANAO YA SIMU KWA PESA MAKATO NI MAKUBWA MNOOOO UUUUU MWIGULUumempotosha sana Mama yetu duuuu
 
Mama anaupiga mwingi sanaaaaaaaaaaaaaa ndio kauli ya wapinzani.watumiaji wengi wa Mpesa ni wafanyabishara wahali ya chini na kati sasa wanachukuliwa kidogo kilichopo,

1)kodi ya mapato
2)kodi ya nyumba kwenye biashara unapolipa TRA
3)kodi ya Ardhi
4)kodi za mtandao
5)kodi ya mafuta kupanda
6)umeme wa bei rahisi hakuna tena
7)leseni za biashara
8kodi ya barabarani
9)kodi ya jengo
Hizi kodi mnazotukamua kwa mzunguko gani wa biashara? Kwa mishahara gani mnayotulipa?
 
Hapa naona fulsa kwa dereva bodaboda mwaminifu. Yaani kama unamtumia pesa elfu 50000/= makato elfu 7500/= si bora umpe bodaboda elfu 2000/= aikimbize fasta
Ndicho nilichofanya leo na nitakachofanya kwa miaka ijayo, serikali itakula kodi yangu nyingine siyo ya miamala ya simu.

Everyday is Saturday............................... :cool:
 
Bei mpya za miamala ya kutuma na kutoa pesa linatoa picha mbaya serikali.
1. Serikali haiko na wananchi
2.serikali ingekuwa karibu na wananchi ingejua wananchi wana HALI GANI.
Hizo bei ni kubwa haikubaliki.
Mfano kutuma TSH 100000/= tunduma nikiwa mbeya
Kutuma= 3000
Kutoa = 7000
Jumla. = 10000
Maana yake:- nilitaka kutuma TSH 100000 nilazima niwe na zaidi ya TSH 110000.
Maana yake nini.
Maana yake ni hii hapa chini:-
Mbeya tunduma nauli = TSH 4000
Tunduma MBEYA
Nauli= TSH 4000
Kwanini hiyo hela nisipeleke mwenyewe nikaokoa TSH 2000.
Au nikampa dereva TSH 4000 anipelekee.
Hili jiwe tutakwepa.
Tutatumia mtandao ambao siyo rasmi wa mabasi ambao ulikuwapo hata kabla ya mpesa.
 
Back
Top Bottom