Tazama hapa jinsi gani mchezo wa Kibati ulivyo chanzo cha madeni kwa taswira nyingine

Fya-fyafya

Member
May 2, 2019
43
150
Mchezo wa kibati ni mchezo wa waaminifu ambao watu wawili au zaidi hucheza kwa kupeana hela/ fedha kwa zamu.

Zamu hizo hufanyika kwa mzunguko wa siku fulani kutokana na makubaliano ya wachezaji wenyewe.

Hapa nchini, katika makundi tofauti ya jamii, mchezo huu umekuwa maarufu sana kwa kuchezwa na watu hasa wenye nia na lengo moja la kujikwamua kimaisha.

Aidha, mpaka sasa kuna kundi kubwa la watu tena wengi tu ambao hawauelewi kabisa huu mchezo. Yaani hawaelewi moja kwa moja faida zake na hudhani kuwa kucheza kibati ni pengine kujipotezea muda, hivo basi hawachezi. Kuna na wengine nao wengi tu wanauelewa huu mchezo na wanaucheza na hawaoni sababu za kuacha na hawaji kuacha kucheza.

Baada ya utangulizi huo, sasa twende kwenye maada husika isemayo. "Ona mchezo wa kibati ulivyo madeni pasua kichwa kwa taswira nyingine."

Deni ni mali, kitu, fedha au kitu chochote cha mtu mwingine kwa njia ya makubariano au vinginevyo unachomiliki au ulichotumia nk kwa maana ya kukirudisha tena kwa mtu huyo aliyekupa. Au kwa maana nyepesi, deni ni kitu au pesa unayodaiwa.

Mchezo wa kibati unakuweje tena deni na tena deninpasua kichwa? Hii ni kutokana na hali ya mchezo wenyewe; yaani watu wawili, wa tatu, wa nne au zaidi (vibati vingine huwa na members hadi 50) kuchanhishana pesa walizokubaliana na kumtoa (kumpa) mmoja wao au wawili kadri wali yokubaliana.

Hii inakuwa deni kwa maana kwamba; mtu akipokea pesa leo maana yake hii pesa aliyopata ni ya wenzake. Kwa hiyo zamu inayofuata na kwendelea atazidi kuzurudisha kwa awamu kwa wale waliompa.

Kwa mfano kibati kina watu wa tano (05) na amekubaliana kucheza kibati sh. 50. 000 kila mwezi. Maana yake kila mwenye zamu ya kupewa hela atakuwa anakabidhiwa sh 200.000 maa yake elfu hamsini hamsini za wenzie wanne.

Hicho kibati alichopewa cha sh. 200,000 ni kama deni au mkopo usio na riba ambao ataurudisha ndani ya miezi minne (04) mfululizo.

Hii na maana kwamba: kwa mfano mwezi huu ndo amepokea basi mwezi ujao ataanza na kwendelea atakuwa anatoa laki moja moja kwa miezi hiyo minne mfululizo kwani itakuwa ni miezi ya vibati vya wenzie. Kwa maana hiyo basi hela ya kibati haikai mfukoni, inaingia na kutoka!

Kwa maana hiyo basi, mchezo wa kibati unakuwa na sura mbili ambazo ni kutunziana au kushikiana pesa kwa muda au kukopesha pesa bila riba.

Changamoto za mchezo wenyewe.

Ukosefu wa waaminifu

Hii hujitokeza sana pele wacheza kibati wenyewe wanaposhindwa kupeana pesa kwa muda. Kwa uchunguzi kidogo ulofanywa ni kwamba kwenye kibati, kiwe cha watu wawili , wa tatu ama zaidi; kunatokea baadhi ya washiriki ambao huwasilisha pesa zao too late.

Kwa mfano memba X anapewa pesa leo lakini hapewi mpaka pengine juma mosi kwa sababu tu wote hawajamalizia kutoa hela. Kwa ujumla kunakuwa na hali ya baadhi ya members kujivuta kuchanga hasa wale ambao zamu zao zilishapita! Hivo hukwamisha wenzao.

Kugombania kuwa wa kwanza kupokea kibati

Katika vibati vingi, kuna hali ya marumbano ya kila memba kutaka kuwa wa kwanza kupokea kibati. Yaani kila mtu anataka ile day one kibati kimeundwa basi yeye awe wa kwanza kukusanyiwa mpunga.

Hivo inasemekana huchukuwa muda kidogo wote kuafikiana nani awe wa kwanza maana kila mmoja hutoa shida zake za maana akiconvince wengine ili hatimaye apewe wa kwanza au awe wa pili kama ni wengi.

Pia, inaelezwa kuwa kuna hali ambayo inajitokeza ndani ya safari ambapo mtu zamu yake ni ya nne (04) au ya mwisho na halafu ndo kibati kipo zamu ya pili sasa mtu huyo anaomba kubadilishiwa zamu ili yeye achukue zamu hiyo ya pili huku akisema amebanwa hana kitu na hana ya kutoa.

Hii humwathiri yule mwenye zamu yake maana naye pia alikiwa amevumilia kwa kutoa pesa kwenye zamu za watu wengine bila kuchoka na alikuwa akisubiri zamu yake.

Zamu kuishia njiani

Kibati chenye watu wengi kuanzia wa tatu na kuendelea huwa kinakuwa na changamoto nyingi ikiwemo ya zamu kukwama na kuishia njiani hivo kuleta tafrani na malumbano.

Hii hujitokeza pale ambapo wale members ambao walishachukua mpunga kwenye zamu zao wanapoishiwa pesa pindi wanapotoa au kurejesha kwa zamu za watu wengine.

Watu wengi wakipokea kibati hutumia hiyo hela kujikwamua kiaisha kama vile: kununua dhamani na vyombo vya ndani, kulipa ada, kulipa kodi ya nyumba, kufanyia starehe n.k .

Watu hao wanasahau kuwa hiyo hela ni ya watu na wao watawajibika kurejesha au kuchangia wengine kwenye zamu zao!

Watu sasa wanajikuta hawana hela ya kuchangia wenzao wa zamu zinazofuata. Kwa hali hiyo basi humcheleweshea mwenzao wakisahau kuwa huyo wanaemcheleweshea alikwisha wachangia pesa Kwenye zamu zao.

Wengine hufika mbali mpaka kibati kinasimama au kuvunjika kabisa na kuanza kipelekana kwa Balozi, kwa mwenyekiti wa mtaa au kwa mtendaji kata kwa shauri la madai.

My takes:

Hela ya kibati si ya kuchezea. Hela ya kibati, huo ni mkopo. Ni mkopo usio na riba, unaorudisha haraka tena mapema kwa wenzako tena kwa mfururizo kutokana na idadi ya mizunguko ya kibati hicho.

Hela ya kibati ni hela ya kutumia kwa makini tena kwa wangalifu kutokana na kipato chako ili kuepusha aibu na misuguano na watu mloaminiana pale mwanzo mlipokuwa mnaanza hicho kibati.

Ni vema kucheza kibati ambacho hakitoathiri maisha yako baada ya kurejesha au kuwachangia wenzako.

Ni vizuri kuepuka kucheza kibati ambacho kiko juu ya kipato chako ili kuepuka kukopa kopa pesa huku na kule ili tu upate ya kibati. Ukikosea tu utahatarisha maisha yako, familia yako na Ndoa kwa ujumla.

Nawasilisha.
 

Lenie

JF-Expert Member
Aug 3, 2012
3,660
2,000
Huu mchezo ni mzuri hasa mkiwa wote waaminifu n mnajitambua, wala usumbufu wowote hautajitokeza pia msiwe wengi sana maana mzunguko ukiwa mrefu inachosha.

Ni kwel kabsa na muhimu mtu acheze wa kiwango ambacho anakimudu kutokana na kipato chake
 

Mr Easy

JF-Expert Member
Jan 16, 2016
1,527
2,000
Sisi tulikuwa wanne tulitengeneza kakatiba kabisa kenye masharti magumu na tulifanikiwa kwa kweli.
Yaani siku ile ile mnapopokea mshahara, bila shuruti wala kukumbushwa, unatuma kwa mwenye zamu kiasi mlichokubaliana bila kupunguza hata senti moja wala visingizio.
Malipo yote lazima yawe ya bank na sio cash au mitandao ya simu.
Kuna kipengele tuliweka mwanakikundi anapojiunga anatoa dhamana (hela) ambayo ni sawa na mchango wa mwezi wa kumchangia wanakikundi.
Dhamana hiyo utarudishiwa mara baada ya kikundi kuvunjika automatically mara baada ya mzunguko kuisha. Ukishindwa kumtumia mwanakikundi kiasi kamili saa 24 baada ya mshahara kutoka, dhamana yako itatumika kumlipa mwanakikundi mwenye zamu, huku wewe ukipoteza kabisa sifa za kuwa mwanakikundi.
 

Akili Sina

JF-Expert Member
Jan 18, 2018
267
1,000
Sisi tulikiwa watatu tunacheza laki 4 kwa mwezi, mmoja akashindwa nikabaki na jamaa yangu paka Leo tunaendelea zetu ........Kiukweli kana saidia....ila si kama vile wanavyocheza wamama wa uswahilini, kikundi kina watu 50, hela yenyewe elf mbili sjui tatu, kila siku kelele ,kurushana , Mara huyu kapokea kakimbia , yaah full vurugu

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom