Tazama gari yenye uwezo wa kupaa. Imepewa kibali huko Slovakia

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,813
4,546
Gari inayopaa yenye uwezo wa kuruka kwa zaidi ya futi 8,000 (sawa na mita 2,500) na kukimbia kwa kasi ya zaidi ya 100mph (sawa na km 160 kwa saa) imeidhinishwa na kupewa cheti cha kuiruhusu kufanya safari za angani na mamlaka ya Usafiri ya nchini Slovakia.

Gari hiyo iliyoundwa na Prof.Stefan Klein kutokea nchini Ujerumani huchukua dakika mbili na sekunde 15 kubadilika kutoka gari hadi kuwa ndege, ambapo imeundwa kwa kutumia injini ya BMW na pia hutumia mafuta ya kawaida ya pampu ya petroli.

Tazama hapo chini

Gari inayopaa yenye uwezo wa kuruka kwa zaidi ya futi 8,000 (sawa na mita 2,500) na kukimbia kwa kasi ya zaidi ya 100mph (sawa na km 160 kwa saa) imeidhinishwa na kupewa cheti cha kuiruhusu kufanya safari za angani na mamlaka ya Usafiri ya nchini Slovakia.
...
Ajali za anga zitakuwa nyingi sababu ndege inataka inspection na preventive maintenance za mara kwa mara.

Pia watu wengi ni Don't care. Hilo tatizo mpaka hapo.
 
Back
Top Bottom