Tazama foleni hii ya wanunuzi wa sukari Morogoro. Juzi Waziri Bashungwa kapitishiwa bajeti ya hovyo iliyoungwa mkono na wanaccm wote Bungeni

Al bashir wa Sudan alionndolewa madarakani kwa kuzidisha bei ya unga wa ngano tu. Watanganyika sisi ni washamba wa maendeleo na tutaendelea kunyanyaswa maisha yetu yote hata na Washamba wanaokuja mjini!
Nenda sudani mkuu mkawe wa mjini, usiwe mshamba!
 
Hata kama usemavyo ni kweli. Swali :Je sukari ipo mitaani?? Je ukibahatisha utauziwa kwa bei elekezi ya Serikali??
Acheni siasa kwenye masuala yanayowahusu au kuwaumiza Wananchi bila sababu za msingi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo lako haupendi kufuata ushauri wa kitaalamu, yule Mhe. alisema sukari sio nzuri kiafya sasa wewe unalazimisha kutumia sukari hivi huwezi kunywa uji? Mbona serikali imetoa vipaumbele vingi tu, kuna uji, maji, soda, pombe n.k we kwanini hutaki kuelewa?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo ni Nyerere, itatuchukua karne nzima kuufuta ujinga wa sera za ujamaa na mapambano yetu dhidi ya maadui wa kufikirika. Tuko tayari kuwalinda mabwenyeye waachache wanaomiliki viwanda vya sukari na wanaohodhi vibali vya kuingiza sukari kwa gharama ya maisha ya mtanzania wa kawaida. Sad.
 
Hii ni foleni ya wanaonunua sukari Morogoro mjini ndani ya duka la mbunge wao.

Kinachonikera zaidi juzi waziri wa viwanda na biashara kapitishiwa bajeti mbovu sana huku wabunge wa CCM pamoja na spika wakijikita kuishambulia Chadema.

Aidha hawa ni wanunuzi wa jumla. Unapata Corona na sukari halafu ukitoka hapo wanakuja watu wa serikali za mitaa wanataifisha.

Kishindo cha awamu ya tano kwelikweli!

dingilai mwenyewew yuko chimbo hana habari na mtu
 
Morogoro kuna viwanda viwili, kilombero na mtibwa ba bado kuna shida ya sukari.

Sasa hivi dukani mpaka muuza dula awe anakujua ndio anakuuzia
Morogoro si kuna kiwanda cha sukari, mbona kwenye picha tunaona viroba vya sabuni... hata hivyo sukari kiafya sio muhimu kiviiiilee tumekariri tu hatujui kula vizuri.

Stay home, stay safe
Corona kills
 
Jana nimeenda sehemu asubuhi nataka chai naambiwa hakuna, kuuliza kwanini wanasema sukari hakuna madukani.

Wanawalazimisha wauzaji wa rejareja wauze kwa bei wanazotaka serikali (bei elekezi), wakati hao jamaa walinunua sukari yao kwa bei ya juu toka kwa wauzaji wa jumla, wauzaji wa rejareja walichoamua sasa ni kuificha sukari yao, hawaiuzi wasijepata hasara.

Ndio nikapata akili, naona siku hizi kama taifa tumeanza kurudi nyuma.

Sent using Jamii Forums mobile app
Leo nimenunua sukari 6000 kilo. Sikuwa na jinsi maana ndani hakuna na inahitajika. Kutokana na mazingira jinsi yanavyoenda nikaona wacha ninunue kilo 10 niweke ndani kupisha lawama ya familia.
 
This is a presidential failure circumstance. Lini alishawahi kuwa sahihi katika migogoro yote ya kiuchumi iliyotokea kuanzia pamba, mbaazi, korosho na mara kwa mara sukari?
Atakimbilia kutambua waziri kama sehemu ya kufichia madhaifu yake mara "wanatumiwa na mabeberu"
 
Hili la sukari nalo mpaka Rais alisemee kweli,,? Sukari tu
Alipoingia madarakani alilizungumzia sana na kupiga marufuku uingizaji sukari toka nje ya nchi. Bei elekezi iliwekwa 1700/- lakini iligomea 2600 mpk 3000/-
Uzoefu unaonyesha hata sasa bei elekezi zitashindikana na sukari either itauzwa kwa bei iliyoko madukani au itaadimika sana
 
Hivi mahitaji ya sukari kwa mwaka yakoje?Uwezo wa ndani wa kuzalisha sukari ukoje?Kaisi gani tunahitaji kuagiza toka nje??Yaani maswali haya rahisi tu tunashindwa kuyasolve?? Hadi sukari kilo moja inauzwa 5k?Tena inapatikana kwa taabu kweli kweli wengine hadi wananunua kwa foleni

View attachment 1445773
Huyu ndiyo waziri wa viwanda aliyeandika hiyo post Twitter?

Hii nchi sijui imelogwa na nani aisee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
27 Reactions
Reply
Back
Top Bottom