Tazama baadhi ya mapungufu yaliyojitokeza katika majina ya ajira za Ualimu yaliyotolewa. Jina la 'ABADALLAH LEONARD SHONDE lajirudia mara 196

Kusema ukweli hizi ajira ni MAGUMASHI, hazina uhalisia wowote. Jina moja linajirudia mara nyngi na kituo ni kilekile.

Kuna wengine wamemaliza fom4 mwaka 2019 eti na wao wameajiriwa....
Hahahahaha huyu shonde mbona ana bahati sanaaa

Sasa inabidi shonde achague kituo cha kazi akipendacho ...
 
Usikalili mkuu unazani watu wanaosomaga uku wakiwa usalama wa Taifa huwa hawana mishe
 
Wakati kundi kubwa la vijana likiwa na nyuso za simanzi baada ya kukosa ajira, haya ni baadhi ya madudu yaliyofanywa na TAMISEMI na kupelekea vijana wengi kukosa ajira huku wakiwa na vigezo;

1. Serikali kupitia TAMISEMI imeajiri jumla ya walimu 28 waliomaliza kidato cha nne mwaka jana, 2019. Swali la kujiuliza kama hawa vijana walimaliza form four mwaka jana, chuo walienda lini na walimaliza lini mafunzo ya ualimu?. Huu ni mwendelezo wa TAMISEMI kuajiri walimu hewa serikalini

2. Serikali imeajiri walimu wenye tahasusi zenye utata kwenye masomo yao. Mf. Mmoja kaajiriwa kama mwl wa mathematics, civics na mwingine ana masomo ya mathematics, history na kiswahili Wote wamepangiwa kufundisha sekondari. Je, walimu hawa walichukua tahasusi gani kidato cha sita?. Hawa nao ni hewa

3. Kigezo cha umri kuajiriwa serikalini mwisho ni miaka 45. Lakini kwenye ajira zilizotangazwa na tamisemi wapo walimu walimaliza kidato cha nne kati ya 1994-1997. Ukipiga hesabu hawa walimu wana umri zaidi ya miaka 45. Swali la kujiuliza, hawa walimu walikuwa wapi miaka yote hiyo? na je, tamisemi hawakuligundua hilo?. Hawa inawezekana wana michongo na wakubwa kule tamisemi.

4. Katibu anasema ajira zilizotolewa ni 13000. Uongo mtupu. Kuna page zina walimu 48, 38, 37, 42, n.k. Ambapo kwa uwiano wa walimu 41 × idadi ya page 197 utapata jumla ya walimu 8077 ndio walioajiriwa. Je hiyo 13000 ya katibu mkuu inakujaje?. Hewa hewa kwa kwenda mbele.

5. Walimu wengi wamepangiwa sehemu ambazo hawakuchagua. Hapa inaonyesha machaguo hayakuzingatiwa kwahiyo hapakuwepo haja ya watu kuchagua shule kama serikali ilikuwa inajua pa kuwapeleka.

Madudu yapo mengi tutaendelea kuyaibua kadri tutakavyo yabaini
 
Kusema ukweli hizi ajira ni MAGUMASHI, hazina uhalisia wowote. Jina moja linajirudia mara nyngi na kituo ni kilekile.

Kuna wengine wamemaliza fom4 mwaka 2019 eti na wao wameajiriwa.

Swali: Kwanini hawajaandika vyuo walivyosomea? Kwanini hawajaweka serial number?

MUNGU TUNUSURU
Inawezekana lengo lao ni tofauti na lako, lengo lao ni umma ujue ahadi ya ajira imetekelezwa, swala la wako wapi hao watu si muhimu.
 
27 Reactions
Reply
Back
Top Bottom