Tayari Sabaya amechomoka, kama alipewa maagizo toka juu ujambazi anahusika vipi?

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Tujiulize kwa kutumia akili za kawaida tu. Mkuu wa wilaya atoke wilaya nyingine alafu aende kufanya uhalifu wilaya nyingine? Hii ni ngumu.

Kwanini Kenan Kihongosi aliyekuwa mkuu wa wilaya Arusha aliruhusu huu uhalifu?

Kwa nini magari ya serikali yalitumika kufanya uharifu?

Kwa nini Sabaya awachukue aliowapora na kuwapekeleka polisi kama wahalifu?

My take: Ofisi ya Dpp imejaa uozo na kukosa weledi. Maana inapoteza rasilimali za umma kushitaki pasipo busara. Kosa la ujambazi liliingia vipi?
 
Kwa bahati mbaya sana kauli alizotoa Sabaya mahakamani kama utetezi huo ndio ukweli halisi. Kwa bahati mbaya sana kuna visa vingi kama hivi havijaripotiwa wala kuibuliwa iwe na wahusika au waathirika

Hadithi ya kutekwa kwa Mohamed Dewji bado ni fumbo na naamini "MAMLAKA" ya sasa ikimruhusu au ikimtaka aseme ukweli mtupu kwa yale yaliyotokea Watanzania tunaweza kujiuliza kulikua na mtu wa aina gani pale jumba jeupe

Yaliyotokea pale Mawingu Radio katika sakata lililowahusisha Nape, Paul Christian na Ruge na staff wake pengine hatutajua ukweli wote lakini kwa wakati ule ushahidi wa mazingira ulijionyesha wazi nani alikua nyuma ya maagizo yale.

Aliyeunda tume ya kuchunguza uhalifu ule akapokonywa wadhiwa wake with immediate effect huku akinusurika kutekwa baada ya jaribio la kufanya hivyo kuonekana public! The culprit aliyetakiwa kuchunguzwa ndio akawa anatamba kwenye vyombo vya habari vya umma huku MAMLAKA yake ya uteuzi ikimpa support

Usia wangu kwa wateule wa "MAMLAKA": OBEY LAWFUL ORDERS FROM LAWFUL AUTHORITY
 
Tujiulize kwa kutumia akili za kawaida tu. Mkuu wa wilaya atoke wilaya nyingine alafu aende kufanya uhalifu wilaya nyingine? Hii ni ngumu.

Kwanini Kenan Kihongosi aliyekuwa mkuu wa wilaya Arusha aliruhusu huu uhalifu

Kuna Precedent ,Kutumwa hakukuondolei msala wa kesi ,rejea kesi ya wafanyabiashara wa madini morogoro , mtuhumiwa badeni alikutwa na hatia ya mauaji ila yeye alijitetea kwamba alitumwa na zombe (mkuu wake), zombe na yeye akasema hajashika silaha na hajawahi kuua huko msitu wa pande kwahiyo ikala kwa badeni.

Hata kama alitumwa na Magufuli ,aliyefanya tukio ni sabaya kwahiyo hakumuondolei msala na hakuna kinga ya kufanya uhalifu maana hakuna aliye juu ya sheria.
 
Tujiulize kwa kutumia akili za kawaida tu. Mkuu wa wilaya atoke wilaya nyingine alafu aende kufanya uhalifu wilaya nyingine? Hii ni ngumu.

Kwanini Kenan Kihongosi aliyekuwa mkuu wa wilaya Arusha aliruhusu huu uhalifu?..
kama ilikuwa nia ni kukamata uhujumu uchumi wapi Salisema kawakamata hao wenyeduka na akiwa na vielelezo vya uhujumu mfano hela taslimu ambazo hazijulikan zimetokea wapi labda sio za mauzo!? utoto mwingi umempeleka miaka 30 jela
 
Tujiulize kwa kutumia akili za kawaida tu. Mkuu wa wilaya atoke wilaya nyingine alafu aende kufanya uhalifu wilaya nyingine? Hii ni ngumu.

Kwanini Kenan Kihongosi aliyekuwa mkuu wa wilaya Arusha aliruhusu huu uhalifu?
Mkuu ebu jiongeze kidogo acha kuelemewa na mahaba.

Tuhumu alizonazo ni jinai. Utetezi wa kuwa nilitumwa haumtoi hapo hasa ukizingatia anayesema alimtuma sasa amerudi mavumbini.
Kumbuka kesi ya Balozi Costa Mahalu ya ubadhirifu katika ununuzi wa nyumba ya Ubalozi Italia; Alichomoka baada ya Rais Mkapa akiwa mstaafu kwenda mwenyewe mahakamani na kusema alimtuma.

Hapo kesi ilikuwa ni manunuzi tu; Kwa Sabaya ni Ujambazi na JPM aliyemtaja is gone..Haya tuone anavyochomoka!
 
Mkuu ebu jiongeze kidogo acha kuelemewa na mahaba.
Tuhumu alizonazo ni jinai. Utetezi wa kuwa nilitumwa haumtoi hapo hasa ukizingatia anayesema alimtuma sasa amerudi mavumbini
Armed robbery huwa inafanyika vipi? Kwani mtu akifa na ofisi huwa inakufa?
 
Back
Top Bottom