Tawi la NMB lililopo Makao Makuu ya TRA Mwanza wana huduma mbovu sana

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
1,487
2,000
Leo nilitakiwa nipate huduma katika Tawi hilo kwa kulipia mapato ya TRA lakini nilipofika pale sikuamini macho yangu. Tawi lile lina madirisha matano ya kutolea huduma lakini ni dirisha moja tu ndilo lililokuwa na mtumishi wao anayetoa huduma.

Wateja tulikuwa zaidi ya 200 na wengi wa wateja walikuwa wanakimbizana na siku ya mwisho wa tarehe 30/6/2020 kwa kulipia mapato bila faini.

Tulipomhitaji Meneja wa Benki hakuonekana na tulipomuuliza Dada mmoja humo ndani majibu aliyotupa hakuturidhisha wateja tuliokuwapo pale.

Meneja na watumishi wote wa pale wanatakiwa wahamishwe na kuleta wapya. Wateja 200 kwa mtumishi mmoja?. Kwa kweli inaumiza na inaudhi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom