Tawi la CCM-Urusi kuanzishwa hivi karibuni.

TANMO

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
11,506
11,250
Kwa sasa mchakato wa kuwasaka wanachama (ambao asilimia kubwa ya walengwa ni wanafunzi wanaosoma katika chuo kikuu cha Lumumba-Moscow) unaendelea huku maandalizi ya vikao vya ufunguzi wa tawi vikiendelea ambapo ajenda kuu zinazojadiliwa kwa sasa ni lini hasa ufanyike mkutano wa ufunguzi na nani aalikwe kama mgeni rasmi kutoka Tanzania. Pia kadi za uanachama zinategemewa kuanza kutolewa punde tu zitakapowasili kutoka Tanzania.

Mlezi wa Tawi anategemewa kuwa Balozi mpya wa Tanzania nchini Urusi Kapteni Jaka Mwambi.

Kwa kuanzia wahusika wameanzisha blog iitwayo: http://www.wanachama.blogspot.com ili kurahisisha zoezi la upashanaji habari kwa wote wenye nia ya kujiunga na Chama.
 
Last edited by a moderator:
Idadi ya Watanzania wanaosoma chuoni Lumumba-Moscow ni zaidi ya wanafunzi 150 kwa sasa na inategemewa kupanda kutokana na wanafunzi wengine 100 ambao watawasili punde kwenye mwaka mpya wa masomo utakaoanza mapema mwezi ujao..
 
Hongereni sana Moscow; imewachukua muda kujifunza kuwa ukiwashindwa, jiunge nao. Smart move. Angalau sasa hela zenu zitawafikia kwa wakati na hasa mkimuweka Balozi kuwa Mlezi. CCM nambari one!!
 
Duh, ni kansa jamani. Frederiko Sumaye aliona mbali - ukitaka mambo yako yanyoke...na huku akina Mallya wakiongezeka kwa kasi, ari na nguvu mpya maanake Urusi nako ndiko kwenyewe.
 
Kwenye Msafara wa Mamba kenge nao wamo.


Hivi ninyi vijana mna jumiya ya watanzania huko? Wale vijana waliosuswa na serikali yao huko Ukraine mbona hamkuonekana mko wengi namna hii katika kuwasaidia wenzenu?

Au tuseme mlikua upande wa Msolla maanake leo mmeamua kabisa kujitangaza kujiunga na waliowatelekeza vijana wenzenu.Leo kwao,kesho kwenu au kwa wadogo zenu.

More Respect,kwa wale waliojiunga nao ili kuleta mapinduzi ya kulikomboa taifa letu kwa kuanzia ndani ya Chama.Kwa kweli waliojiunga na CCM kwa lengo hili nawapa Respect kubwa
 
Wote wanaofungua matawi ya CCM wakiwa nje ya nchi, wengi wao wanavunja katiba ya CCM. Ninashangaa sana kuwa viongozi wa CCM ambao ndio wanaotakiwa kulinda katiba ya chama chao hawalioni hilo. Chini ya katiba ya CCM, kifungu 31(1)(d), tawi la CCM litaundwa nje ya nchi kama kuna wana-CCM wengi wanaoishi katika sehemu mbalimbali za nchi hiyo na ambao wana Mashina yao; tawi hilo litaundwa kwa idhini ya kamati kuu ya CCM. Kila tawi linataakiwa aliwe na wanachama wasiopungua 50 na wasiozidi 600.

Chini ya kifungu hicho kuna mambo kadhaa yanayosababisha matawi mengi nje ya nje yawe ni batili:

(a) kuwa na wanachama wengi katika mji mmoja hakuhalalishi kuundwa kwa tawi, lazima wanachama hao wawe wametoka sehemu mbalimbali za nchi husika. Matawi ya Reading, Mysore na sasa Moscow hayajaonyesha kuwa yana wanachama kutoka sehemu mbambali za nchi husika, hivyo yananweza kuwa yanvunja katiba.


(b) Kabla ya kuundwa tawi ni lazima kuwa na mashina kadhaa kutoka sehemu mbalimbali za nchi husika. Sikusoma katiba vizuri lakini tawi haliwezi kuundwa na shina moja tu. Kwa vile kila shina linatakiwa kuwa na wanachama wasiopungua kumi, wakati tawi linatakiwa kuwa na wanachama wasipungua hamsini, basi ni sawa na kusema kuwa kila tawi linatakiwa liwe na mashina yasiyopungua matano. Nina wasiwasi kama matawi yote yanayoundwa nje ya nchi ama yana idadi kamili ya wanachama wanotakiwa na au yanayo idadi sahihi ya matawi.


Matawi yote ya CCM nje ya nchi ambayo nimewahi kusikia huwa yako mahala anakoishi ama kada au mtoto wa kada fulani wa CCM, kwa mfano Reading kulikuwa na mtoto wa Kikwete, Mysore kulikuwa na Nape Nnauye, na sasa huko Moscow hatujui kuna kada gani tena.
 
Mwalimu Kichuguu,

umefanya vyema kuwawekea hao vilaza wa katiba yao wenyewe mapungufu waliyo nayo katika huu mkakati.Hata hivyo Hapo kwa Nape Nnauye ni kwamba Nape anatokea Bangalore,ila huko Mysore kuna mtoto wa VP Dr.Shein ambaye ndiye alisoma hotuba ya ufunguzi wa hilo Tawi mbele ya spika wa Bunge Samwel Sitta kwan alikua mgeni Rasmi.Sasa hebu nuikipata muda nitafuatilia kama matakwa ya hii katiba yao yamefuatwa ktk uanzishwaji wa hayo matawi.

Tunapokua na viongozi wa matawi ambao hawazingatii katiba za vyama vyao ndio source ya kuja kuweka viongozi mazezeta ambao wanashindwa hata kuichambia katiba ya Nchi kama ilivyo sasa kwani ukilaza wao umeshindwa hadi sasa kutengua kitendawili cha Zanzibar kuwa nchi ama la! It doesnt make sense!
 
nyie vijana mmetumwa kusoma ua kusomea ukereketwa shughuli zenu, mtakapotelekezwa na hicho chama msije kulaLAMIKA HAPA JAMVINI
 
Nimesahau, Someni Kwa Bidii Acheni Ndoto Hizi

Kwamba Mkijikomba Kwa Ccm Mkimaliza Shule Mtachukua Nafasi Za Makamba Na Kingunge, Wale Hawazeeki Wana Miaka Kama 40 Hivi, Nyie Ndo Mtazeeka

Pia Msijivike Kilemba Ambacho Hamnacho, Zamani Ukiwa Nje Ukirudi Hapa Kila Mtu Alikuwa Nakuona Wa Ajabu Ajabu Vile, Leo Kila Wakati Watu Wanakuja Huko Moscow Kufanya Shopping. Malizeni Shule Njooni Tujenge Taifa La Kweli Lisilo Na Mafisadi, Acheni Kuota Alinacha
 
Nilikuwa nichukuwe kadi katika matawi ya UK... sasa nasubiri hili la Moscow kwani lipo karibu nami.

Kidumu Chama Cha Mapinduzi
 
naona umetoa pongezi za ufunguzi wa tawi kiunyonge...ndio hivyo tena wameshika mpini!! vijana wanaona isiwe taabu...lakini bottomline huu ni upuuzi tu na kuwatia matatizoni wale watakao kataa kuwa memba inapafika wakati wa "hawa-llonce."

Stop hatin'....na wewe anzisha tawi huko Boston...kwani umekatazwa na mtu?
 
Unaona sasa? Tayari serikali yao waliojikomba kwao imeshawaletea usanii.Wameenda ubalozini kufanya nini sasa.
 
wale wa china wana vyama vya umoja wa watanzania kila state.Istoshe wameshakuwa wakomunist.Who knows!!
 
hahaaaaaaaaaaaaa haya mwanakijiji nimekufuma hapa leo
Hongereni sana Moscow; imewachukua muda kujifunza kuwa ukiwashindwa, jiunge nao. Smart move. Angalau sasa hela zenu zitawafikia kwa wakati na hasa mkimuweka Balozi kuwa Mlezi. CCM nambari one!!
 
Back
Top Bottom