TAWAQAL Petrol Station, Ipogolo, Iringa; huduma ya chakula mgawahani ni mbovu sana

Lole Gwakisa

JF-Expert Member
Nov 5, 2008
4,728
2,259
Kwa muda sasa nilikuwa na simama kupata msosi katika kituo hiki cha Petroli, na kupumzika kwa ingalau nusu saa kabla ya kuendelea na safari yangu ambayo huwa marathon, Dar-Mbeya.

Kituo kina mandhri nzuri ingawaje sasa kimeanza kuchakaa kutokana na kukosa matunzo.

Mbaya zaidi ni huduma ya chakula.

Mgahawa uliopo unaendeshwa kienyeji mno, hata mama Ntilie afadhali.

Chakula baridi nilikuwa served hapo majuzi, nikiuliza kwa nini, hakuna jibu.

Wahudumu wametoka vijijini na hawajui hata namna ya kuhudumia wateja kwa haraka.

Baada ya kughairi chakula, nilienda dukani ingawaje ninunue vitafunwa vya kusindikwa-duka limefungwa!

Tumewalalamikia wale ma pump attendants na walituambia hayo malalamiko wamemjulisha mwenyewe lakini hakuna kinachoendelea.

Na kwamba inawakosesha wateja wa kujaza mafuta.

Kuanzia sasa naona nitaenda pale SAS, mbele kidogo, ilipopahama muda sasa, ingawaje wao ni vitafunwa vidogo na chai/kahawa inakuwa served.
 
Mimi nipo hapa mda huu mkuu na hayo unayoyasema siyaoni !!??angalizo mie natokea Dodoma kuelekea mbeya
 
Mkuu kwa maelezo yako ni kama unadrive mwenyewe wala hushushwi na basi kula au nakosea? Kama unadrive kwannini usimame hapo si uende sehemu nyingine au pandisha Iringa ukale uendelee au jivute hadi Mafinga au Ilula kama unaenda Dar
 
Mimi nipo hapa mda huu mkuu na hayo unayoyasema siyaoni !!??angalizo mie natokea Dodoma kuelekea mbeya
Basi una bahati mkuu, nimepita hapo juzi, kuna dada kavaa jeans, ana urefu wa kati, yupo?
Nimemlalamikia sana baada ya kuletewa ugali wa baridi,.
Hebu chungulia, yule mhindi wa duka lipo wazi?
Na ulizia hao pump attendants ujuridhishe malalamiko ya wateja.
 
Kwa muda sasa nilikuwa na simama kupata msosi katika kituo hiki cha Petroli, na kupumzika kwa ingalau nusu saa kabla ya kuendelea na safari yangu ambayo huwa marathon, Dar-Mbeya.

Kituo kina mandhri nzuri ingawaje sasa kimeanza kuchakaa kutokana na kukosa matunzo.

Mbaya zaidi ni huduma ya chakula.

Mgahawa uliopo unaendeshwa kienyeji mno, hata mama Ntilie afadhali.

Chakula baridi nilikuwa served hapo majuzi, nikiuliza kwa nini, hakuna jibu.

Wahudumu wametoka vijijini na hawajui hata namna ya kuhudumia wateja kwa haraka.

Baada ya kughairi chakula, nilienda dukani ingawaje ninunue vitafunwa vya kusindikwa-duka limefungwa!

Tumewalalamikia wale ma pump attendants na walituambia hayo malalamiko wamemjulisha mwenyewe lakini hakuna kinachoendelea.

Na kwamba inawakosesha wateja wa kujaza mafuta.

Kuanzia sasa naona nitaenda pale SAS, mbele kidogo, ilipopahama muda sasa, ingawaje wao ni vitafunwa vidogo na chai/kahawa inakuwa served.
Ni kweli kabisa wanahuduma za hovyo siku hizi
 
Kwa Tanzania hii njia yenye hoteli zenye misosi ya kueleweka ni ya kaskazini tu..huko kwingine ni Mungu saidia.
 
Kuna vibinti vya hovyo pale vinajivunia urembo wa kuchonga wakati huduma mafi matupu
Tatizo kubwa zaidi ni mwenye Petrol Station.
Pamoja na uzuri wakituo huduma ni hovyo sana.
Biashara inamshinda.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom