Tawala zinazoangushwa uarabuni zitalipizia kwetu tusipojiandaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tawala zinazoangushwa uarabuni zitalipizia kwetu tusipojiandaa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by jambotemuv, Feb 3, 2011.

 1. jambotemuv

  jambotemuv JF-Expert Member

  #1
  Feb 3, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 207
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Heshma kwenu wachangiaji.
  Wanajamii uarabuni kwa bahati ya miundombinu mizuri ya mawasiliano wameshirikishana nia zao na kusema sasa basi. Hatimaye uma utashinda. Swali labaki. Je? watawala hawa watabadili mioyo?

  Nahisi hapana.
  Wakishafukuzwa kwao wataturudia. Ni kama mashetani wamtokapo mgonjwa. Wakikosa pengine hurudi kwa nguvu zaidi. Waarabu sasa tuwategemee bongo wakiwa na nguvu zaidi kuliko walizokuwa nazo walipotuuza kama watumwa. Miaka ile walitumia vibaraka miongoni mwetu na sasa serikali yetu yaonekana ipo tayari kuwatumikia tena.
  Wafanyayo mafisadi wa DOWNS, EPA, MEREMETA, IPTL etc ni mfano tu wa yajayo.

  Kuyaruhusu haya ni kuwatukana wote walomwaga damu kuupinga udhalimu miaka ile. Ni Kujilaani wenyewe.


  Kuyaazuia tutahitaji zaidi ya mawe na kelele.
  Tutahitaji idadi kubwa ya wazalendo walioelimika kwenye fani mbalimbali.
  Tutahitaji idadi kubwa ya wazalendo wanaomiliki misingi yetu ya uchumi wakilenga kujijenga zaidi hapahapa kwetu na wao.
  Tutahitaji sana utaifa.

  Haya hayapatikani kwa serikali kuwakumbatia mafisadi.
  Hayaji kwa kushusha kiwango cha elimu tufanyavyo sasa.
  Watawala wetu wa sasa yafaa waamke na kuwakabili mafisadi kwa dhati.
  Kuwapigia magoti mafisadi ni kujidanganya.Wakishaukamata uchumi majuto yatakuwa makubwa na kwa marefu.
   
Loading...