Tawala za Kiimla Huzalisha Magaidi

Wagabuli

Member
Nov 28, 2015
78
144
Wanajamii kipindi cha nyuma nilikuwa nashangaa inakuwaje mtu anajitoa mhanga kwa kujilipua na bomu na kuuwa watu, nilikuwa sipati jibu kama ni uendewazimu au ni imani kali za dini?

Lakini kwa fikra zangu siaamini kama wote ni watu waliorukwa na akili, na amini kabisa uonevu unapovuka mipaka na watu wakakosa namna ya kuukabili kwa njia ya amani, namna inayobaki ni kupandwa na hasira na kuwa na kisasi cha kupitiliza, na ndio matokeo ya machafuko mengi duniani.

Siungi mkono mauaji ya aina yoyote ile lakini pia siungi mkono uonevu wowote pia, na ukweli toka kwenye nafsi yangu nimeanza kuwa na mtazamo tofauti na watu wanaojitoa mhanga, inawezekana ni watu wanaojitambua kabisa na wanaopenda maisha ila wajinga wachache wanawafanya wafikie hapo.

Maana ikifika mahali uonevu unazidi hakuna jinsi, tukose wote au tupate wote. Huu ni mtazamo wangu, nakaribisha mawazo mengine.
 
Mleta mada hupo sahihi. Ilijullikana tu zaman ni wapalestina pekee yao ndio walikuwa wanajitoa mhanga ikaja waarabu wengine. Zamani hata siku moja hukusikia chechens akijitoa mhanga.

Kinacho shtua sasa hivi wasomali wanajitoa mhanga na kinachotisha sana maniga (waswahili)nao ndio hivyo tena wamejumuika kwenye hili kundi. Ni hatari sana kwa muafrika kuanza kujitoa mhanga kwasababu ni rahis kupumbazwa na kua zoba na anavyopenda kuigaiga

Mniga ukimkalisha Chini vizur ukamdanganya eti ukijitoa mhanga kuna msosi wa nguvu (tunavyopenda kulakula)na papuchi inakusubiria kuzim/pepon wee...
 
pemba ooh pemba, upepo mzuri marashi ya karafuu...
tuipende Zanzibar,unafki uwe mwiko! Hatutaki kuona mtu akijilazimishia mambo atakavyo yeye na kikundi chake,hatutaki serikali ya kijeshi pia,waswahili husema wengi wape,usipowapa watajichukulia wenyewe (bilashaka kwa mabavu).
 
Kuna yule aliyejichoma moto kwa hasira tunisia akaanzisha mageuzi yaliyowang'oa ghaddafi na mubarak.
 
Wanajamii kipindi cha nyuma nilikuwa nashangaa inakuwaje mtu anajitoa mhanga kwa kujilipua na bomu na kuuwa watu, nilikuwa sipati jibu kama ni uendewazimu au ni imani kali za dini?? Lakini kwa fikra zangu siaamini kama wote ni watu waliorukwa na akili, na amini kabisa uonevu unapovuka mipaka na watu wakakosa namna ya kuukabili kwa njia ya amani, namna inayobaki ni kupandwa na hasira na kuwa na kisasi cha kupitiliza, na ndio matokeo ya machafuko mengi duniani.
Siungi mkono mauaji ya aina yoyote ile lakini pia siungi mkono uonevu wowote pia, na ukweli toka kwenye nafsi yangu nimeanza kuwa na mtazamo tofauti na watu wanaojitoa mhanga, inawezekana ni watu wanaojitambua kabisa na wanaopenda maisha ila wajinga wachache wanawafanya wafikie hapo.maana ikifika mahali uonevu unazidi hakuna jinsi, tukose wote au tupate wote. Huu ni mtazamo wangu, nakaribisha mawazo mengine.
Kuna utafiti ulifanywa na chuo kimoja huko Australia,ukabaini baadhi ya vitu kama:-
Wengi wanaojitoa muhanga ni vijana wadogo,kuanzia miaka 25 kushuka baada ya kugundua kuwa wengi walioenda kupigana Iraq kati ya 137 walikuwa wanatoka Libya na lengo la wao kwenda kufanya hivo ni kulipiza kisasi kufuatana na madhira aliyofanyiwa na wababe wa kivita,amezaliwa au akiwa tayar ana umri wa kujielewa,kashuhudia ndugu zake wote wanauawa kinyama na bomu,hana cha kupoteza mama hayupo wala baba(kuna mwanajesh mmoja wa kimarekani amewahi toa ushuhuda huu kuwa wamewah baka nyumba nzima na kuwaua wote) sasa kwa hari hii umetoka kuchunga mbuzi unakuja mchana kula unakuta nyumba imeshakua kifusi hamna hata ndugu mmoja unaye mfaham aliyebaki.....na km ilivyohada ya wa middle east ukoo mzima unakaa nyumba moja,
Sasa tawala zetu zina moyo wa kujali?
Kuna viongozi wepi waadilifu kuzuia haya?
Kama hivyo tumekubaliana tufanye maamuz yetu ya kisiasa kwa kufuata demokrasia,but viongoz wetu hawatak kufuata utawala wa sheria.....unategemea nn?
Hakuna hata mila moja wala dini inayoruhusu kujitoa muhanga....hizi ni mbinu tuu za wanyonge zinazodhaniwa kuwa zaweza tumika kujikomboa
Lakini wanajitoa muhanga si wajinga km wengi tunavyodhani japo si njia sahihi ya kutatua matatizo
 
Wasiwasi wangu ni hili suala la Zanzibar, tusijeshangaa vijana wanakuwa radicalized kule. Itatuwia ugumu sana kucontrol kule ukanda wa pwani pakiharibika...chamsingi serikali iache uonevu kule.
 
Cha kushangaza ni kwamba magaidi wanashambulia nchi za kuigwa katika demokrasia !
 
Back
Top Bottom