Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 7,198
- 12,691
Kwenye utawala wa kifalme, nchi na serikali ilikuwa ni mali ya mfalme. Tofauti na kwenye demokrasia ambapo nchi na serikali ni mali ya wananchi wote, wakimuweka Rais kuwa mdhamini.
Binadamu ni social animal, na kwenye social animals wote kuna pecking order. Zamani waliokuwa wanakuwa wafalme ni wale waliokuwa wababe, kama tu kwenye maisha ya simba, mbwa mwitu nk. Hii ndiyo asili ya social animals wote.
Sasa kwenye ufalme, huyu mbabe na familia yake wanakuwa wanamiliki nchi nzima. Siku zote akili yao ipo macho kuhakikisha mali yao inastawi. Wakikopa ni wao watalipa. Wakipigana vita ni wao watagharamia. Walihakikisha wanatunza vizuri nchi hizo sababu zilikuwa ni urithi wa watoto na wajukuu wao. Mfalme alikuwa na uchungu na mali yake.
Sasa kwenye demokrasia nchi ni mali ya watu wote. Rais ni msimamizi tu. Rais hana uchungu wowote na nchi, yeye ni muangalizi tu, siyo mali yake. Na kwa kuwa msimamizi kuna faida binafsi anapata, hivyo basi, akili ya rais siku zote ni kuhakikisha anaendelea kuwa msimamizi wa mali ya wananchi, hata kama kufanya hivyo ana hatarisha ustawi wa hiyo mali. Kama kutapanya mali kutamfanya aendelee kuwa mdhamini wa mali hiyo atafanya hivyo.
Hivyo basi, binadamu kutoka kwenye mfumo wa kifalme kwenda kwenye mfumo wa kidemokrasia alijirudisha nyuma hatua nyingi sana. Mfumo wa kifalme ni bora kuliko mfumo wa kidemokrasia. Lakini sisemi kwamba mfumo wa kifalme ndiyo bora kabisa kwa binadamu. Binadamu bado hajapata mfumo bora wa kumuongoza.