Tawala za Afrika wasio wafalme waliopo madarakani kwa muda mrefu zaidi mpaka mwaka huu 2021

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,470
46,001
1. Equatorial Guinea
Rais wake Teodoro Obiang Nguema; yuko madarakani kwa miaka 41 sasa. Mbili ya tatu ya wananchi wake wanaishi katika umaskini uliotopea licha ya kuwa nchi namba 3 kwa uzalishaji wa mafuta kusini mwa jangwa la Sahara.

2. Cameroon
Rais Paul Biya; yuko madarakani kwa miaka 38 sasa. Cameroon bado ni maskini haswa ila huwa anashinda chaguzi zote!
Tangu uhuru wa nchi mwaka 1960 Cameroon imeongozwa na chama kimoja na Marais wawili tu.

3. Congo Brazzaville
Rais wao Denis Sassou yuko madarakani kwa miaka 36.Nchi ni maskini na yenye vita kila mara. Congo zote mbili ni kama zina hii laana au bahati mbaya.

4. Uganda jirani yetu
Yoweri Museveni yuko madarakani kwa miaka 34 sasa. Huwa anapenda kuliita taifa lake wajukuu zake! Alipohojiwa mara ya kwanza na BBC punde tu baada ya kuwa Rais kwamba tatizo kubwa la Africa hasa ni nini alisema ni viongozi wanaokaa madarakani muda mrefu!

5. Chad
Idriss Deby yuko madarakani kwa miaka 30. Dikteta kipenzi cha mabeberu wanoamini ni mshirika wao muhimu kupambana na magaidi Africa Magharibi

6. Eriteria
Isaias Afwerki yuko madarakani kwa miaka 27. Wananchi wanalikimbia taifa lake kwa maelfu.

7. Djibouti
Ismail Omar Guelleh anaitawala nchi hiyo kwa miaka 21 sasa. Alichofanikiwa zaidi ni kuigeuza nchi hiyo kuwa kituo pendwa cha kijeshi kwa mataifa makubwa ya nje na sehemu pendwa ya biashara ya ngono.

8. Rwanda
Paul Kagame; Anaitawala nchi hii jirani yetu kwa miaka 20 sasa. Ni bingwa wa propoganda haswa tofauti na madikteta wengine ambao hupenda kutumia nguvu tu.
Amefanikiwa kuimanisha sehemu kubwa ya dunia kwamba Rwanda imepiga maendeleo makubwa sana chini ya utawala wake.

9. Togo
Faure Gnassingbé Eyadéma; Anatawala nchi hiyo kwa miaka 16 sasa akipokea utawala kutoka kwa baba yake Gnassingbé Eyadéma aliyeitawala nchi hiyo kwa miaka 38. Familia moja ya Eyadema inatawala nchi kwa miaka 54 mfululizo!

10. Gabon
Ali Bongo anaitawala nchi hiyo kwa miaka 12 sasa akipokea utawala kutoka kwa baba yake Omar Bongo aliyeitawala nchi hiyo kwa miaka 42. Familia moja ya Bongo imeitawala nchi kwa miaka 54 mfululizo au sawa na miaka mitano ya jiwe uzidishe mara 11!

Hawa wote wanaongoza Jamuhuri sio falme!
 
Angel Merkel yuko madarakani mwaka wa 16 sasa na huu ni mwaka wake wa mwisho madarakani. Utawala wake umeifanya Ujerumani kuwa taifa lenye nguvu na uchumi mkubwa katika Umoja wa Ulaya.

Pia fahamu kwamba Ujerumani Raia wanapigia kura chama kisha chama chenye wabunge wengi kinateua Chancellor au kama hakuna chama chenye wabunge wengi muungano wa vyama unateua.Merkel amekuwa Chancellor kwa namna hiyo.

Fahamu pia kwamba Merkel hukubadilisha sheria zozote ili aendelee kubaki madarakani kwa miaka 16.

Mwisho fahamu kwamba Ujerumani ina Rais wake mwenye nguvu na mamlaka makubwa juu ya Chancellor ila huwa hayatumii mara kwa mara. Chancellor wa ujerumani ni kama Waziri mkuu tu hapa Tanzania.

Kuhusu Vladimir Putin wewe andika listi ya madikteta waliokaa muda mrefu kutoka bara la Asia.
Chancellor Merkel amekaa miaka mingapi,vipi kuhusu Vladimir Putin,Au Africa ndo tatizo?
 
Yule aliyetaka kulazimishwa atawale hadi achoke aka "atake asitake" alizima ghafla kabla mission haijatimia. Sijui angetawala hadi lini.
Hakujua kwamba taifa linazindiko la mwenge na kupokezana vijiti , haya yote yameasisiwa na baba wa taifa, Huyu mzee alikuwa vision sana.
 
Chancellor Merkel amekaa miaka mingapi,vipi kuhusu Vladimir Putin,Au Africa ndo tatizo?
Putin ni Dikteta kama wa Africa tuu,kuhusu Germany wao wana uchaguzi huru na haki bila kusahau katiba yao haina kikomo. Hata Africa kama Tume za uchaguzi zingekuwa huru na haki na Wananchi wengi wangechagua wampendae hata akichaguliwa miaka na dahari sio tatizo.
 
Katiba yao haina ukomo kwa Chancellor ila kwa Rais ina ukomo wa miaka kumi.
Putin ni Dikteta kama wa Africa tuu,kuhusu Germany wao wana uchaguzi huru na haki bila kusahau katiba yao haina kikomo. Hata Africa kama Tume za uchaguzi zingekuwa huru na haki na Wananchi wengi wangechagua wampendae hata akichaguliwa miaka na dahari sio tatizo.
 
Hulka ya kung'ang'ania madarakani haibagui rangi. Iko maeneo mengi duniani yakiwemo uliyotaja bila kumsahau Daniel Ortega wa Nicaragua. Lakini wengine ni kidemokrasia, hawalazimishi kama ilivyo Ujerumani na Uingereza
Chancellor Merkel amekaa miaka mingapi,vipi kuhusu Vladimir Putin,Au Africa ndo tatizo?
 
Back
Top Bottom