Tausi wa Ikulu wa Mwl. Nyerere bado wapo?

ninanina

Member
Jun 25, 2011
37
24
Salute kwa wewe msomaji. Kwa wale wenye taarifa, hivi wale tausi wa Ikulu kipindi cha Mwalimu Nyerere bado wapo? Kama hawapo, kuna yeyote anajua walipelekwa wapi ama waliishia wapi? Kwa wale tu wenye majibu tafadhali, siyo maswali kwa maswali.
 
Umenikumbusha mbali sana.

Nimewafurahia sana hao tausi enzi za utotoni!

Uliwahi kuingia Ikulu nini kucheza footbal na mzee Ruksa?
nina classmates wa primary walikuwa wanaingia Ikulu
wanapiga football na mzee Ruksa....
 
Yah, those good old
Uliwahi kuingia Ikulu nini kucheza footbal na mzee Ruksa?
nina classmates wa primary walikuwa wanaingia Ikulu
wanapiga football na mzee Ruksa....

Yah, those good old days, kulikuwa hakuna fence Ikulu, unasimama nje ya Ikulu kuangalia tausi, it was the best outing.
 
They are all gone.Ile miti waliyopanda wakoloni imeangushwa karibia yote na hamna jitihada yoyote ya kupanda miti mipya.Pia majengo mapya yameharibu msitu wa ikulu na kuvuruga makazi ya tausi wale wa kihistoria.
 
Nakumbuka enzi zangu Za bunge primary tumeuza Sana manyoyaaaa ya Tausi enzi hizo Rais Alhaji Ally Hassan Mwinyi.
 
Back
Top Bottom