Tatizo siyo UDOM, vyuo vyetu vinafanana!

Plato

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
420
94
Wakati wa uchaguzi nilibeza uamuzi wa tambo za wanaharakati kuandamana kuhusu wanavyuo kuondolewa vyuoni wakati wa uchaguzi.

Nilisema haikuwa ktk wanavyuo wenyewe. Wanavyuo wengi wawapo vyuoni ni mazezeta, hawana interest na fikra tunduizi zaidi ya disco na kuangalia mechi za mipira ya nje.

Tazama, wengi hawajali maslahi ya jamii ila wakiwa vijijini ndo wanavaa ngozi za kondoo ili waonekane wasomi. Kama kweli wana uchungu, wamesharudi sasa waitishe maandamano hata Dar pekee kulaani kitendo kile, hawawezi, akili hizo hawana. Kwa sasa ni bash na wiki chache tu test basi.

Nani anajua kuwa inawezekana vijana nane wa chuo kikuu wanaweza kukusanyika kuangalia pornography ktk chumba? Juzi wanashangilia kauli ya Pinda eti ataboresha mikopo. Wamesahau ahadi ya JK?
 
du! aisee umetumia jicho lako la tatu kuona hili jambo, yaani mpaka wasubiri taasisi ziwapiganie wakati wao wanaruka majoka debeni..a.k.a disco
 
Ni kweli kabisa wanachuo wa siku hizi wengi hawajui nini kinaendelea katika nchi yao, ila ukiwauliza habari za Arsenal, Manchester, liverpool utapewa maelezo hadi utashiba, Hamna kitu jamani, mambo ya ndani ya nchi yao wanaona hayawahusu.
 
Ole wake Taifa lisilo na ufahamu: taifa lisilo na ufahamu litaangamia....wake up young generation, don't let yourselves down and the generation after you. Football and porno will not put food on your mouths....study hard,
 
Ni kweli kabisa wanachuo wa siku hizi wengi hawajui nini kinaendelea katika nchi yao, ila ukiwauliza habari za Arsenal, Manchester, liverpool utapewa maelezo hadi utashiba, Hamna kitu jamani, mambo ya ndani ya nchi yao wanaona hayawahusu.

Haya huwa yanajidhihirisha wakati wa Zain Africa Challenge .....unaona jinsi vijana wetu walivyo na knowledge ndogo hata kwa mambo ya kawaida kabisa.
 
Back
Top Bottom