Tatizo siyo "Elimu ndogo ya Wananchi" au "Elimu ya Uraia"! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tatizo siyo "Elimu ndogo ya Wananchi" au "Elimu ya Uraia"!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jul 26, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jul 26, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Nimesikia mara kwa mara tena kwa lugha ya dharau ya aina fulani kuwa "Watanzania hawaju" na kuwa "Huko kijijini watu hawaelewi" na wengine wamefikia mahali pa kudai kuwa "wananchi hawana elimu ya kutosha ya uraia" na kuwa vitu hivyo ndivyo vinavyosababisha CCM ishinde.

  Nimejiuliza swali moja: Mwaka 1995 (Nyerere akiwa bado hai) kwanini kulikuwa na mwamko mkubwa wa upinzani kuliko 2000, 2005 hasa tukiangalia matokeo ya Urais? Hili ukizingatia kuwa matumizi ya cellphones hayakuwepo, internet ndiyo kabisa, na vyombo vya habari bado vichache?

  Hivi kweli tukilinganisha kuwa wananchi wa 1995 hawakuwa na uelewa wanachokitaka zaidi kulinganisha na hawa wa "digital age"?

  Nakataa tatizo haliko katika uelewa wa Watanzania.. na tutadagangana tukifiria ati tukitoa elimu zaidi, matangazo ya kwenye TV kuhusu "usia wa Nyerere" n.k utawafanya watu waamke zaidi. Ni makosa kudhania kuwa elimu zaidi ya uraia itawafanya watu wachague upinzani na kuwa kueleza zaidi mabaya ya CCM kutawafanya waichukie.

  Labda hatuangalii vitu kwa usahihi?
   
 2. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #2
  Jul 26, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Siyo kudharau wananchi wala nini lakini tatizo ni elimu ndogo iliyo changanyika na ujuaji. Watu wana perception ya mambo wanayo ona ndiyo iko sahihi na wame jiaminisha kuwa iko sahihi kwa hiyo kuwapa elimu ya uraia ni sawa sawa na kumuambia mtu mke/mume wake ni mbaya na wakati yeye kasha jiaminisha duniani hakuna mtu mzuri kama yeye.

  Kwa hiyo mkuu hilo ndiyo tatizo letu. Wengi wetu hatujui kitu kutokana na elimu ndogo lakini hatu kubali kuonekana hatujui na kujifunza. Na mjuaji siku zote hubaki mjinga maana hayupo tayari kuuliza maswali au kubadili fikra hata akionyeshwa ukweli.
   
 3. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #3
  Jul 26, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Mwanakijiji uko sahihi kabisa.Lakini je umeshafanya utafiti na kuweza kufahamu ni kundi lipi lilokuwa na huo mwamko?je ni wasomi,vijana au wapi?umefuatlia na kujua vote ditribution za Mrema alizozipata mwaka 1995 zilitoka wapi? na je ni hasa kilipelekea watu hawa wakawa na huo mwamko?na je umepimaje mpaka unaona kuwa mwamko wa 1995 ulikuwa mkubwa kuliko miaka ya hivi karibuni?
   
 4. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #4
  Jul 26, 2010
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mkuu Mwanakijiji, naona kwenye hii hoja yako dhana ya elimu umeipatia maana nyembamba sana.

  Mfano uliotumia wa Mrema/ Upinzani mwaka 1995 hautoshelezi kujenga hoja kuwa wananchi wana elimu ya kutosha ya uraia au hawana. Pengine, mfano huo huo unaweza kuwa kigezo tosha kujenga hoja kuwa Watanzania ni malimbukeni inapokuja kwenye kupiga kura. Mwaka 1995 kura alipigiwa Mrema na siyo upinzani (kwa maana ya Sera zao). Iwapo kama Watanzania wangekuwa wamepigia kura kwa sababu ya Sera wanazo zikubali za Upinzani ni dhahiri kuwa mpaka leo Upinzania ungekuwa na nguvu sababu sera zao hazijabadilika sana. Tena zaidi kwa sababu CCM wamejiwekea madoa kutokutimiza baadhi ya sera zao.

  Leo hii Kwa kiwango kikubwa sana CCM inapigiwa kura kwa sababu ni CCM ( the brand) na uwepo wao karibu na Wananchi (nyumba kumi, Serikali za Mtaa n.k). Huenda utakubaliana na mimi kuwa yakifanyika majaribia ya kuondoa viongozi wote kutoka CCM na kuwahamishia Chadema na wale wa Chadema kuwaleta CCM (wa hame na sera zao au sera za Chadema ziwe CCM na vice versa)...ukifanyika uchaguzi CCM yenye wakina Mbowe na Dr Slaa itashinda bila ubishi.!!

  Sasa kama tatizo sio Elimu (kwa mapana yake) basi nitakuwa wa kwanza kukubali sijui maana ya Elimu.
   
 5. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #5
  Jul 26, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kiini mach kilich nje ya pazia ndiyo kinafanya CCM ichaguliwe na wanaoichagua si wa vijini na wasiosoma, wengi wao ni wasomi waliobobea ukiangalia maprofesa,madr(phd)na wasomi wakubwa wangapi wako CCM kwa kuganga njaa hata kujiamini kwao kama wasomi hakupo tena. Ninaona na kuamini siri ya ushindi ni njaa na umbumbu wetu watanzania waliosoma na wasiosoma hatujui kipaumbile tunataka nini ili tuendelee na kwa kuangalia wasaliti wakubwa ni wasomi kwani wanaufahamu mkubwa ila njaa na kutafuta nyeo vya kisiasa vinawafanya wawe vipofu
   
 6. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #6
  Jul 26, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Ur very genius.Hoja yako imenikuna.Unajua tatizo kubwa watu hatujafanya analysis za kutosha kujua why Mrema alipata votes zote hizo?je ni kwasababu alikuwa ni Mrema au ni upinzani?na hata kufahamu ni makundi yapi hasa yaliyomuunga mokono Mrema and why the y did so. Nikubaliane na wewe na hoja zako zote why CCM wanapata votes nyingi huko vijijini..
   
 7. T

  Tom JF-Expert Member

  #7
  Jul 26, 2010
  Joined: May 14, 2007
  Messages: 472
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  TZ kumejaa ushabiki, hata siasa zetu ni hivyo hivyo: eti ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya utadhani kulishawahi kua na mwamko wowote na ukapotea. Watu wetu elimu wanayo inatosha lakini 'mamillion ya JK' yanafanya kazi yake na pia CCM imefanikiwa sana kupumbaza akili za watu kiasi kua hamna anayejali nani ni raisi ili mradi ameletwa na NEC ya CCM.
  Nyerere alileta mwamko wa upinzani, sidhani. Nyerere enzi zake aliweka wapinzani kizuizini, akasema makabila makubwa km wachagga, wahaya nk ni wakabila na akaunda utaratibu unatumika hadi leo ambapo minority ndio hutoa maraisi. Kwa amani na utulivu kila mmoja kadharau na kukubali hali ilivyo ili mradi tumbo linashiba - lakini ndio miafrika ilivyo.
  Hata wapinzani nao ni waafrika, waafrika hawajaonyesha uwezo wa kuongoza na kuinua jumuia zao zaidi ya kujijali mmoja mmoja.
   
 8. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #8
  Jul 26, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Wasomi ndio wanatuangusha na hasa wahadhiri wa vyuo vikuu. Wanapotoa lekcha zao wanachambua vizuri sana mapungufu ya serikali na wanaamsha ari ya wanafunzi wao kujiunga na upinzani au kuwaunga mkono. Lakini mwisho wa siku hao wasomi ndio wanakuwa wa kwanza kunadi sera za sisiem ambazo kutwa walikuwa wakiziponda!
   
 9. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #9
  Jul 26, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Napenda kuchangia kwenye hili la kuwa na uelewa, ufahamu au taarifa japo sitahusisha na siasa.

  Uzoefu wangu unaniambia kuwa Watanzania kwa miaka ya sasa wana uelewa wa mambo mengi sana kuanzia mijini hadi vijijini. Lakini tujiulize wanafanya nini na uelewa huo? Mathalani mtanzania anapokuwa na ufahamu kuhusu haki zake za kisheria, ina maana hatadhulumiwa haki zake? Au anapofahamu kuwa huwezi kupata mkopo benki mpaka uwe na dhamani, ina maana ufahamu huu utamsaidia kupata dhamana? jibu rahisi ni LA HASHA! More needs to be done ili uelewa huo uweze kumsaidia.

  Tuna wasomi wengi zaidi miaka ya sasa kuliko "ENZI ZA MWALIMU"... watu wana madigirii hadi hawajui wafanye nayo nini.Watu wako more exposed miaka hii kutokana na utandawazi - wanapata elimu au ufahamu kupitia technolojia za mawasiliano - TV, internet etc........ je inawasaidiaje kubadilisha maisha yao yawe bora?
   
 10. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #10
  Jul 26, 2010
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mkjj, kwanza kabisa ahsante kwa hoja.
  Pili, naona hili swala la 'mwamko vs elimu' ni gumu kulielezea hata kwako (mmoja wa wachache wenye upeo na udadisi mpana zaidi na hali ya kisiasa hapa Tz kuliko tuliowengi). Kwa maelezo machache uliyojaribu kutoa hapo juu, kuna maswala yaonekana kujikanganya moja juu la jingine. Kwa maoni yangu kuhusu huu mkanganyiko, ni dhahiri kwamba kuna kitu hakipo. Kitu hicho nadhania ni research ya hili swala kwa undani zaidi. Kwani pale unapotaja kutokuwepo kwa mapungufu ya elimu, au hiyo elimu ya uraia, na wakati huohuo kutaja kwamba mwamko wa wananchi katika ku-support upinzani ulikuwa mkubwa zaidi huko nyuma sembuse na sasa hivi kwenye digital age; hapo panakuwa na mambo yaliyojichanganya. Na katika kujaribu kuchanganua na kupata majibu, inabidi kujiuliza baadhi ya maswali:

  -- Je, hapo awali mwamko huo unaousema wa wananchi kujua wanachokitaka ulisababishwa na nini? Elimu yao kiujumla, au elimu ya uraia?
  -- Je, elimu ya uraia inapatikana vipi hivi sasa kulinganisha na hapo awali?
  -- Je, influence ya Mwl. Nyerere ilitawala kwa kiwango gani katika swala zima kulinganisha na sasa? Bado ipo au ilishajifia?
  -- Je, mwananchi mwenye elimu kutoka kwenye mitaala yetu tuliyoizoea anatofauti gani na yule mwenye elimu ya uraia pekee?
  -- Je, kwa wenzetu wanaochagua upinzani, au wale wanao badilisha serikali zao mara kwa mara zinapovurunda kupitia demokrasia ya uchaguzi wanafanikisha hilo kutokana na yapi?!
  -- Je, elimu ya uraia na kuwepo kwa upinzani mkubwa kivyama kunaendana na tabia za watu (jamii) wa pahala fulani?!
  -- Je, swala la elimu kiujumla (ya mitaala na uraia) linachangamana vipi na swala la mwamko wa kisiasa?! Yanaendana, ni lilelile, au hayafungamani?

  Maswali ni mengi, na kwa kweli kama nilivyodokezea hapo awali, hili linapelekea kuwepo kwa kila aina ya research kwenye nyanja hii, haswa pale zinapoonekana kutokuwepo kabisa kwenye jamii yetu tangu mfumo wa vyama vingi ufurumke!

  Mkjj, nimetumia neno 'ufurumke' hapo juu makusudi, kwani namna jinsi vyama vya upinzani viliposhika hatamu awali ilikuwa kwa mfurumko. Kuna jambo ambalo nimeshaongelea nawe mara nyingi, naro ni swala la wananchi kuwa na uwezo wa kung'amua ubaya na uzuri wa viongozi walionao sasa hivi na hapohapo kujua kuwa wana nguvu kubwa ya kidemokrasia ya kumng'oa kiongozi yeyote yule waliomchagua wao pale wanapoona amekejeli matakwa yao na kutotimiza ahadi zake. Sasa kama hili ni swala la elimu kiujumla, kama hili ni swala la elimu ya uraia, au kama hili ni swala la mwamko wa kisiasa pekee; hapa ndipo penye kuhitaji majibu kwa maoni yangu.

  Katika kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi kisiasa, natamani sana kama Mwl. Nyerere kutokana na influence yake alipokuwa hai na akiwa bado ndani ya CCM angeli-endorse kuvunjwa-vunjwa kwa CCM na kukifanya kiwe vyama viwili vinavyotofautiana katika baadhi ya mambo, au kuivunja kabisa na kuiweka kibindoni kwa muda, nchi kuongozwa by an interim government, kisha kutangaza mchakato wa kuunda vyama vya kisiasa, vile vyenye mrengo wa kushoto, kulia na vile vya mrengo wa kati. Well, hii ni ndoto iliyochelewa, CCM ilishabarikiwa kuwa na nguvu and I think Mwl. Nyerere must have known the foreseeable problem but chose to ignore it. Naongelea tamanio hili kuwepo wakati wa mwanzo wakati wa Nyerere, kwani CCM imekuwa na disproportional advantage over other parties. Wakati vyama vingine vinaanzishwa, CCM ilikuwa na financial backup ya kutosha, vitega uchumi kama viwanja vya michezo na majengo vilikuwa na bado viko mikononi mwake. Kujulikana na kuwa favourite party kulikuwa na bado kunaendelea kuwa. Hivyo platform nzima ya kuwepo kwa vyama vingi haikuwa stable na hiyo hilo kwa maoni yangu laweza kuwa jambo moja ambalo limezorotesha upinzani kwa mapana.

  Swala la kuaminika kwa Nyerere na influence yake katika society ni moja ya jambo muhimu kwenye hii equation ya elimu ya uraia-vs-mwamko wa kisiasa. Mwamko ulipo sasa hivi unaweza kuwa umezorota kulinganisha na wakati ule wa mwanzo kutokana na ukweli kwamba wananchi wengi walimwamini sana Mwl. na bado wengi wanaendelea kuamini mambo yake mengi (wengine hata kuamini bado yu hai!), hata sisi hapa mtandaoni wengi wetu tunamkubali kuwa he was a patriotic person na tunaenzi mengi aliyotuachia. Lakini katika kuenzi haya mengi aliyotuachia, tunasahau mojawapo ya aliyotuachia ni CCM. Personally, I wish he quitted from CCM na kukifanya kisimame dede chenyewe (not forgetting that kilisha simama tayari) just for the sake of trying to put all parties on an equal footing. Kwani kutofanya hivyo ameicha CCM na ameacha legacy kwamba CCM ni chama cha Nyerere na kilichoikomboa Tanzania. Kwenye jamii ya watu ambao elimu ya msingi ni darasa la saba na vyanzo vya habari kijamii kwa ukubwa viko controlled na CCM, bila shaka wanajamii wengi watakuwa ni wanaCCM. That plus the current voracious propaganda machinery iliyopo ndani ya CCM isiyo na lengo la kuendeleza upinzani (kama moja ya nguvu ya kuleta mabadiliko chanya Tz) kama jinsi vile mwasisi Nyerere angelipenda iwe bali kuuua kabisa kabisa; hapo wananchi wanakuwa na only one option, nayo ni CCM. Maana through media wanakuwa wametishiwa kuhusu upinzani na kulaghaiwa vya kutosha.

  Swala la elimu ya uraia-vs-mwamko wa kisiasa linaweza pia kuchanganuliwa kwa kuangaliwa kwa kuweka jicho la kengeza kwa wenzetu waliofanikiwa katika haya. Jicho la kengeza maana jamii zinatofautiana, Watanzania siyo Wakenya, siyo Wahispania, siyo Waingereza na siyo Wazimbabwe wala Waamerika. Inabidi kuangalia pahala tu pale system zinapo-cross link. Katika mfumo wetu wa vyama vingi, ni wapi jamii yetu inafanana na hizo nyingine, kielimu za mitaala, elimu ya uraia au basi hili swala zima tunalolipatia jina la 'mwamko wa kisiasa'. Je, wamefanikisha vipi hayo yote kwenye ulimwengu huu wa utandawazi hali hapa kwetu upinzani ukififia?!

  Ngoja niishie hapa, ila kama nilivyosema Mkjj, hili swala tunaweza kulikimbia kuwa siyo tatizo la elimu, au basi kusema kwamba ni tatizo la elimu ya uraia; lakini ukweli unabakia palepale, tatizo lipo na tatizo hili la wananchi kutokuwa na nia au uwezo wa kung'amua viongozi bora ni wapi na wale wanaovurunda ni wapi kisha kuwabadilisha chaguzi zinapotokea limetapakaa nchini mwetu. Ni tatizo sugu na nitatizo linalozidi kuturudisha nyuma kama Taifa. Laiti tu wananchi wa Tanzania wangeliweza kutambua wana nguvu kubwa sana kama raia wa Taifa hili (isiyo hitaji elimu wala mwamko wa kisiasa) ya kuweza kubadilisha viongozi wabovu, nchi yetu ingelishapiga hatua kubwa. Tatizo, chama kilichopo madarakani, CCM yaonekana kabisa haitaki wananchi watambue nguvu hii.

  Ahsante.

  Steve Dii
   
 11. W

  WildCard JF-Expert Member

  #11
  Jul 26, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Mwaka 1995 tulidhani tuna upinzani wa kweli. Tukadhani kutakuwa na sera/itikadi mbadala wa hizi za CCM zisizotekelezeka. Tukadhani pia VIONGOZI wa upinzani ni tofauti kiuongozi, kiitikadi, kiMAADILI na hawa wa CCM. Yote haya hayakuwa kama ilivyokuja kujidhihirisha baadae.
  Tukagundua kumbe watu walikuwa wanasaka vyeo, madaraka, utajiri, umaarufu na mambo kama hayo. Mwalimu naye ana mchango wake kuturudisha CCM hasa aliponyanyuka kumfanyia kampeni Mkapa. Baadhi yetu tukamwamini kama ambavyo tumekuwa tukimwamini siku zote. Tulikosea. Na hasa baada ya kuwa amefariki. Tukawa na Mkapa mwingine kabisa.
  Dr Slaa sio mtu wa kubadilikabadilika hasa kwa masuala ya MSINGI. Anaweza asiwe hivo pengine akiupata URAIS na akajizungushia wajinga, wanafiki na waroho. Akiendelea kubaki JF na akawa msikivu tatizo hili anaweza asiwe nalo. Humu JF hatumchekei mtu.
   
 12. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #12
  Jul 26, 2010
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Watanzania hawajui, Hawaelewi, Hawana elimu ya kutosha = T-shirt, kanga za India, Pilao na pombe za kienyeji, Hakuna hata mtanzania mmjoja aliyewahi kuuliza hizo pesa zimetoka wapi na kwanini zisiletwe kabla ya msimu wa uchaguzi. Wengi wanaopewa hivyo vitu humwona mtoaji ni mtu mwenye roho nzuri na anyefaa kuwa kiongozi!
  Nikiwa kijijini kwetu week kama mbili zilizopita nilimwona mama mmoja kavaa T-shirt iliyoandikwa chagua mkapa, ni mpya kabisa!! Maana yake hiyo ni nguo nzuri kabisa kwake aliyotunza kwa ajili ya mtoko!!
  NInachoamini mimi ni kuwa hawajui na hawawezi kujua! kwa kifupi elimu duni kwa watanzania ni Sera ya CCM!
  Kama sivyo Swali ninalojiuliza, 60% ya watanzania wote wakipata elimu ya form 6, CCM ya sasa itaweza kuwa madarakani!
   
 13. W

  WildCard JF-Expert Member

  #13
  Jul 26, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Unaongelea 60% ya Watz kuwa form 6? Zaidi 70% ya watu wapya waliochukua fomu kutafuta nafasi ya kuteuliwa kugombea Ubunge kwa tiketi ya CCM ni Graduates wa miaka ya hivi karibuni.
   
 14. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #14
  Jul 26, 2010
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Wasomi sio tu wanatuangusha kwenye kupiga kura lakini pia kwenye kushirki kuomba nafasi za kuchaguliwa na kupigiwa kura. Mimi naamini wananchi wa vijijini ndio tulioathirka zaidi na sera za CCM, sisi ndio tunao tembea umbali mrefu kufuata kuni, maji, zahanati, shule, nk. sisi ndio kila siku tunatoa michango ya kujenga madarasa na vyoo vya shule pesa zinazoishia mikononi mwa wenyeviti wetu wa halmahsauri za wilaya, madiwani na watendaji wa wilaya na madarasa hayaishi miaka nenda rudi. Kwa ujumla tumechoshwa na tunataka sana mageuzi na kuweka watu wapya kutoka vyama mbadala, lakini wapi tunashindwa??? Kwanini hatuwezi??

  Tunashindwa kutekeleza dhamira yetu hiyo kwasababu Vyama vya upizani na wasomi wanatuangusha. Vyama vaya upinzani Wanateua wagombea wazuri na wenye sifa nzuri kugombea mijini na sio vijijini, majimbo ya vijijini ambayo wapinzani waliweka wagombea wazuri kama akina Slaa, akina Zitto, Ndesamburo, wapinzani walishinda, lakini majimbo ya sisi wengine wanaweka mtu hawezi hata kueleza chama chake kinaamini nini??


  Nitawapa mfano wa jimbo langu la Makete:

  Mwaka 1995 jimbo la Makete lilikuwa na wagombea wawili wa ubunge Aliyekuwa anatetea nafasi hiyo Mh. Tuntemeke Sanga akipambana na msomi wa Form six mwenye diploma ya uhasibu(UDP), sasa utaona mwenyewe nchi nzima ilikuwa inamfahamu Bw. Tuntemeke kwa Makeke, ubishi, uwezo wa kujenga hoja na msimamo thabiti, achilia mbali shule yake ya degree 5, unadhani wananchi wa Makete wangeweza kuweka rehani jimbo lao kwa kijana wetu wa form six ambaye hana uzoefu kwenye medani za kisiasa?


  Mwaka 1997 Mh. Tuntemeke alifariki ukaitishwa uchaguzi mdogo. CCM walimteua Dr. Hassy Kitine (PhD) wakati huku upinzani ukimteua mgombea wao kwa ticket ya NCCR- Mageuzi (Form IV hana hata cheti cha kozi) Wote mnamfahamu Kitine kuwa alikuwa ni Mkurugenzi wa usalama wa Taifa, na mkuu wa mkoa wa Tanga, na baadaye waziri unadhani ingekuwa rahisi kwa huyo mpinzani kushinda kwa kungalia CV tu achilia mbali kutumia vijana wake wa UWT kufanya kile kinachowezekana kufanywa. Lakini pia Wananchi wa vijijini sio washamba kiasi hicho cha kulinganisha Form IV na PhD na kwenda kwa Form IV bila sababu za kueleweka.


  Mwaka 200 yakarudiwa yale yale Kitine akashinda tena


  Mwaka 2005. CCM walimteua Registrar wa DIT Dr. Binilith Mahenge (PhD) Upinzania ukamsimamisha mgombea kupitia CHADEMA safari hii tena kijana wa Form IV, pamoja na uwiano mbaya wa uzoefu na elimu wa wapinzani na wagombea wa CCM bado unakuta hawa wagombea wa Upinzani wanapata kura za kutosha kitu amabacho naamini kama wananchi wa kijijini wangeletewa wagombea wazuri kutoka upinzani wangewachagua tu. Baada ya uchaguzi huyu kijana akarudisha kadi ya CHADEMA akapewa utendaji wa kata, sasa hivi anafisadi nchi kwa kwenda mbele, mbolea za ruzuku, ndio fringe benefit zake.


  Wasomi sio tu washiriki kwenye modahalo na kupiga kura naamini kama watashiriki kugombea na kutafuta nafasi za kuongoza kutoka huko vijijini watatusaidia sana watanzania. Bila kubadirisha namna wagombea wanavyokuwa allocated, Bunge litaendelea kutawaliwa na CCM
   
 15. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #15
  Jul 26, 2010
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Katika yote uliyoandika, nimesoma hapo pekundu tu! MMKJ kaja na madai ambayo hayana fact! And as usual...kaingiza emotions kusudi watu tuvutiwe zaidi na ku-side naye! - mfano: "lugha ya dharau", nk. Mwisho wa siku, its clear kuwa hana fact zozote zinazobeba mada yake! CCJ imemmaliza! Nafuu angesema kuwa anaamini kuwa WaTz wana elimu ya uraia ya kutosha. Lakini kuja kuweka haya madai kama facts si busara!
   
 16. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #16
  Jul 26, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,552
  Likes Received: 18,238
  Trophy Points: 280
  Mzee Mwanakijiji, nimekusoma ila sina uhakika kama nimekuelewa sawasawa.
  Mimi naamini ukweli kabisa toka ndani ya moyo wako kuhusu kuchaguliwa CCM na kuendelea kuchaguliwa na kuchaliwa unaujua vizuri tuu, ila sasa unahoji ili kuthibitisha hata eulewa ukifikia asilimia 100%, bado CCM itachaguliwa, nakuhakikishia no, a very big NO!.

  Nimebahatika kushuhudia chaguzi za 1995, 2000, 2005 ambazo zote CCM imeibuka kidedea, na huu ujao 2010, things will not be the same again, belive me kama wananchi watahamasishwa madhila yote yanalolikuta taifa letu hili lenye utajiri wa asili, udongo wenye rutuba, vyanzo lukuki vya maji, madini ndio usiseme, yamesababishwa na CCM, wananchi wakikubali kusema basi, mambo yatabadilika. Nakuhakikishia, asilimia 100%, CCM inaangukia pua!.

  Naamini kabisa Mzee Mwanakijiji, uwezo wa Dr. Slaa kiongozi, ability to lead, unaujua, na ukimlinganisha na JK, lazima utakubali JK si lolote, si chochote mbele ya DR. Slaa, ila unaijua nguvu ya JK sio uwezo binafsi, bali atacapitalize na mtandao wake wa CCM uliotapakaa nchi nzima, ila pamoja na huo mtandao, wana CCM nao wakielimishwa uchafu wa CCM, t-shirt na kofia watavaa, pesa watapokea na pilau watakula, lakini kura watapigia kwenye ukweli, na sio kwenye ubatili tena.

  Chaguzi ndogo za Tarime, Busanda na Biharamulo zimenifundisha mengi, ile nimefika mahali nimekubali Watanzania sio mazuzu tena, wanaweza kupembua pumba na mchele, kile kipindi cha bendera fuata upepo, na huyu ni mwenzetu, soon kitapita with much awareness kampaign na ule utabiri wako, mimi naita Unabii wa Anguko La CCM, utatimia!.
   
 17. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #17
  Jul 26, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,176
  Trophy Points: 280
  Mbogela umesema vizuri, lakini hufikiri kuwa judge wagombea kwa elimu ya darasani - hususan ukizingatia wananchi wetu wengi hawajapata elimu ya kutosha ya darasani- ni sawa?

  Hao wasomi wanafanya kazi vizuri? Wanapunguza matatizo ya wananchi inavyotegemewa?

  Maana inawezekana form six akawa anawajibika vizuri kwa wananchi kwa sababu hana kiburi cha usomi kama hao ma PhD wanaojiona huu ubunge ni haki yao ya kuzaliwa na hawatetemeshwi lolote na wananchi wa vijijini.

  Mwanakijiji unasema tatizo si elimu ndogo ya wananchi, una maana tatizo ni wapinzani hawana mipango thabiti ?
   
 18. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #18
  Jul 26, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Suala la elimu kwa wananchi nalikataa pia? Sidhani kama kuna msomi yeyote nchi hii asiyejua ni kiasi gani tuna poteza kwa kuendelea kuwalea CCM madarakani! Na siidhani kama kuna mtu yeyote asiyejua suluhisho la matatizo haya yote ni kutowapa nchi CCM ambao wameshindwa kuleta maendeleo kwa miaka zaidi ya 50. Cha kushangaza maprof na waosomi wengine kibao wanakimbilia CCM kugombea viti njaa na ubinafsi ndio vinawatawala watz. Kama ni elimu basi maeneo ya mijini tungetarajia kuona upinzani mkali. Shida inayotukabiri watz ni ushabiki, uoga wa kuthubutu, na ubinafsi. Hakuna mwenye nia njema na nchi hii! Tena wananchi wa vijijini naweza kusema wanamwamko mkubwa zaidi kuliko wale mjini! Ndio with all the information magazeti, Television mitandao simu nk....nk mtu unashidwa kuona tunaibiwa kiasi gani? Kuna viongozi wenye nia ya kuleta maendeleo kweli CCM. Tangu tupate uhuru mpaka leo nini cha zaidi kimefanyika!
  Mafisadi yanacheza ngoma barabarani no body cares! Mapato ya nchi yanahujumiwa kila siku nobody cares. Miradi ya maendeleo hakuna kinachofanyika kama sio ujanja ujanja tu. Cha kushangaza hata mambo yaliyokusudiwa kufanywa yanaposhindwa kufikiwa hakuna anayejali!
  Kilimo kwanza kiko wapi? Mradi pembejeo uko wapi? Mradi wa mabasi yaendayo kasi uko wapi? Rushwa bandarini nani hata amejaribu kulisemea! watu wasio na hatia wanapigwa risasi kisogoni na ushahidi unatolewa mahakamani at the end mtuhumiwa anaachiliwa huru tena kwa mbwembwe! viongozi wa nchi wanachekelea tu!

  Haya yote yakifanyika mwananchi unahitaji usomi gani wa kuyaelewa? hakuna mlinganyo hapo! Mwananchi!!!! Fungua macho!!!
   
 19. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #19
  Jul 26, 2010
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Mkuu upo sahihi kuwa kuwahukumu wagombea kwa elimu yao ya darasani sio sahihi, nakubalina na wewe, pia uko sahihi kuwa wagombea wenye Elimu ndogo wanaweza wakawa viongozi wazuri zaidi na watakaowajibika kwa wananchi NAKUBALIANA.

  Lakini HAPA kumbuka tunaongelea kushinda na kuchagulika na wananchi wakati wa kampeini na siku ya kupiga kura. Mpiga kura hawezi kujua kuwa mgombea atakuwa muwajibikaji na msikivu kwa wananchi asiye na kiburi kama mgombea hajajenga hiyo hoja ikawaingia wananchi vizuri, na kujenga hoja kunahitaji mambo mawili, aidha kipaji au shule. Sasa unaweza ukawa na nia njema lakini ukashindwa kujenga hoja jambo ambalo linawezekana limetokana na upeo wako mdogo wa elimu na ukishindwa kujenga hoja unashindwa kuwashawishi wapiga kura na ukishindwa kuwashawishi unaangushwa na matokeo yake Kambi nzima ya Upinzani inaangukia pua na kutokuaminika kwa wananchi. Nilichotaka kusema kwa 2010 CHADEMA wajipange sana kwenye suala la Ubunge na Udiwani, nadhani watumie mtindo walioufanya kumpata mgombea URAIS, kama kuna watu na wanachama wao wazuri ambao hawajaonyesha nia ya kugombea wawaombe wakagombee kwenye majimbo yao ya uchaguzi, hili la kusubiri mpaka watu wajitokeze, watu wanaogopa jamani kuweka vibarua vyao walivyopata wa mizengwe rehani unless kuna insurance fulani, hata ya support tu inatosha. Elimu ya Uraia inakosekana kwa wenye sifa za kuwa wagombea.
   
 20. Bramo

  Bramo JF Bronze Member

  #20
  Jul 26, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 9,452
  Likes Received: 2,502
  Trophy Points: 280
  Ladies and Gents.
  Nadhanni hatulitumii jukwaa hili ipasavyo,i came to realize that hapa ndani JF kuna watu wanjua sana kujenga hoja..MM akiwa ni mmoja wapo,na wengine wengi tu...
  Nadhan its high time now kutumia jukwaa hili kuelezezana mikakati mbali mbali itakayowezesha watu makini kama Dr. Slaa kuweza kushinda uchaguzi...napinganana mawazo ya MM,hayana facts zozote na yanakanganya wa Tanzania kwa kiasi kikubwa,yanazidi kuwaaminisha wa Tanzania kuwa CCM itatawala milele.
  Its high time now kuelimishana na kuelezana kwanini hatuihitaj CCM tena,tujenge hoja zenye fact za kuwa convice wapiga kura wasichague tena CCM,sio kukaa na kujadili oooh,CCM itashinda..na blah blah nyingi tu ambazo zinachelewesha ku create awareness among Tanzanians on the torturers CCM wametupatia katika kipindi chote tokea uhuru.

  Nashauri tuanze na Ajenda ya ufisadi wa Kagoda,meremeta Deep Green Finance n.k

  Nawakilisha
   
Loading...