Watanzania,
Serikali imedhamiria kuipunguzia Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) majukumu ya udhibi wa vyakula na vipodozi na kuibadilisha jina kuwa Mamlaka ya Udhibiti wa Dawa na Vifaa Tiba (TMDA). Hatua hii ya Serikali ni kutokana na kufanyia kazi malalamiko ya wafanyabiashara juu ya utendaji wa mamlaka husika.
Hata hivyo, kwa maoni yangu sioni hatua hii ya serikali italeta tija na kuondoa malalamiko kwa biashara dawa na vifaa tiba. Ukiangalila juu juu unaweza kudhani watendaji wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) wako “serious” na wazalendo kweli kweli wa nchi yao katika udhibiti wa ubora wa bidhaa husika. Ukweli ni kwamba, sio kero kwa wafanyabiashara tu, watendaji wa mamlaka hii wanaihujumu serikali. Tatizo ni hujuma, urasimu na rushwa iliyokithiri kwa watumishi wa mamlaka hii. Leo nitaelezea urasimu, hujuma na rushwa zinazofanywa na watumishi wa mamlaka hii.
HUJUMA
Kwa mujibu wa kananuni na taratibu Za kufanya malipo kwa TFDA (Tanzania Food, Drugs and Cosmetics (Fees and Chargees) Regulations) inaelekeza hivi; nanukuu.
Kinyume chake, viwango vya malipo vimekadiriwa kwa dolari ya Kimarekani peke yake. Maana yake ni kwamba viwango vya malipo kwa wateja walio ndani ya nchi (wanaotumia shilingi ya Tazania) hubadilika kila wakati kutegemea na thamani ya dolari ya Marekani dhidi ya shilingi ya Tanzania. Sasa kutokana na kubadilika mara kwa mara kwa shilingi ya Tanzania dhidi ya dolari, TFDA huweka kipindi cha wiki moja tu cha uhalali wa proforma invoice wanazotoa kwa waombaji wa vibali.
Kwa kufanya hivi TFDA sio tu wanakiuka utaratibu wa kisheria na sera za nchi, bali wanahujumu uchumi na kuwaumiza wateja wao wa ndani na kuwapa nafuu wale wa nje. Huu si uzalendo. Lakini, endapo shilingi yetu ingetumika kama kigezo, dola ndio ingekuwa inabadilika na kusingekuwa na haja ya kuweka kipindi maalumu cha uhalali wa invoice kwa wateja wa ndani.
URASIMU
Ingawa zaidi ya 80% ya maombi ya vibali vitolewavyo na mamlaka hii hufanyika kwa mfumo wa kielektroniki kwa ajili ya kurahisisha na kuharakisha michakato, matumizi ya mfumo huo haisaidii kwakuwa kuna urasimu wa kiwango cha juu. Kuna wakati mteja hulazimika kupiga simu au hata kufika kwenye ofisi za mamlaka ili kuwajulisha au kuwahimiza wafanyie kazi maombi yaliyotumwa kwa njia ya kielektroniki. Na maombi yanapopokewa, bado hayawezi kuidhinishwa mara moja; lazima watoe “query” na kila query itakayojibiwa lazima izae query nyingine na nyingine.
Query ni wito unaomtaka mteja kukamilisha matakwa Fulani, vielelezo au ufafanuzi kuhusu bidhaa inayoombewa kibali ambavyo bila kufanya hivyo mamlaka haitoi kibali kinachoombwa. Mathalani, unapotaka kuingiza bidhaa ambayo ni kifaa tiba utajaza fomu ya maombi na kuambatanisha nakala zote zinazohitajika ikiwa ni pamoja na risiti ya malipo, utapokea query inayosema “bidhaa hiyo haijasajiliwa na TFDA na kwahiyo hairusiwi kuingizwa nchini bila usajili”. Majibu ya query hii kwa mtuma maombi ni kusema “Bidhaa hii ni kwa ajili ya matumizi ya utafiti”. Mamlaka itakutumia tena query kukutaka uambatanishe “ethical clearance” ya kufanya utafiti. Wewe kama mfanyabiashara utajibu ethical clearance haikuhusu bali mteja wako aliyekutaka umsambazie ndiye anayehusika. Ukijibu hivyo TFDA watatoa query inayokutaka usajili hiyo bidhaa ndipo upate kibali cha kuingiza.
Ili muombaje asipoteze biashara itamlazimu kusajili. Sasa kwa bidhaa hiyo hiyo moja utalazimika kujaza fomu ya maombi ya usajili na mwishowe unapewa proforma invoice ya kulipia ambayo ina thamani ya $1500. Kumbuka usajili ni mchakato na unatakiwa utengeneze “dossier” na wakati Fulani uambatanishe na sampuli ya hiyo bidhaa. Sasa mbali na kulipia registration fee ya $1500, itakubidi pia uagize bidhaa andalau moja kwa ajili ya kuwasilishwa kwenye mamlaka kama sample.
Muombaji akiweza kutimiza hayo yote ni heri kwake; lakini je ataweza kupata usajili wa hiyo bidhaa ndani ya mweizi mmoja ili aweze kumsambazia mteja wake? Uzoefu unaona kuwa TFDA huwachukua miezi 6 hadi 10 kukamilisha usajili wa bidhaa. Vile vile ikumbukwe kuwa ukiweza kulipia ada ya usajili na wakifanyaa evaluation wa dossier uliyowasilisha, bado huwezi kupata kibali kwasababu utakapofuatilia utaulizwa (query nyingine), je ulilipia gharama kufanya GMP inspection? GMP ni good manucturing practice yaani ili bidhaa husika ipate kibali sharti kwanza kiwanda kinachozalisha hiyo bidhaa kikaguliwe na TFDA kuona kama mchakato wa uzalishaji unakidhi viwango vyake vya ubora. Gharama ya kufanya GMP inspection ni $6000 – 8000 kwakuwa kiwanda cha bidhaa husika kiko Ulaya au Markani. Kiwango hiki ni gharama ya kuwatuma wakaguzi kwenda nje ya nchi kufanya ukaguzi.
Kwa kweli huu ni urasimu usio wa lazima. Bali TFDA wanafanya kusudi kutoa invoice ya malipo ya usajili wa bidhaa bila kujumlisha na gharama ya ukaguzi wa GMP. Wanafanya hivyo ili kuficha gharama halisi ya kusajili bidhaa. Ukweli ni kwamba, kusajili kifaa tiba cha daraja C, mathalani kaseti za kipimo cha malari (Malaria RDT), gharama yake si $1500, bali ni $9500, sawa na shilingi 21,850,000. Sasa jiulize mfanyabiashara mmoja ana bdhaa ngapi za daraja C anazotakiwa za kulipia ilia pate idhini ya kuingiza na kuuza hapa nchini. Je, huku si kukomoana? Lakini je kwa gharama hizi ni mfanya biashara gani anaweza kusajili kila bidhaa anayoingiza nchini?
RUSHWA
Siku zote urasimu gharama kubwa za huduma huzaa rushwa. Hebu jaalia mfano hizo query hapo juu na wewe ni mfanyabiashara (muingizaji na msambazaji wa vifaa tiba, dawa na vitendanishi) umepata mkataba na mteja umsambazie bidhaa hizo kwa ajili ya matumizi ya utafiti wake unaotarijiwa kuanza ndani ya mwezi mmoja baada ya mkataba kutolewa. Je, huyo mteja bado atakuwa anasubiri tu muda wote wa miezi 6 hadi 10?
Kiufupi hakuna mtu anaweza kufuata mlolongo huu wote. Hakuna mfanyabiashara ambaye yuko tayari kupoteza mauzo kwa vikwazo hivi vya TFDA. Wahenga wanasema penye udhia penyeza rupia. Maana yake ni kwamba wafanyabishara wanalazimika kuwapa rushwa watendaji wa mamlaka ya TFDA ili wapate vibali kwa wepesi. Bali watumishi wa mamlaka hiyo wanajifanya wako serious kusimamia sheria kumbe wanafanya hivyo ili wapewe rushwa.
Wafanyabiashara wamejifunza kwamba ili mpokea maombi ya vibali huko TFDA asitoe query katika maombi ya vibali inatakiwa wapatiwe pesa. Makampuni makubwa yanapata vibali na wanaingiza vifaa tiba vipya vya kila aina bila usajiliwa. Ukiangalia kwenye mtandao wa mamlaka hiyo utaona orodha ya vifaa tiba na vitendajishi vilivyosajiliwa ni vichache kuliko vinavyoingizwa kutoka nje ya nchi kila siku.
MWISHO
Tatizo kubwa si uwepo wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) wala sio uwingi wa majukumu ya mamlaka hiyo. Kuipunguzia majukumu ya kudhibiti ubora na biashara ya vyakula na vipodozi na kuibadili jina kutoka TFDA na kuiita TMDA hakutasaidia kuondoa changamoto kwa wafanyabiashara zinazotokana na utendaji wa mamlaka hii. Kuna haja kwa serikali kuifumua na kuisuka upya Mamlaka hii ili iendane na mabadiliko kutoka TFDA na kuwa TMDA. Vile vile viwango vya tozo na ada viangaliwe upya kwani ni kubwa sana. Vinginevyo mabadiliko hayo haya hataleta tija kwa serikali na wafanyabiashara bali ni kuendeleza kuwanufaisha watendaji wa mamlaka.

- Fees and charges paid under these Regulations shall be paid in Tanzanian shillings or US$ equal to the amount of Tanzania shillings or any convertible shilling equal the amount payable in Tanzania Shillings