Tatizo sio siasa, tatizo ni nani aliye nyuma ya hiyo siasa..(ni muono wangu tu)

THE GREAT CAMP

JF-Expert Member
Jun 29, 2012
765
194
Nimekuwa nikilaumu siasa ya Tanzania kuzorotesha maendeleo ya nchi yangu (TZ) lakini nikaamua kuangalia kwa jicho lingine. Kwa kweli hakuna nchi ambayo inatengeneza sera na miongozo mizuri kama Tanzania. Nchi nyingi za Afica zimekuwa zikitumia sera zetu na miongozo yetu na kuifanyia kazi na kupata maendeleo,(Naomba nisizitaje). Kwa wale wenzangu ambao mmeshapitia sera na miongozo mbalimbali ya nchi hii mtakubaliana na mimi. (KWA KWELI WATAALAMU WANAJITAHIDI SANA......pamoja na mapungufu waliyo nayo).

Sasa ni nani anayesimamia utekelezaji wa sera hizo? Wilayani ni Madiwani (full council), Hivi C.V zao ukizipitia unaweza kweli ukaamini kuwa wanaelewa nini kimeandikwa kwenye sera, mipango na miongozo mbalimbali ya nchi hii? Kali zaidi, C.V za mawaziri mbalimbali wa nchii hii haki ya MUNGU ukizisoma utalia, yaani elimu ni za kuungaunga tu. Hivi hapo unategemea waziri anaweza kuwa na upembuzi yakinifu kweli wa kusimamia maendeleo ya nchi hii?

Ushahidi fungua website ya Bunge la Tanzani usome C.V za hawa viongozi wetu utajua nachosema, Yaani nyingine ni uongo uongo tu unakuta waziri haijulikani shule ameanza lini lakini mwaka wa kumaliza umeandikwa, au Mwaka wa kuanza shule umeandikwa lakini mwaka wa kumaliza haujulikani......ghafla utakuta wameandika ana masters.

Ukiangalia C.V za wabunge....mama yangu utalia wengine hata darasa la 4 hawajafika. Ndiyo maana binafsi naamini tatizo siyo siasa, HAPA TATIZO NI WALE WALIO NYUMA YA HIYO SIASA...... (Empty headed). (Huo ni muono wangu tu...sijui wenzangu mna mawazo gani kuhusu hili.!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom