Tatizo sio raisi ni nani badi ni mfumo gani Tanzania tunautaka kwa kizazi kijacho. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tatizo sio raisi ni nani badi ni mfumo gani Tanzania tunautaka kwa kizazi kijacho.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kamundu, Jul 26, 2012.

 1. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #1
  Jul 26, 2012
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,112
  Likes Received: 461
  Trophy Points: 180
  Zitto ni mfano mmoja wa maraisi watarajiwa lakini Tanzania ni lazima tujiulize ni viongozi gani tunawataka na ni jinsi gani tunaweza kuendeleza Tanzania kwa kizazi kijacho.
  Tanzania ni nchi ambayo ni ngumu kwa sababu zifuatazo

  (1) Wananchi hawapendi kutawaliwa: Tofauti na Rwanda Watanzania ni waongeaji na wajasilimali vilevile Watanzania wana utamaduni mchanganyiko. Watanzania wengi wana mawazo tofauti hawataweza kuwa na raisi kama Kagame wa Rwanda maana hawapendi kuwambia ya raisi wafanye nini.
  (2)Upole: Tanzania vilevile haiwezi kuwa kama China kwani tuna upole ambao umefanya sheria zetu zile laini na zisizo na meno. China mfano wala rushwa wanafungwa maisha au hata kuamuliwa kifo wakati Tanzania hakuna hata mtu mmoja amefugwa kwa skendo ya Rada, Richmond au EPA!. Tunapenda serikali ifanye kila kitu wakati hatutaki na hatuna uwezo wa kufanya serikali iwe na nguvu kama ya China.

  Zitto ni raisi ambaye ataweka mfumo wa China ambao ni mchanganyiko wa upepari na ujamaa kwa serikali ku sign mikataba na kuwa na serikali kubwa sana. Zitto kama tulivyo ona anampenda Kaunda!. Mimi kwa mawazo yangu Tanzania haiwezi kuwa kama China kwasababu za hapo juu.

  Lowassa vilevile atataka nchi yetu iwe kama Russia ambako wafanya biashara wachache ndiyo wanafanya kila kitu muhimu kwa nchi. Tatito ni kwamba hii system italeta ubeberu na kama Russia itapunguza uwekezaji kwani serikali itakuwa na watu wanaofanya vitu kwa manufaa yao kwanza na biashara zote zitakuwa kwenye mikono michache. Hii system vilevile inakuwa na pupinga demokrasia ya habari. Sithani kwama hii itawezekana Tanzania.

  Tanzania inataka raisi ambaye ni wa kibepari lakini anaweza kuwaeleza Watanzania faidi za biashara, uhuru wa mawasiliano na magazeti, ubunifu wa binafsi kwenye teknologia, bank zenye kusaidia uchumi, serikali ndogo na ushindani wa wazi . Tanzania inataka viongozi kama wa Brazil na USA maana hizo ndizo nchi zinazofanana na Tanzania kwa mchanganyiko wa utamaduni na mahitaji ya nchi. Kufanikisha hili tunataka mahakama iwe na nguvu zaidi.

  Imefika wakati wa Watanzania kufanya maamuzi kwanza ni nchi gani tunaitaka kabla ya kukimbilia kuchagua maraisi ambao hawatafanya mabadiliko. Kikwete na ushabiki wote hajabadilisha chochote kwasababu hatuna uhakiki kwenye mfumo na wanasiasa wanapenda kufaidisha kila mtu.
   
Loading...