Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 5,053
- 4,499
Mara tu baada ya kushika mamlaka ya uraisi, Mh. JPM alianza kufunga makufuri kwenye hazina za taifa kama alivyokuwa ameahidi kwenye hizo kampeni zake. Alianza kuweka makufuri yake kule TRA na bandarini. Takwimu zilionyesha jinsi mapato yalivyokuwa yanatoroshwa, hususani makontena takribani 12,000 yalikuwa yakitoroshwa kwa mwezi kabla ya kufunga makufuri!
Sasa baadhi ya watu wamekuwa wakilalama eti mbona ameshindwa kuyapata hayo makontena? Sasa atayapataje mamilioni ya makontena yaliyotoroshwa kwa kipindi cha zaidi ya miaka 10 kwa kiwango cha kontena 12,000 kwa mwezi?
Jamaani tatizo si vilivyotoroshwa (kuibiwa) kabla ya makufuri kufungwa. Tatizo ni vitakavyotoroshwa baada ya kufunga kufuri. Kama vitaendelea kwa kiwango hicho hicho au kuongezeka, basi hapo tutakuwa na la kusema.
Uwezekano wa kufikia kiwango cha 0 (zero) bila shaka haupo kwani binadamu si mchezo - wapo watakaobuni mbinu zingine. Tusubiri takwimu zitaeleza, zoezi ni endelevu! Mapato yameongezeka hadi kufikia Shs. trioni 1.3 toka 0.9 trioni yaani ongezeko la 40% kwa mwezi.