Tatizo si Rais kama mtu, bali tatizo ni "vetting system" kuwa corrupted & compromised

Tatizo ni wanaofanya vetting, hiyo idara imevamiwa na watu wasio na nia njema na nchi hii.
Kila mwenye "nafasi" anataka kijana wake "awekwe" kwenye system... ndio maana hatushangai "mivujo ya siri-kali" ikitapakaa mitaani... maana inajadiliwa kama familia majumbani!!!
TUNA SAFARI NDEFU...
 
Kila mtu makini naamini hushangaa na kutatizwa sana pale ambapo mamlaka ya uteuzi ya viongozi iwe Rais ama Waziri ama yeyote ili mradi ni mamlaka ya uteuzi inapofanya uteuzi muda huu, kisha in less than 24hrs inatengua uteuzi huo huo...

Hili lilijitokeza mara kadhaa ktk utawala wa Rais Hayati John P. Magufuli. Sina kumbukumbu kwa awamu zingine za Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete...

Na sasa ktk awamu hii ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassani ambayo haina hata wiki 3 tangu ianze kutawala, taratibu kwa mwendo wa spidi ya mwanga, imeanza kurithi udhaifu huu mbaya usiopaswa kuwepo ktk serikali ambayo iko well organized...

Hii siyo ishara njema. Hii ni ishara kuwa kuna tatizo katika mifumo ya ufuatiliaji na uchakataji wa taarifa katika eneo hili. Hii ni ishara mbaya kuwa, kuna tatizo la kukosa utulivu na umakini na pengine kutoaminiana miongoni mwa mifumo ya utendaji serikalini...

Aidha tunajua kuwa katika nchi na serikali zote duniani, kwa nafasi zote za uongozi wa kuteuliwa, kabla ya uteuzi wa mtu na ukiachilia mbali sifa za jumla na za wazi alizonazo mtu huyo kama elimu, umri nk, basi huwa zipo sifa zingine za ziada (sifa mficho) ambazo mtu huyo anayelengwa kuteuliwa huwa lazima a - fit ktk hizo ndipo jina lake linakwenda kwenye mamlaka ya uteuzi wake...

Hizi zinaitwa "sifa mficho" kwa sababu si kila mtu anaweza kuziona isipokuwa ni watu maalumu wenye sifa na utaalamu wa kuzithibitisha na kutoa recommendation ya "go ahead or don't" kwa mamlaka ya uteuzi...

Mfumo huu wa kufuatulia na kuchakata taarifa za mtu au watu wanaopaswa kuteuliwa kushika nafasi hizi za uongozi ktk taasisi au mashirika nyeti ya umma huitwa kwa lugha rahisi kama "Vetting System"...

Na kwa kadiri ya ufahamu wangu, kazi hii hufanywa na kitengo maalumu ktk Idara ya Usalama wa Taifa ambayo ndiyo roho na moyo wa nchi yoyote. Hapa kwetu Tanzania inaitwa TISS....

Ni bahati mbaya sana kuwa, kuna kila ishara kuwa TISS wako corrupted and compromised katika jukumu lao hili muhimu sana...

Hawa wakishindwa kutekeleza wajibu wao huu muhimu kiweledi (professionally) tujue kabisa kuwa, kama taifa ipo siku na inakaribia kufika tutavurugikiwa na na tutaanguka na tukapata shida sana kuinuka tena...

TISS imeharibiwa sana na viongozi wa kisiasa ambao actually tunaweza kuwaita si wazalendo kwa nchi na taifa hili hata chembe japo wenyewe kwa midomo yao huuimba kujipaka rangi ya uzalendo kinafiki tu....

Viongozi hawa huwa wameathiriwa na njia ovu zisizo za haki walizotumia kujipatia madaraka na uongozi walio nao ambazo ni wizi wa kura kupitia chaguzi walizoandaa wao wenyewe zisizo za kidemokrasia....

Kwa sababu ya style waliyotumia kupata vyeo au madaraka, basi muda wote hujiona hawako salama (insecure) ambayo ni tabia ya mwizi au mtenda maovu yeyote na hivyo ili kujihakikishia usalama wao hutumia vyombo kama TISS kujihami si kwa manufaa ya watu na nchi bali kwa manufaa yao binafsi ya kulinda nafasi zao za kisiasa wasije wakanyang'anywa...

TISS ya sasa inafanya kazi zake ktk misingi ya siasa za U - CCM sambamba na RUSHWA wakipuuza au kuweka kando ETHICS & PROFESSIONALISM ya mambo ya usalama....

Hivyo hatuwezi kushangaa kwa Rais wa nchi kuletewa majina na kuhakikishiwa na "KITENGO" kuwa "vetting" imefanyika kikamilifu na Rais kwa kuwaamini, anatangaza uteuzi wa majina hayo lakini baada ya masaa kadhaa (from No. 3 eye) zinapatikana taarifa zingine contrary kumhusu mtu huyo huyo tena na kisha mamlaka hiyo hiyo ya uteuzi (Rais) inatengua uteuzi wake...

Hii ni aibu sana kwa serikali makini. Na ofcoz, this is purely incompetence ya idara hii muhimu kwa nchi...

Mimi siwezi kushangaa kusikia kuwa idara hii muhimu (TISS) kwa nchi na taifa letu imeshavamiwa na mdudu rushwa...

Kwamba, maafisa wa TISS huomba rushwa kwa mtu mlengwa wa kuteuliwa na hivyo badala ya kum - recommend kwa haki kulingana sifa zake halisi, badala yake hufunika madhaifu yake na mwisho wa siku as we go, udhaifu wake unathibitika kuwa, kumbe ni mtu asiye sifa ya kuteuliwa ktk nafasi hiyo..!!

Wanachoweza kufanya baadhi ya maafisa TISS waliopewa kazi ya kufuatilia taarifa za mtu X, ni kumtaarifu tu kuwa bwana eeh, kuna deal la kuukwaa u DG wa TPDC (kwa mfano)...

Watamwambia mtu huyo, kuwa, sisi ndiyo tumpewa kazi ya kuku - vet. Tukisaini sisi umepita. Changamka, leta 50M Tshs (mfano) hapa tupeleke jina lako...

Duuh...!! Mambo kama yako hivi, basi hii ni hatari sana. Mungu Yehova tusaidie maana nchi itauzwa hii...!

Na kwa dalili hizi za teua asubuhi kisha jioni tengua, ni ishara kuwa haya mambo yapo na yanafanyika....

USHAURI KWA RAIS MPYA, MS. SAMIA S. HASSANI

Mama kama unataka kuwa kiongozi wa mafanikio, angazia na Fanya marekebisho ya kimfumo na kisheria ktk idara hii muhimu iliyo moyo wa nchi. Else, hata wewe unaweza kuuzwa tu ukiwa ofisini kwako...
huu mwandiko ni wa mtu ninayemjua sana hapa JF (mzee wa multiple IDs).
ila haina shida, tujikite kwenye mada.
 
TISS ni taasisi kubwa tafadhali msitupe maji machafu kwenye baseni pamoja na mtoto aliyemo kwenye beseni. Ufanisi wa kiutendaji wa kila taasisi unategemea na uwezo wa mtu anayeiongoza. Akiongoza vizuri taasisi inakuwa nzuri, akiongoza vibaya taasisi nayo inakwenda vibaya lakini haina maana taasisi yote ni mbovu. Pia TISS ni taasisi ya ushauri na ni pia ya utendaji chini ya maelekezo ya Serikali Kuu. Ukipeleka ushauri inategemea unayempelekea ushauri atakavyoamua kuutumia ushauri wako.
Aidha, Kwa baada ya msiba huu wa kitaifa ambao haujawahi tokea, bado nchi yetu Tanzania iko salama na uongozi mbadala umewekwa bila matatizo; huu ni ushahidi tosha kuwa TISS na vyombo vingine vimefanya kazi ya kuiwezesha nchi yetu ibaki salama. Tushukuru.
Viongozi hawa wapya wa sasa kama binadamu wote tulivyo,wangependa uongozi wa kupendwa na wananchi. Kwa hiyo naamini kuwa watapenda kusahihisha makosa ya awali. Mimi siyo msemaji wala mwana TISS lakini ni mzoefu wa utawala nawaomba tuelewane hivyo.



wananchi kwa kufanya wajibu wao. Tuwape muda na haya matatizo madogo madogo pamoja na makosa vianzo vyake vitajulikana ama na TISS yenyewe

, Serikali Kuuu au Chama kilichopo kwenye madaraka. Tusimwage maji machafu kwenye beseni na mtoto aliyemo!
Si kwamba hatushukuru au si kwamba hatuoni BALI MATUKIO MBALIMBALI YALIYOTUKIA NA YANAYOTUKIA NDIO YANAYOTUSEMEZA "KULIKONI?"Je matatizo haya na yale na ile "mivujo" inakuwaje? YAWEZA KUWA "SHAURI HIZI" zinakera au kuwakera baadhi ya watu ila ni KWA USALAMA WA NCHI NA SISI.
WAJITATHMINI... magugu yaondolewe...
 
TUTULIE JAMANI NI MAPEMA MNO .TISS WAPO VIZURI SANA NA WANAFANYA KAZI NZURI SANA . VETTING KUNA WAKATI INAWEZA KUWA BAHATI MBAYA ZA KIBINADAMU ,SISI SI MALAIKA.MUNGU TUSAIDIE TUZIDI KUIPENDA NCHI YETU
Mnampoteza mama yetu. Msaidieni na rudisheni heshima ya hiyo taasisi muhimu kwa nchi yetu.
 
H
Obviously, hii siyo TISS tena bali inaonekana kama idara ndani ya Chama Cha Mapinduzi - CCM maana haijawahi kutokea Nyani (CCM) huyu akaweza kuona kundule (makosa) yake..

Hebu fikiri unashindwaje kuona udhaifu wa viongozi kama Ole Sabaya (DC - Hai), Chalamila (RC Mbeya), Ally Hapi (RC Iringa), Jerry Muro (DC - Arumeru), aliyekuwa RC - DSM, Paul Makonda...

Yaani kwa mfano TISS walishindwa nini kujua kwa urahisi tu kuwa, mtu kama huyu Paul Makonda hastahili nafasi yoyote ya uongozi na utumishi wa umma kwa sababu ya ufisadi ktk elimu yake??

Mtu kama huyu akipewa ofisi ya umma lazima tu atatumia madaraka yake vibaya ikiwemo kufisidi mali ya umma...!!
Hapa sikubaliani na wewe, kuwa na shida kwenye vyeti vyako doesn't mean huwezi kuwa muadilifu. Mengine yanafanywa tu na wazazi wako, mfano kwa kesi ya makonda inawezekana ni wazazi walifanya hivyo. Ikumbukwe makonda alikuwa mdogo kufanya maamuzi yake mwenyewe.
 
Walingozi hakuwahi DG kwa vile baadaye aligombea ubunge, lakini alikuwa na afisa mwandamizi sana aliyekuwa anashughulikia operations zote za TISS. Wengine katika grupu hilo walikuwa ni pamoja na Mwang'onda (baadaye alikuwa DG), Agustino Mahiga (baadaye alikuwa balozi) na Othman Rashid (naye baadaye alikuwa DG).
DOI
 
USHAURI KWA RAIS MPYA, MS. SAMIA S. HASSANI

Mama kama unataka kuwa kiongozi wa mafanikio, angazia na Fanya marekebisho ya kimfumo na kisheria ktk idara hii muhimu iliyo moyo wa nchi.
Mkuu The Palm Tree, kwanza naunga mkono hoja.
Pili sio tuu Mama anaweza kupelekewa makorokocho akayateua, bali pia kuna uwezekano watu wazuri, waadilifu wanakwepwa kwenye uteuzi, hivyo taifa kukosa viongozi bora, wazuri, waadilifu, kwa ajili ya kupitisha hayo makorokocho yao!.
Hili nimelizungumza hapa
P
 
Mkuu The Palm Tree, kwanza naunga mkono hoja.
Pili sio tuu Mama anaweza kupelekewa makorokocho akayateua, bali pia kuna uwezekano watu wazuri, waadilifu wanakwepwa kwenye uteuzi, hivyo taifa kukosa viongozi bora, wazuri, waadilifu, kwa ajili ya kupitisha hayo makorokocho yao!.
Hili nimelizungumza hapa
P
Ina maana huna imani na vetting system iliyopo ?...
 
Ina maana huna imani na vetting qsystem iliyopo ?...
No sio sina imani na vetting process, bali natatizwa na hawa watu kwa sababu ni watu hao hao wa vetting ndio wanaomchomekea mama yale makorokocho, mama anateua leo, kesho anatengua!.
P
 
Aisee...kwani ni lazima yeye apitishe kila anacholetewa ?
No!, sio lazima apitishe kila anacholetewa, na hapa ndipo penye udhaifu wa sisi mhimili wa nne!. It's a fact IQ ya mama na yule Blaza wangu, hazifanani, wale jamaa zetu wameligundua hilo na ku take advantage ya kumchomekea makorokocho!, enzi za Blaza walikuwa hawafanyi maana yule jamaa..., sisi mhimili wa nne ni kazi yetu kumsaidia mama kwa kuuliza hao wachomeka makorokocho ni kina nani na wamefanywa nini?. Wanavyomfanyia Maza sio fair!.
P
 
No!, sio lazima apitishe kila anacholetewa, na hapa ndipo penye udhaifu wa sisi mhimili wa nne!. It's a fact IQ ya mama na yule Blaza wangu, hazifanani, wale jamaa zetu wameligundua hilo na ku take advantage ya kumchomekea makorokocho!, enzi za Blaza walikuwa hawafanyi maana yule jamaa..., sisi mhimili wa nne ni kazi yetu kumsaidia mama kwa kuuliza hao wachomeka makorokocho ni kina nani na wamefanywa nini?. Wanavyomfanyia Maza sio fair!.
P
Brother Pascal , wewe ni mtu anaye aminika hapa jukwaani, umejijengea heshima kubwa Hilo halina ubishi.

Leo nashindwa kuelewa huu ufafanuzi wako, eti Blaza wako , hakuchanganyiwa makorokocho, umesahau mteule alie shindwa kuapa? Je teuzi uliendelea au aliteuliwa mwingine?
 
25 Reactions
Reply
Back
Top Bottom