Tatizo si Rais kama mtu, bali tatizo ni "vetting system" kuwa corrupted & compromised

Mkuu joka kuu hapo hakuna la kushangaza hilo jina limefikaje kwenye meza ya rais, na hata mleta uzi kagusia kwenye uzi wake mama. Ni ukweli ulio wazi kuwa serikali hii iko madarakani kwa wizi wa kura, na hilo kila mtu analijua. Na hao kitengo walishiriki moja kwa moja kwenye wizi ule wa kura. Hivi unategemea nini kwa viongozi walioko madarakani kwa wizi wa kura, huku idara nyeti ikiwa sehemu ya uchafu huo? Kwa vyovyote vile hicho kitengo cha vetting ndio kilichoshiriki kwenye wizi ule, na sasa wanachofanya ni muendelezo wa kile kilichoiweka serikali hiyo madarakani. Tusitegemee usalama wa taifa wenye waadilifu, wakati viongozi wa nchi wanapatikana kwa kushirikiana na kitengo hicho cha usalama wa taifa kunajisi mifumo halali ya kupata viongozi wa nchi.
Isije ikawa tukafika mahala badala ya kuwa na usalama wa taifa tukawa na usalama wa wahalifu wa taifa... Mungu atuepushie idara yetu nyeti kufika huko
 
Isije ikawa tukafika mahala badala ya kuwa na usalama wa taifa tukawa na usalama wa wahalifu wa taifa... Mungu atuepushie idara yetu nyeti kufika huko

Mkuu kwa sasa tuko tayari kwenye usalama wa wahalifu wa taifa. Kama rais anashirikiana na usalama wa taifa kunajisi uchaguzi, unataka nini zaidi ya hapo?
 
Kila mtu makini naamini hushangaa na kutatizwa sana pale ambapo mamlaka ya uteuzi ya viongozi iwe Rais ama Waziri ama yeyote ili mradi ni mamlaka ya uteuzi inapofanya uteuzi muda huu, kisha in less than 24hrs inatengua uteuzi huo huo...

Hili lilijitokeza mara kadhaa ktk utawala wa Rais Hayati John P. Magufuli. Sina kumbukumbu kwa awamu zingine za Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete...

Na sasa ktk awamu hii ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassani ambayo haina hata wiki 3 tangu ianze kutawala, taratibu kwa mwendo wa kinyonga inaanza kurithi udhaifu huu mbaya usiopaswa kuwepo ktk serikali ambayo iko well organized...

Hii siyo ishara njema. Hii ni ishara kuwa kuna tatizo katika mifumo ya ufuatiliaji na uchakataji wa taarifa katika eneo hili. Hii ni ishara mbaya kuwa, kuna tatizo la kukosa utulivu na umakini na pengine kutoaminiana miongoni mwa mifumo ya utendaji serikalini...

Aidha tunajua kuwa katika nchi na serikali zote duniani, kwa nafasi zote za uongozi wa kuteuliwa, kabla ya uteuzi wa mtu na ukiachilia mbali sifa za jumla na za wazi alizonazo mtu huyo kama elimu, umri nk, basi huwa zipo sifa zingine za ziada (sifa mficho) ambazo mtu huyo anayelengwa kuteuliwa huwa lazima a - fit ktk hizo ndipo jina lake linakwenda kwenye mamlaka ya uteuzi wake...

Hizi zinaitwa "sifa mficho" kwa sababu si kila mtu anaweza kuziona isipokuwa ni watu maalumu wenye sifa na utaalamu wa kuzithibitisha na kutoa recommendation ya "go ahead or don't" kwa mamlaka ya uteuzi...

Mfumo huu wa kufuatulia na kuchakata taarifa za mtu au watu wanaopaswa kuteuliwa kushika nafasi hizi za uongozi ktk taasisi au mashirika nyeti ya umma huitwa kwa lugha rahisi kama "Vetting System"...

Na kwa kadiri ya ufahamu wangu, kazi hii hufanywa na kitengo maalumu ktk Idara ya Usalama wa Taifa ambayo ndiyo roho na moyo wa nchi yoyote. Hapa kwetu Tanzania inaitwa TISS....

Ni bahati mbaya sana kuwa, kuna kila ishara kuwa TISS wako corrupted and compromised...

Hawa wakishindwa kutekeleza wajibu wao huu muhimu kiweledi (professionally) tujue kabisa kuwa, kama taifa ipo siku tunakuja kuvurugikiwa na kuanguka na tukapata shida sana kuinuka tena...

TISS imeharibiwa sana na viongozi wa kisiasa ambao actually tunaweza kuwaita si wazalendo kwa nchi na taifa hili hata chembe japo wenyewe kwa midomo yao huuimba kujiita wazalendo kinafiki tu....

Viongozi hawa huwa wameathiriwa na njia ovu zisizo za haki walizotumia kujipatia madaraka na uongozi walio nao ambazo ni wizi wa kura kupitia chaguzi walizoandaa wao wenyewe zisizo za kidemokrasia....

Kwa sababu ya style waliyotumia kupata vyeo au madaraka, basi muda wote hujiona hawako salama (insecure) ambayo ni tabia ya mwizi au mtenda maovu yeyote na hivyo ili kujihakikishia usalama wao hutumia vyombo kama TISS si kwa manufaa ya watu na nchi bali kwa manufaa yao ya kulinda nafasi zao za kisiasa wasije wakanyang'anywa...

TISS ya sasa inafanya kazi zake ktk misingi ya siasa za U - CCM sambamba na RUSHWA wakipuuza au kuweka kando ETHICS & PROFESSIONALISM ya mambo ya usalama....

Hivyo hatuwezi kushangaa kwa Rais wa nchi kuletewa majina na kuhakikishiwa na "KITENGO" kuwa "vetting" imefanyika kikamilifu na Rais kwa kuwaamini, anatangaza uteuzi wa majina hayo lakini baada ya masaa kadhaa (from No. 3 eye) zinapatikana taarifa zingine contrary kumhusu mtu huyo huyo tena na kisha mamlaka hiyo hiyo ya uteuzi (Rais) anatengua uteuzi wake...

Hii ni aibu sana kwa serikali makini. Na ofcoz, this is purely incompetence ya idara hii muhimu kwa nchi...

Mimi siwezi kushangaa kuwa kuna rushwa ndani ya TISS. Kwamba maafisa wa TISS huomba rushwa kwa mtu mlengwa wa kuteuliwa na hivyo badala kum - recommend kwa haki, wanafunika madhaifu yake na mwisho siku as we go, udhaifu wake unathibitika kuwa, kumbe alikuwa hana sifa kuteuliwa ktk nafasi hiyo..!!

Wanachoweza kufanya baadhi ya maafisa TISS waliopewa kazi ya kufuatilia taarifa za mtu X, ni kumtaarifu tu kuwa bwana eeh, kuna deal la kuukwaa u DG wa TPDC (kwa mfano)...

Watamwambia mtu huyo, kuwa, sisi ndiyo tumpewa kazi ya kuku - vet. Tukisaini sisi umepita. Changamka, leta 50M Tshs (mfano) hapa tupeleke jina lako...

Duuh...!! Mambo kama yako hivi, basi hii ni hatari sana. Mungu Yehova tusaidie maana nchi itauzwa hii...!

Na kwa dalili hizi za teua asubuhi kisha jioni tengua, ni ishara kuwa haya mambo yapo na yanafanyika....

USHAURI KWA RAIS MPYA, MS. SAMIA S. HASSANI

Mama kama unataka kuwa kiongozi wa mafanikio, angazia na Fanya marekebisho ya kimfumo na kisheria ktk idara hii muhimu iliyo moyo wa nchi. Else, hata wewe unaweza kuuzwa tu ukiwa ofisini kwako...
Tangu Walingozi aondoke, TISS haijawahi kuwa TISS tena! Miaka ya80 na mwanozi mwa miaka ya 90 nilikuwa karibu na maafisa wengi wa TISS na wale wa TAKURU ya wakati huo. Utendaji wa maafisa wengi waliopo sasa hivi ni light weight ukilinganisha na wale wa zamani. Nadhani inachangiwa na mambo kadhaa moja wapo likiwa hili la utandawazi; siku hizi hawajifichi tena, na maisha yao yanajulika wazi wazi. zamani zile walikuwa i maafisa spesho sana serikalini, na walikuwa hawajulikani hovyo hovyo.
 
Upatikanaji wa Watumishi wa Umma hasa Makatibu wakuu na MaDED ndio ubadilike.
Hizi ni nafasi nyingi sana kupewa mtu mmoja afanye uteuzi.

Uteuzi wa MaDC na wakurugenzi utahitaji uangalifu sana kwani ni wengi hivyo chances za makosa kujirudia ni kuwa!! Let the President take her times so that she is thorough.
 
Ukingalia kwa picha kubwa shida katiba iliyopo ambayo hutukuza watu badala ya taasis, taasis karibia zote zinaingiliwa kirahisi na wamasiasa kutokana mamlaka waliyopewa kuwa juu ya mifumo ya taasis
 
Lini WALINGOZI alikuwa DG wa TISS? Nadhani alikuwa mkurugenzi wa Idara!
Walingozi hakuwahi DG kwa vile baadaye aligombea ubunge, lakini alikuwa na afisa mwandamizi sana aliyekuwa anashughulikia operations zote za TISS. Wengine katika grupu hilo walikuwa ni pamoja na Mwang'onda (baadaye alikuwa DG), Agustino Mahiga (baadaye alikuwa balozi) na Othman Rashid (naye baadaye alikuwa DG).
 
Mkuu joka kuu hapo hakuna la kushangaza hilo jina limefikaje kwenye meza ya rais, na hata mleta uzi kagusia kwenye uzi wake mama. Ni ukweli ulio wazi kuwa serikali hii iko madarakani kwa wizi wa kura, na hilo kila mtu analijua. Na hao kitengo walishiriki moja kwa moja kwenye wizi ule wa kura. Hivi unategemea nini kwa viongozi walioko madarakani kwa wizi wa kura, huku idara nyeti ikiwa sehemu ya uchafu huo? Kwa vyovyote vile hicho kitengo cha vetting ndio kilichoshiriki kwenye wizi ule, na sasa wanachofanya ni muendelezo wa kile kilichoiweka serikali hiyo madarakani. Tusitegemee usalama wa taifa wenye waadilifu, wakati viongozi wa nchi wanapatikana kwa kushirikiana na kitengo hicho cha usalama wa taifa kunajisi mifumo halali ya kupata viongozi wa nchi.

Absolutely, hili la kupata uongozi na madaraka kwa njia za udanganyifu, rushwa na wizi wa kura ndiyo sumu ya kuliua taifa hili zuri la Tanzania...

Mtu aliyejipatia uongozi kwa njia ovu isiyo ya haki, hawezi kuwa kiongozi mzuri, atakuwa mbinafsi tu, hawezi kujiamini, atakuwa mwoga hata kwa kivuli chake mwenyewe, atajiona insecure kwa muda wote na atatumia njia zote za kiovu kujilinda ikiwemo ku - abuse madaraka yake kwa nia ileile ya kujilinda.

Hili ndilo tatizo lililokuwa linamsumbua Mwendazake a.k.a Jiwe a.k.a Meko a.k.a Bulldozer kiasi cha kuanza kujiita yeye mwenyewe kuwa kuwa kichaa...
 
TUTULIE JAMANI NI MAPEMA MNO .TISS WAPO VIZURI SANA NA WANAFANYA KAZI NZURI SANA . VETTING KUNA WAKATI INAWEZA KUWA BAHATI MBAYA ZA KIBINADAMU ,SISI SI MALAIKA.MUNGU TUSAIDIE TUZIDI KUIPENDA NCHI YETU
No, usiwatetee hawa...

Hakuna excuse ya namna hii...

Human errors kwa mtu anayefanya kazi vizuri inaonekana kwa urahisi sana na inasameheka...

Hawa TISS hawafanyi kazi yao. Wameshanyweshwa maji ya itikadi za siasa za CCM na wao wameyanywa na sasa wanakubali kupelekwa pelekwa tu wakisahau ethics na professionalism inayoongoza utendaji kazi wao..

Ninachoweza kukubaliana na wewe kuwa ni tatizo kwao, ni labda tuseme, mfumo mbaya wa kimuundo wa taasisi unaochagizwa na ubovu wa katiba na sheria zetu...
 
..tatizo ni wanaofanya vetting.

..hiyo idara imevamiwa na watu wasio na nia njema na nchi hii.

Obviously, hii siyo TISS tena bali inaonekana kama idara ndani ya Chama Cha Mapinduzi - CCM maana haijawahi kutokea Nyani (CCM) huyu akaweza kuona kundule (makosa) yake..

Hebu fikiri unashindwaje kuona udhaifu wa viongozi kama Ole Sabaya (DC - Hai), Chalamila (RC Mbeya), Ally Hapi (RC Iringa), Jerry Muro (DC - Arumeru), aliyekuwa RC - DSM, Paul Makonda...

Yaani kwa mfano TISS walishindwa nini kujua kwa urahisi tu kuwa, mtu kama huyu Paul Makonda hastahili nafasi yoyote ya uongozi na utumishi wa umma kwa sababu ya ufisadi ktk elimu yake??

Mtu kama huyu akipewa ofisi ya umma lazima tu atatumia madaraka yake vibaya ikiwemo kufisidi mali ya umma...!!
 
NISAIDIENI HIVI NI TAIFA GANI LIMEWAHI NYANYULIWA VYEMA AU LILIKOMBOLEWA NA MWANAMKE????
LABDA KUTETEA HAKI ZA WAMAMA,WATOTO YATIMA,WAKIMBIZI NK.
LAKINI KUJENGA MAMIUNDOMBINU MARELI/MELI/BANDARI/AIRPORT, KUINUA ELIMU/AFYA/MAJI/UMEME, KUPAMBANA NA MAFISADI/MABEBERU NK. TUSAHAU KIDOGO!!!
HAPA NIAMINIVYO NI MIAKA MINNE NANUSU YA MAKITAIMU...
HIZI FACT KUMI KAVU TUSIJIKAUSHE!!!
-KWANZA MMAMA (hawapaswi kazingumu),
-PILI MZANZ (kwao yote hewalaaa), -TATU MUISLAM (desturi wamama hutakiwa kukaandani)
-NNE MNENE (pilikapilika atachoka nchi kubwa),
-TANO JICHO LAINI (hashtui ukiiba), SITA ELIMU KAWAIDA (hajisomeagi sana),
-SABA HAJUI KILIMO/UFUGAJI (kazi ya 75% ya watz),
-NANE HAJUI VEMA WATU (hajichanganyi namasela kumshika mkono tu uzu),
-TISA HAJAKULIA BARA (hajapigwa na shidazetu na hazijui vema)
** KUMI AMIRI JESHI MKUU HAFAI KUWA MWANAMKE (toka enzi kiongoz wavita huwa ni mwanaume).
Swali ni Je? Sisiembu bado nichama dumeee???
*NB. sijaiongelea Tanzania wasojulikana hawakawii kuja nibana pum6u
 
Isije ikawa tukafika mahala badala ya kuwa na usalama wa taifa tukawa na usalama wa wahalifu wa taifa... Mungu atuepushie idara yetu nyeti kufika huko
TISS ni taasisi kubwa tafadhali msitupe maji machafu kwenye baseni pamoja na mtoto aliyemo kwenye beseni. Ufanisi wa kiutendaji wa kila taasisi unategemea na uwezo wa mtu anayeiongoza. Akiongoza vizuri taasisi inakuwa nzuri, akiongoza vibaya taasisi nayo inakwenda vibaya lakini haina maana taasisi yote ni mbovu. Pia TISS ni taasisi ya ushauri na ni pia ya utendaji chini ya maelekezo ya Serikali Kuu. Ukipeleka ushauri inategemea unayempelekea ushauri atakavyoamua kuutumia ushauri wako.
Aidha, Kwa baada ya msiba huu wa kitaifa ambao haujawahi tokea, bado nchi yetu Tanzania iko salama na uongozi mbadala umewekwa bila matatizo; huu ni ushahidi tosha kuwa TISS na vyombo vingine vimefanya kazi ya kuiwezesha nchi yetu ibaki salama. Tushukuru.
Viongozi hawa wapya wa sasa kama binadamu wote tulivyo,wangependa uongozi wa kupendwa na wananchi. Kwa hiyo naamini kuwa watapenda kusahihisha makosa ya awali. Mimi siyo msemaji wala mwana TISS lakini ni mzoefu wa utawala nawaomba tuelewane hivyo.



wananchi kwa kufanya wajibu wao. Tuwape muda na haya matatizo madogo madogo pamoja na makosa vianzo vyake vitajulikana ama na TISS yenyewe

, Serikali Kuuu au Chama kilichopo kwenye madaraka. Tusimwage maji machafu kwenye beseni na mtoto aliyemo!
 
Mwigulu Ana shida gani ? Umefanya nae kazi closely au unamuona kwenye mitandao ?
Mwigulu ni mganga njaa wala sio Mwanasiasa.

Mwigulu anamkono wake kwenye hii covid kuachwa isambae na kufichwa takwimu za vifo na maambukizi

Mwigulu hafai
 
Mwigulu ni mganga njaa wala sio Mwanasiasa.

Mwigulu anamkono wake kwenye hii covid kuachwa isambae na kufichwa takwimu za vifo na maambukizi

Mwigulu hafai

Ulitaka Mwigulu awavalishe mask wewe na Jiwe RIP , mwigulu lini amekua waziri wa Afya Mpaka afiche takwimu? Ukimchukia mtu uwe na sababu la sivyo huo ni wivu wa kike tena wa mama kijacho

Mwigulu alipata tabu na Maghufuli , Mwigulu alikua anapiga Makofi kabisa na JPM sijui ulitaka amshawishi nini Raisi hasieshaulika na mtu yoyote

TISS ilitumia akili ya ziada kumchomoa Makonda ili Raisi hasiendelee kufedheeshwa na kuchafulia kwa kumdanganya agombee ubunge Raisi atampa uwaziri Mkuu , Makonda akaingia mzima mzima
 
Tangu Walingozi aondoke, TISS haijawahi kuwa TISS tena! Miaka ya80 na mwanozi mwa miaka ya 90 nilikuwa karibu na maafisa wengi wa TISS na wale wa TAKURU ya wakati huo. Utendaji wa maafisa wengi waliopo sasa hivi ni light weight ukilinganisha na wale wa zamani. Nadhani inachangiwa na mambo kadhaa moja wapo likiwa hili la utandawazi; siku hizi hawajifichi tena, na maisha yao yanajulika wazi wazi. zamani zile walikuwa i maafisa spesho sana serikalini, na walikuwa hawajulikani hovyo hovyo.
Majukumu yao wanaingiliwa na wanasiasa mno ingawa bado ni wazuri.
 
Back
Top Bottom