Tatizo si posho, Tatizo ni wakwepa kodi wakubwa na taifa kutonufaika na rasilimali zetu (Zitto) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tatizo si posho, Tatizo ni wakwepa kodi wakubwa na taifa kutonufaika na rasilimali zetu (Zitto)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Godwine, Dec 6, 2011.

 1. G

  Godwine JF-Expert Member

  #1
  Dec 6, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Nimeona maneno ya zitto kabwe ya kupingana na posho, mimi natambua anamtazamo na mawazo yanayoweza kutofautiana na mimi au na watu wengine kwani huo ndio uhuru wa kufikiri.

  Tanzania si taifa la kupambana vita kwenye posho za wafanyakazi wake, bali ni taifa linalotakiwa kufanya mapambano katika kudhibiti wakwepa kodi kwenye sekta ya madini na wengine kama wahindi wanaotumia maduka ya jeshi kukwepakodi kubwa sana.

  kuwa mfanyakazi wa tanzania si kwamba ulipwe mafao dhaifu, na wafanyakazi wengine kama walimu wakipunjwa mishahara basi ni lazima watu wote wapunjwe mishahara na posho. nadhani ningemuelewa zitto kama angepigania kwanza wafanyakazi wengine kama walimu wapate posho na mishahara mikubwa na kuimiza ukusanyaji wa kodi na taifa kunufaika na rasilimali zetu.
   
 2. k

  king11 JF-Expert Member

  #2
  Dec 6, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ​yah nakubali kuwa taifa lazima liende mbali na kutazama mifumo na si matokeo
   
 3. G

  Godwine JF-Expert Member

  #3
  Dec 7, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  mapambano ya posho sasa ndio mwanzo na tunatarajia taifa kutikisika kwa mambo mengi
   
 4. M

  Mkandara Verified User

  #4
  Dec 7, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Tatizo ni Posho yenyewe.. Posho haizalishi na kwa nchi maskini kukata matumizi ndilo jambo la kwanza kabisa maana Posho ni sawa na anasa tu haina uzalishaji. Walipwe watu mishahara ambayo inajumuisha kazi zote za mwajiriwa ikiwa ni pamoja na vikao maana nijuavyo mimi mshahara wa Mfanyakazi unalipwa kwa mwezi (8hrs/fivedays a week/monthly) na muda wote vinapofanyika vikao hivi huyo mfanyakazi huwa hafiki kazini lakini hulipwa mshahara mzima hata kwa siku ambazo hakuwepo kazini akiwa ktk mikutano inayolipwa posho.. Haya ni malipo mara mbili..
   
 5. k

  king11 JF-Expert Member

  #5
  Dec 9, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  huwezi kujumuisha posho zote kwenye mishahara kwa mfano je unaweza kuzijumuisha posho za safari na zile za nje ya kituo cha kazi kwenye mshahara?
   
 6. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #6
  Dec 9, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  si lazima pesa yote ya kodi ilipe mishara la nchi ni masikini sana tunapaswa tujinyime ili tupate pesa kwa aajili maendeleo mtumishi alipwe mshara wa kumtosha na fedha ya kujikimu kama kuna ulazima na siyo posho ya VIKAO huu ni wizi wa mchana

  Hata kama utakusanya kodi kiasi gani kama zitaishia kwenye posho naona haina maana - tunahitaji maendeleo mkuu
   
 7. kaburungu

  kaburungu JF-Expert Member

  #7
  Dec 9, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,608
  Likes Received: 2,461
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mh.Zitto nadhan ameanza kwa kupinga hizo posho ikiwa ni hatua ya mwanzo kuelekea kufungua njia ya kuwabana wakwepa kodi wakubwa. Kumbuka hili la posho bado linasuasua na bado linahitaji mwitikio wa pamoja kutoka kwa wanasiasa, wanaharakati+wananchi kwa pamoja..
  Tusubiri tuone hatma ya hili la posho na mafanikio ya hili ndo mwanzo wa kuibua uozo mwingine.
  Nawasilisha!
   
 8. d

  dada jane JF-Expert Member

  #8
  Dec 9, 2011
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  sawa kabisa G tz kuna tatizo zaidi ya posho ya wabunge. Mimi ni ticha wa primary huwa kinaniuma sana tunavyotaniwa na ze komed eti kichwa kama mwl wa pr. Hii yote c kwa7bu ya kipato cha chini
   
 9. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #9
  Dec 9, 2011
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Na wananchi wajiulize kama uwakilishi wa aina hii una manufaa kwao, na kama hauna kwanini tuendelee kuwa nao. We can do better without these thieves.
   
 10. Sungurampole

  Sungurampole JF-Expert Member

  #10
  Dec 9, 2011
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 987
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  tatizo in posho... hili halina mjadala.

  Kukwepa kodi kwenye madini na kwingineko nalo ni tatizo.. tena kubwa sana

  Kwa bahati mbaya unataka tusahau kuwa posho ni tatizo na tuhamie la madini na makampuni hatukubali -- POSHO ni tatizo kwani hata kodi za migodi zikilipwa hatutakubali wazifaidi wachache kupitia posho

  POSHO NI TATIZO KUBWA SANA VIPOFU TU KAMA VIONGOZI WETU NDIYO HAWALIONI
   
 11. M

  Mkandara Verified User

  #11
  Dec 9, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Huwezi kuzijumuisha na kuna sababu ya kutofanya hivyo. Mtu anaposafiri kikazi fedha anazolipwa haziendi mfukoni mwake bali analipia usafari, malazi hotelini, chakula n.k..hivyo haziingii ktk mfuko wake ikiwa ni ongezeko la pato, na anaporudi kutoka safari hukabidhi stakabadhi za matumizi hayo kisha zinawekwa ktk kifungu chake cha matumizi kimahesabu na sio fungu la Posho.. Kwa hiyo jua kwanza tunazungumzia kitu gani?
   
 12. jebs2002

  jebs2002 JF-Expert Member

  #12
  Dec 9, 2011
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 4,393
  Likes Received: 2,438
  Trophy Points: 280
  Mwambie mwalimu wa shule za msingi, sekondari na vyuoni, vya serikal, kuwa wabunge walipwe hayo mafao ya wizi, wakati wao kupokea tu laki 2 kwa mwezi ni kazi!
  Sijui mnatetea nini hili swala la ongezeka la posho na iliokuwepo, bila kutazama majority!
  Tuna matatizo mengi, ukusanyaji wa kodi, malipo ya TANESCO na DAWASCO/DAWASA, malipo kwa huduma za TTCL n.k.
  hata tukikusanya kodi zote hizo na malipo yote ya huduma, hii haiwapi wabunge haki ya kupokea maposho hovyo hovyo tu!
  FIKIRI!i
   
 13. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #13
  Dec 9, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0

  Sio kwamba watu wanapenda waone watumishi wa umma hawana mafao ya kutosha Tatizo haya mafao yanvyotolewa hayaaangali mambo kama:-

  • Umuhimu wa kazi- Kwa nini mbunge amzidi RPC, Afisa Kilimo, Mifugo, Afya wa mkoa. Ni kazi gani ya umma ni muhumu Tatazame mifano USA, UK, na nchi zilizondelea. matoeo yake watu wanaacha hata kazi vyuo vikuu wanakwenda kuwa wabunge badala ya kufanya kazi za profeefsion zao kwenye mikoa na wilaya.
  • Ukubwa wa kazi- Ukijumlisha na umuhimu wa kazi, watendaji wa afya,elimu, kilimo mikoani na hat wilayani eneo wanalotakiwa kuwajibika ni kubwa zaidi ya wabunge lakini hawana resources.
  • Wapi tunawekeza - Kwa nini Siasa iwe ni kazi inavyvutia kuliko kazi za utendaji. Kwa nini mtu afikirie kusaidia jamiii kwa kuwa mbunge na sio kwa kazi kama ya RPC, afisa elimu, afya, bishara, mhandisi, maji, etc Kwa nini mbunge(mwanasiasa) ndio awe best paid public employee mkoani na sio mtendaji
  Tusidanganyanye wanasiasa wao wanajiongezea mishahara wakidhani wao ndio muhimu sana. Tunajenga kizazi cha wanasiasa badala ya watendaji. Hawa hawa wansiasa huwasikii wakiomba watendaji wanoshughulikia hasa maendeleo waongezewe uwezo hata kuwazidi.

  Hivi mbunge atamlauu vipi afisa elimu wa mkoa wakati hata yeye(mbunge) anajua afisa elimu hajawezeshwa kama wewe.
  • Je anayetakiwa kuleta mabadiliko ya kweli kwenye jamii ni huyu mbunge au ni watu ama maafisa elimu, faya, kilimo
  Kwa hiyo ziitto aelewe suala sio mafao dhhaifu dhaifuaifu suaa ni kazi gani zinapewa Priority??? Kazi gani za umma zinatakiwa kuito Tanzanai kwenye umasikini? Wanasiasa wanajiona wao wanataiwa kuwa juu ya wengine. Wafanaye uchunguzi wabunge wa huko majuu na walinganishe mapato yao na watendaji wengine waone.

  NB
  90 % ya matatizoyetu yamesababishwa na kuchangiwa na siasa. Lakini sio hata 15% ya matatizo yetu yatatuliwa na wanasiasa au kisiasa.
  Kama ni ajira za vijana watangaze kazi za mikataba miaka mitano mitano kwenye kilimo, faya elimu mikoani na wilayani. Na malipo yawazidi wabunge. matokeo watayaona hata bila kuongezza idadi ya majimbo
   
 14. k

  king11 JF-Expert Member

  #14
  Dec 9, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  suluhu ni kuwe na sheria ya malipo ya mishahara kwa kiwango cha elimu na sii taasisi ya kazi unayofanya. mbunge darasa la saba alipwe sawa na darasa la saba wenzake wafagizi wa maofisi na makarani, pia mbunge profesa alipwe sawa na profesa aliye chuo
   
 15. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #15
  Dec 9, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Ukweli ni kwamba serikali haiko serious kwene mapato ila iko bize kukopa na kutumia vibaya hata kile kidogo inachokusanya. Mi ningeshauri kuwepo na task force ya kudumu itakayochunguza mianya yote ya upotevu wa mapato (misamaha ya ajabu ajabu ya kodi,kanuni za kijinga za procurement, ukwepaji chronic wa kodi), njia za kuboresha mapato na kuangalia vyanzo vipya. Hatuezi kuimba maendeleo wakati serikali yenyewe haioni umuhimu wa kuwa na mapato ya kuridhisha.
   
 16. M

  Makupa JF-Expert Member

  #16
  Dec 9, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Zitto anatafuta tu umaarufu sidhani kama anamini.anachokiongea
   
 17. k

  kindafu JF-Expert Member

  #17
  Dec 10, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,114
  Likes Received: 866
  Trophy Points: 280
  Hongera mkuu! Tanzania "siasa" inathaminiwa kuliko "profession"!! Ndo maana watu wanakimbia profession zao wanaingia siasa kwani kwa Tz inalipa zaidi! Je, kwa mtindo huu tutafika?
   
 18. M

  Mkandara Verified User

  #18
  Dec 10, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Hasaaa! unajua nchi zote zenye nia nzuri ya kimaendeleo migogoro ya mishahara na posho hutolewa na watumishi wa Umma, sio kutoka kwa Wabunge wenyewe kwa sababu hawa huangalia zaidi matumizi kutokana na pato la taifa kuepuka kuliingiza taifa ktk deficit. Maajabu kwetu Tanzania migogoro ya posho inaanza na Bunge ambao wanajua fika kuna malipo kibao hayajafanywa, mfumko wa bei, miradi mingi imelala, nchi iko ktk hali mbali kiuchumi, lakini wapo radhi kukataa hata ongezeko la mishahara kwa watumishi wa serikali lakini wanajiongezea wao Posho zao..Hii kama sii laana kitu gani?
   
 19. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #19
  Dec 10, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Lazima zichukuliwe hatua maalum kubana matumizi ya kile kidogo kilichopo sambamba na kuongeza kipato cha serikali

  Hatuwezi kusema kwa vile kuna tija zaidi kwenye kuongeza mapato kwa hiyo faida ndogo ya kubana matumizi ya posho idharauliwe

  Tunatakiwa tubane matumizi kwenye safari za viongozi, sherehe za kitaifa, na kuondoa wabunge wa viti maalum pia. Each and every penny counts
   
 20. G

  Godwine JF-Expert Member

  #20
  Dec 10, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  natambua ya kuwa taifa lina mfumo mbaya wa malipo kwani walimu wanapunjwa sana na polisi ndio usiseme hawawezi ata kujilisha bila ya kutumia rushwa. lakini je suluhu ni kupunguza mafao ya sekta zingine au kuweka sheria ili kila mmoja apate ingawaje laki 8 na kuendelea?
   
Loading...