Tatizo si Madaktari, Walimu, Wafanyakazi,...

nimie

JF-Expert Member
Sep 9, 2011
525
104
Yamesemwa mengi kuhusu migomo na makusudio yake ikihusisha madaktari, walimu na wafanyakazi kwa ujumla wao. Si kwamba hatuoni hali halisi, tuna macho na kwa kweli tunaona. Ukweli ni kwamba, pamoja na kuambiwa kuwa uwezo wa serikali ni mdogo, lakini tunaona jinsi wenzenu waliona nafasi wanavyofaidika na nchi hii. Tunaona na kusikia maliasiri mbalimbali na mahela ya ajabu yanayokwapuliwa humu humu na kwenda kuwekwa huko Uswisi, South Afrika nk. Kweli serikali kama iko puu, lakini mbona fedha nyingi zinaingia mikononi wa wateule wachache? Hiki ndicho kinachotia uchungu na kuwafanya watu wafikie maamuzi yenye muonekano hasi. Mgomo wa madaktari wengi watakufa, wa walimu wanafunzi wengi wanakosa elimu bora, wafanyakazi nao ufanisi unapungua. Watu wamechoka! Ndivyo ninavyoiona hali ya nchi yetu pendwa Tanzania!
 
ni swala la nchi nzima kugoma bila kujali una kazi gani iwe serikalini au nje ya serikali
 
Yamesemwa mengi kuhusu migomo na makusudio yake ikihusisha madaktari, walimu na wafanyakazi kwa ujumla wao. Si kwamba hatuoni hali halisi, tuna macho na kwa kweli tunaona. Ukweli ni kwamba, pamoja na kuambiwa kuwa uwezo wa serikali ni mdogo, lakini tunaona jinsi wenzenu waliona nafasi wanavyofaidika na nchi hii. Tunaona na kusikia maliasiri mbalimbali na mahela ya ajabu yanayokwapuliwa humu humu na kwenda kuwekwa huko Uswisi, South Afrika nk. Kweli serikali kama iko puu, lakini mbona fedha nyingi zinaingia mikononi wa wateule wachache? Hiki ndicho kinachotia uchungu na kuwafanya watu wafikie maamuzi yenye muonekano hasi. Mgomo wa madaktari wengi watakufa, wa walimu wanafunzi wengi wanakosa elimu bora, wafanyakazi nao ufanisi unapungua. Watu wamechoka! Ndivyo ninavyoiona hali ya nchi yetu pendwa Tanzania!
ni kweli kabisa,uwezo wa kulipwa vizuri upo.mbona malipo yao wanarekebisha kila wanapoona inafaa...
 
Naunga mkono kabisaaaa!watz sijui kwa nn wagumu hivi kuchukua hatua,au tumezoea shida!
 
Unajua wenye nchi wameamua kufumba macho na masikio kuweka 'supa glue', hili la madaktari ndilo linawashtua kwa kuwa madhara yake ni ya papo kwa papo, lakini walimu ambao madhara yao ni mpaka matokeo ya mitihani yatoke, hayawasumbui sana.
Lakini hili la walimu watu wasipate shida saana kuliongelea, wao si wanatumia dola kukandamiza wanyonge, sasa mm naishauri serikali ifanye kautafiti haka kadogo tu:
  1. Ni wabunge na wanasiasa wangapi ambao hapo awali walikuwa walimu.
  2. Chunguzeni ni wataalamu wangapi waliobobea katika fani zenye maslahi leo hii serikalini au sekta binafsi ukiangalia CV zao hapo awali kama hakuwapi kupitia Ualimu.
  3. Tembeleeni Vyuo vya Elimu ya Juu, robo ya Wanachuo (Ukijumlisha wale wa Full time & Part time) wanaochukua fani tofauti tofauti zenye maslahi mazuri huko baadaye utagundua ni walimu tena waandamizi. Hii itakupa jibu zuri tu,ndiyo maana walimu wengi wanamaliza vyuo lakini mitaani bado hawatoshi.

Suluhisho:
Naishauri Serikali yangu sikivu kwamba kuongeza vyuo vya Ualimu sio suluhisho la upungufu wa walimu, isipokuwa inaongeza wigo wa wasomi ambao baadye watachukua shahada za juu za fani tofauti na ile ya awali. Suluhisho ni mgawanyo sawa wa rasilimali zilizopo ili kila mtanzania pale alipo anufaike na jasho lake. Lakini kwa stahili ya sasa ya mtu anayesinzia kwenye kiyoyozi kila mwaka anaongezewa marupurupu/mshahara na yule mvuja jasho anaambiwa serikali haina fedha awe mstahimilivu, tunakoelekea mataifa jirani wanatucheka.
 
..... Lakini kwa stahili ya sasa ya mtu anayesinzia kwenye kiyoyozi kila mwaka anaongezewa marupurupu/mshahara na yule mvuja jasho anaambiwa serikali haina fedha awe mstahimilivu, tunakoelekea mataifa jirani wanatucheka.

Watucheke mara ngapi, na sasa wanakuja kwa wingi kuchukua ardhi yetu, serikali unayoiita sikivu inawaangalia tu kana kwamba hawajui kinachoendelea!
 
Back
Top Bottom