Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,529
Watanzania tuna tatizo moja kubwa sana, nalo ni umaikini, umadhubuti, uwajibikaji wa usimamizi wa kanuni, sheria hata katiba!
Si kweli kuwa sheria nyingi ni dhaifu, butu au hakuna "makali" ya kisheria au hata kikatiba. Tatizo letu ni lile lile usimamizi mzuri wa kanuni, sheria na katiba kwa ufanisi, kuzingatia haki, kufuata taratibu na la zaidi kutimiza wajibu ipaswavyo: Kuwajibika.
Majuzi Benki Kuu ilipitia maduka ya fedha Dar, sawa na ilivyofanya maduka ya fedha Arusha mwaka jana. Matamko ya BOT ni kuwa wenye maduka wanakiuka masharti ya uendeshaji maduka hayo.
Leo naibu waziri wa mawasiliano katoa tamko kukataza usafirishaji wa vifurushi kwa njia binafsi mpaka wasafirishaji wapewe vibali na TCRA.
Naomba nimnukuu Rais Magufuli jana kusmea "Watanzania si wajinga sana... niongezee kiasi hicho! Watanzaia si Wajinga, wala si Wajinga sana au Wajinga kidogo. Tunauwezo wa kuuliza na kuhoji na kuuliza na kuhosi kwetu hata kama kutaishia kubaininsha mapungufu au kukosoa haina maana sisi hatuna uzalendo, ni makuwadi wa mabeberu au tunapiga vita kasi ya maendeleo inayofanywa na Serikali ya awamu ya tano.
Suala la BoT na Vifurushi vimenifanya nipekue mtanda na kupitia sheria za Maduka ya fedha na sheria za Posta.
Nilichokikuta kwenye sheria hizo ni uwepo wa misingi thabiti na imara yenye kubainisha masharti ya uendeshaji wa shughuli hizo za biashara (maduka ya pesa, usafirishaji barua na vifurushi) na udhibiti wake ama kwa namna ingine ukaguzi kutoka kwa wenye majukumu ya ukaguzi (regulatory and licencing bodies) kuhakikisha unyoofu wa shughuli hizo za biashara.
Sheria ya BoT ya Maduka ya fedha ya 2015 na 2017 zinazungumzia wenye maduka kuwa na kumbukumbu za mauzo na manunuzi ya fedha na kila transaction ifuate masharti ya kuendesha biashara pamoja na kumjua mteja (Know your customer) na kuzuia utakatishaji wa fedha (Anti Money Laundry and Anti terrorism policy).
Kwenye sheria za Posta za national Postal Policy ya 2018, Postal regulation act ya 2018 na Electronic and Postal Communication quality of services regulation act of 2017, zinazungumzia kwa kina watoaji wa huduma za usafirishaji wa barua na vifurushi kuwa wamesajiliwa na mamlaka husika na wawe wanafuata kanuni, sheria na wajibu kwa mujibu wa sheria.
Aidha kwa sheria zote za BoT na za Posta, kuna msisitizo wa ukaguzi wa uendeshaji biashara hizo kutoka mamlaka husika: supervision and inspection- audit.
Sasa najiuliza, kama yote haya yapo kwenye sheria zetu, inafikaje kunakuwa na uvunjifu mkubwa wa sheria hizi tena kwa muda mrefu bila woga na kuzaa gonjwa la watu kutokufuata kanuni na sheria?
Je leo tunapoona watendaji wanakimbia kuwasilisha miswaada mipya ya sheria na kulundika mafaili kwa Rais apitishe sheria mpya "kali" ni kuficha madhaifu yao ya kushindwa kuwajibika ipaswavyo an kujitengenezea njoa ya mkato ya kuongeza sheria ambazo kiuhalisia zipo sema utekelezaji wake kutoka kwa regulators ni dhaifu?
Je inakuwaje tunakuwa na watendaji ambao wanashindwa kusimamia kwa dhati kanuni na sheria na badala yake kutoa matamko au kufanya mambo ambayo kwa Ujinga wetu mdogo au kutokuwa wajinga sana tunajiuliza kulikoni?
What does Magufuli need to do to fix this problem of lack of accountability kutoka kwa watendaji ( na sizungumzii mawazirri na wateuliwa, hapa ongeza makatibu wakuu, wakurugenzi wa idara na kadhalika)?
Napenda kutoa hoja!