Tatizo si CCM, Tatizo ni unafiki, ujinga, uoga na kukata tamaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tatizo si CCM, Tatizo ni unafiki, ujinga, uoga na kukata tamaa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by only83, Dec 7, 2011.

 1. only83

  only83 JF-Expert Member

  #1
  Dec 7, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  ...................Kila kona ya hii nchi kwasasa ni malalamiko na vilio visivyokwisha vya watanzania wengi....kila mmoja analalamikia maisha magumu na yanazidi kupanda...Baya zaidi,narudia tena baya zaidi hata viongozi wetu wanafahamu kuwa watanzania wanalalamika lakini hawachukui hatua stahiki..badala yake wanaendelea kufanya vituko siku nenda rudi....

  Si ajabu kusikia maneno kama ya spika wa bunge jana..."TUMEONGEZA POSHO KWA WABUNGE KWASABABU YA MAISHA KUWA MAGUMU PALE DODOMA...." Halafu ukapata comments kama hizi kwa watanzania wanafiki,waoga na wajinga....."JAMANI HATA ROMA HAIKUJENGWA KWA SIKU MOJA....." au kusikia hotuba za mkuu wa nchi akisema....

  "TUMEJITAHIDI KUNYANYUA UCHUMI NA KUBANA MATUMIZI,TATIZO MAMBO MENGI YANAYOTOKEA NI NGUVU TOKA NJE,YAANI UCHUMI KUYUMBA ULAYA NI TATIZO KUBWA..." Halafu ukasikia comments za mitanzania mijinga "NI KWELI YAANI ULAYA NI TATIZO KUBWA...."

  .......................Je,mpaka lini watanzania tutaendelea kuilalamikia CCM badala ya kuchukua hatua...Dharau ya spika kwa wananchi maskini ni dhambi kubwa ambayo mimi nashindwa kuvumilia, moyo wangu unataka kupasuka kwa hasira na huzuni..TUJIULIZE watanzania MPAKA LINI ITAKUWA HIVI? Kukubali viongozi wetu watuchezee akili?

  Tumekosa wanaharakati imara akina JUKWAA LA KATIBA wanapelekwa na upepo na wanafikia na maoga...Je tutaendelea kucheka na hawa manyani mpaka lini ili tuje kuvuna mabua?

  ....................Lowasa nae jana katoa kituko TBC1 ati anasema viongozi wanaotuhumiwa kwa ufisadi na dhuluma wawajibike,yaani yeye kashajisafisha muda mrefu,na sasa anawaasa wenzake wachukue uamuzi mgumu kujitoa kwenye chama...

  Hii pia ni dharau kwa watanzania,inakuwaje mwizi unatembea mbele ya watanzania na kuwaambia mimi sio mwizi wakati wafahamu kuwa ulivunja nyumba siku fulani ukaiba? si watakuchoma moto haraka sana? sasa hii ni tofauti kwa Tanzania ya sasa..tunaendelea kucheka na hawa watu...shit!!

  My take:
  Kwa vyovyote vile tatizo la TANZANIA sio CCM ni kwasababu ya Mi-Tanzania mingi minafiki,mioga,mijinga na iliyokata tamaa...

  Nawasilisha!!
   
 2. cooper

  cooper JF-Expert Member

  #2
  Dec 7, 2011
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 394
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Nani kawakatisha tamaa watanzania hawa...., kama hakuna chakula nyumbani nani wa kulaumiwa, watoto au baba mwenye nyumba?
   
 3. a

  alkon Member

  #3
  Dec 7, 2011
  Joined: Sep 25, 2011
  Messages: 16
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nakuunga mkono asilimia zote kabisa. Kwa kweli huwa najiuliza sana kwamba sisi Watz tukoje? Watu wanadanganywa na wanaridhika na majibu mepesi bila shida yoyote. Nchi inakwenda kombo watu wapo tu wanaangalia. Maisha yamepanda, watu wanakufa njaa, nchi inaporwa na maharamia wa kisiasa, lakini shwariiiiiiiii! Kwa kweli kuna mambo ni magumu sana kuyaelewa.

  Cha kushangaza zaidi ni kwamba hao hao wenye shida, wanaokufa njaa, ndio wako mstari wa mbele kufia CCM. Jamani! Ingawa nimekuwa mpinzani mkubwa wa ile nadharia kwamba waafrika wako duni kiakili, huwa kuna nyakati nashindwa hoja za msingi za kujitetea. Hebu angalia bara letu lote uone mambo yanayotendeka. Hebu angalia ubinafsi ulivyokithiri.

  Hebu angalia unyama unaotendwa na watawala. Hapana. Tuna matatizo. Tena Tz tunaongoza kwa kuwa nusu binadamu. Hata mnyama wa porini hawezi kusinzia kama hapa kwetu. Halafu watu wamevaa suti kubwa kubwa, wanajifanya wajanja, lakini vichwani matope matupu. Hata kama fujo hatupendi, je, hatuwezi hata kuitoa CCM madarakani kwa kura?
   
 4. ntogwisangu

  ntogwisangu JF-Expert Member

  #4
  Dec 7, 2011
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 516
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  na hapa ndipo kwenye hoja!!!!wananchi wamechoka!!!!tukichanga karata vizuri ccm watatoka madarakani!!!!hoja yangu kuna ombwe la uongozi cdm!!!!nafasi ya kuingia ikulu hipo wazi ila kamanda mbowe mh!!!sijui!!
   
 5. Komeo

  Komeo JF-Expert Member

  #5
  Dec 7, 2011
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 2,393
  Likes Received: 423
  Trophy Points: 180
  Nakubaliana nawe. Sasa nini kifanyike ili kuwaondolea wenzetu watz walio wengi ujinga na ili wachukue maamuzi sahihi ya kuwawajibisha viongozi wao waliowachagua wenyewe kwa "kishindo" baada ya kuhongwa kapelo na pilau? Ni kweli dharau ipo kila kona ya nchi, na kibaya zaidi hao mafisadi wanaofaidika na ujinga wa ndugu zetu wanatumia mbinu zote kuhakikisha kuwa ujinga hautoki vichwani mwa ndugu zetu. Hakika inatia hasira.
   
 6. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #6
  Dec 7, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Hapana.Tatizo si mitanzania mioga.Mkuu tatizo ni CCM.Narudia tatizo ni chama dhalimu cha kibepari cha CCM.CCM ndiyo imetengeneza mazingira yote ya unyonge na uzuzu wa mitanzania unayoisema.CCM ndiyo yenye serikali lakini inaiacha serikali ifanye utumbo inavyotaka.Imeshindwa kuidhibiti serikali yake.CCM imeshindwa kuwatetea watanzania wanyonge!Spika kutoka CCM anabariki WIZI kupitia POSHO lakini CCM inashangilia tena kwa vigelegele!Mkuu CCM imepoteza maana ya kuundwa kwake.Si chama cha wanyonge tena.Ni chama kinachojali maslahi ya wabunge wake na matajiri.Watanzania tusiwaonee kabisa.Tatizo ni CCM ambayo imejipa haki miliki ya kutawala milele kwa kila mbinu.Lakini OLE WAO.Siku yao yaja.
   
 7. TECHMAN

  TECHMAN JF-Expert Member

  #7
  Dec 7, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 2,677
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 160
  Siku elewi unaposema tatizo sio CCM, mimi nasema Tatizo ni CCM kwa asilimia 100%.
  Viongozi wabaya tulio nao ni zao la uongozi mbovu wa CCM, maendeleo duni tuliyo nayo ni mzao wa sera mbovu za chama tawala CCM,

  Unafiki, ujinga,uoga na kukata tamaa, vimesababiswa na CCM
   
 8. only83

  only83 JF-Expert Member

  #8
  Dec 7, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Kama ingekuwa ni CCM tungekuwa tumewang'oa muda mrefu bila kujali kwa kura au shinikizo...tumebakia tunawakenulia meno tu...Pumbavu!!
   
 9. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #9
  Dec 7, 2011
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Udanganyika symptoms
   
 10. b

  buyegiboseba JF-Expert Member

  #10
  Dec 7, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jipu halitumbuliwi kabla halijaiva ukiliwahisha litahamia sehemu nyingine ya mwili,usipate shida hata kule walikoweza imewachukua miaka ya dhuluma,taabu,uonevu na uchafu wa kila namna, ila jipu lilipoiva walitumbua na kuondoa kiini kabisa.yanayotokea tz ni mchakato wa kuiva jipu,Utashangaa watanzania hawa hawa unaohoji wakoje watambua jipu na kuondoa kiini chote,na ingekuwa vizuri zaidi kama kero zinazidi anza WEWE kuonyesha mfano badala ya kuhoji wako wapi kina...!
  Lenye mwanzo..

   
 11. A

  Ame JF-Expert Member

  #11
  Dec 7, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Tatizo la Tanzania ni CCM kwajinsi yoyote wala tusi dilute hapo. Wana intimidate watu sana; wana victimize wachache wanaojitokeza na burden ya uzalendo wao unabebwa na familia siyo watanzania hao wanao tetewa.

  CCM imeweka system ya unyanyasaji wenyewe wanaita matawi na mashina wakishirikiana na maafisa utendaji wasio tenda chochote zaidi ya kuiba michango ya raia wasiojua haki zao; hao viongozi ni miungu watu huko wanako patikana. Hao ndiyo ambao niwanafaki na vibaraka ambao wanalipwa kwa bei ya t-shirts; kanga, pilau ya mara moja pale viongozi wanapo watembelea na sifa za kijinga kuwa eti wao ndiyo wakuu wa maeneo. I hate the behaviours of these CCM members wa ngazi ya chini kama ninavyo ichukia dhambi. Its a devide and rule mechanism ambayo kiongozi anapewa incentive kidogo inayo mtofautisha na wenzake ili aendelee kuwa kibaraka. Hiyo inaendelea mpaka juu ambapo chief executive ni kada mzuri wa chama na juu yake kuna waziri ambaye ni kada mwingine wa chama na package yao ina kila kinono huku wengine wakiambulia mifupa.

  CHADEMA wamesaidia sana kupunguza nguvu ya hili dubwana CCM lakini bado haijaweza kuipeleka hatua ya kuwa disintegrated kwakua pia hali za raia wengi ni masikini ambao kwasababu ya un-commercialised economy wanaweza kujipatia chakuingiza tumboni so wanaona kuliko waswekwe magereza na kuawaacha wanaowategemea wawe tu wanfiki mpaka mwokozi atakapo patikana.

  Hiki ndicho kilichonifanya niichukie CCM na kuiepuka kama ukoma kwani hawako objective wamekaa ki-vimpire zaidi na watu wasio na huruma wala staha inapokuja kwenye kulinda its corrupt system kwa faida ya wachache.
   
 12. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #12
  Dec 7, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Craaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaap hakuna kitu na km watanzania wako hivyo ww ndio zaidi yao sasa

   
 13. R

  RMA JF-Expert Member

  #13
  Dec 7, 2011
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtoa hoja hajakosea hata kidogo! Tatizo ni watanzania wenyewe! Hiyo ccm ni nani aliipa ushindi wa kuongoza? Si ni watanzania wenyewe wanaoleta ushabiki usiokuwa na tija katika siasa baada ya kupokea rushwa ya vikofia vya kijani na chumvi? Ccm sio tatizo kwa vile iko chini ya uwezo wa watanzania kwa njia ya masanduku ya kura. Tatizo ni fikra butu za watanzania wanaodanganywa kwamba bila ccm hakuna amani!
   
 14. M

  Madcheda JF-Expert Member

  #14
  Dec 7, 2011
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 416
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Naunga mkono na mguu hoja! Soma kitabu cha malima bundala "waafrica ndivyo walivyo"
   
 15. m

  massai JF-Expert Member

  #15
  Dec 7, 2011
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mtanzania ni bora afe na njaa kuliko afe kwenye vita yakupinga njaa
   
 16. damper

  damper JF-Expert Member

  #16
  Dec 7, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 207
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  kweli tuna shida lakini hatujapata MWOKOZI wa ukweli. Hata hawa wenye dhamana walikuwa kama hawa waliopanga foleni ya kwenda magogoni. KAMA LIMEKUKERA LIV ME ALONE
   
 17. Kifimboplayer

  Kifimboplayer JF-Expert Member

  #17
  Mar 12, 2016
  Joined: Nov 24, 2013
  Messages: 1,438
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  aliona mbali huyu jamaa
   
 18. cerengeti

  cerengeti JF-Expert Member

  #18
  Mar 12, 2016
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 3,633
  Likes Received: 1,165
  Trophy Points: 280
  Mi-tanzania, nimeipenda sana
   
Loading...