Tatizo: nikinywa maziwa, bia au nikila chakula chenye pilipili nasikia maumivu kifuani yanayodumu kwa Masaa kadhaa.

nacho1

nacho1

Member
Joined
Aug 31, 2014
Messages
38
Points
95
nacho1

nacho1

Member
Joined Aug 31, 2014
38 95
Mwanzo wa tatizo
Tatizo lilianza mwaka jana August 2018 pale ambapo nilianza kuhisi maumivu yanayokuja kwa kasi na kupungua kifuani karibu na eneo la moyo. Maumivu hayo nilihisi yanahusiana na moyo moja kwa moja. Kadiri muda ulivyoenda ilifika wakati nikawa nashindwa kumeza kitu.

Nilienda hospital ambapo dr. Alinieleza maumivu hayo hayahusiani na moyo bali huenda ni ulcers inaninyemelea. Nilipimwa damu ili kuona kama nina bacteria aitwae H. Pylori ambapo baada ya vipimo nilionekana sina tatizo hilo. Dr. Aliniandikia dawa za kupunguza acid tumboni na dawa nyingine za kutibu UPD.

Nikiwa pale hospital nilimsikia Dr. Akitamka 'heart burn' hivyo nilihamua kwenda ku-google ambambo moja kwa moja ilinileta JF the home of great thinkers nikakutana na uzi wa mdau mmoja akielezea namna alivyotibu heart burn kwa kutumia BICARBONATE OF SODA nikahamua kuachana na zile dawa za hospital na kutumia hio bicarbonate. Nilipata nafuu kubwa na maumivu yalipotea kwa miezi kadhaa.

Hali ilivyo Sasa
Kwanzia mwaka huu 2019 March imekua nikinywa maziwa, bia au kutumia pilipili napata shida sana kwani baada ya hapo nasikia maumivu mithili kwamba kifuani ndani kuna mchubuko flani. Mwezi wa tano nilirudi hospital nikamkuta Dr. Mwingine akaniambia niassume sijawahi kupimwa chochote akachukua vipimo upya lakini hakuona tatizo lolote akaniandikia dawa zilezile za mwanzo na nilizitumia lakini sikupona.

nimefika hapa kuomba msaada kwayeyote mwenye kujua sulihisho
 
E

E and E

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2017
Messages
749
Points
1,000
E

E and E

JF-Expert Member
Joined Jun 15, 2017
749 1,000
kuna hali nyingi zinazohusiana na maumivu kama hayo achilia mbali hiyo unayoita ulcers, waza kuhusu moyo mfano endapo damu haizunguki vyema kwenye mishipa ya damu ndani ya moyo(coronary heart disease, myocardia ischaemia, angina pectoris ), trachea ni njia ya kupitisha hewa inapopata vijeraha kutokana na matumizi ya pombe,sigara au kufanya kazi kwenye hewa iliyochafuliwa mfano viwandani au kwenye vumbi nyingi , Aina za virus is na bacteria kuvamia maeneo hayo (tracheitis ), mapafu kutopata damu vyema kutokana na kuzuiwa na uvimbe au kitu kitaalamu inaitwa thromb ( pulmonary embolisim ).

Nenda kufanyiwe vipimo katika maeneo hayo kama ECG, na vingine kulingana na jinsi daktari wako atavyoona.
 
Sawa mkuu nitalifanyia kazi.
 
sinajinasasa

sinajinasasa

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2013
Messages
1,939
Points
2,000
sinajinasasa

sinajinasasa

JF-Expert Member
Joined Dec 10, 2013
1,939 2,000
Ukome!
Ulishapata dalili hizo za heartburn, ukashauriwa utumie bircarbonate of soda ukapata nafuu kubwa.
Umeanza tena mchezo wako wa kujitia matakataka mwilini ya Bia, maziwa na pilipili, hujui kwamba hayo ndo yanakudhuru?
Wewe mwenyewe unajua kabisa kuwa vitu hivyo ndo vinakupa shida na wewe unang'ang'ania kuvitumia, si uviache sasa?Watu mnapenda kutumia vitu vyenye kuwadhuru afu unalalamika kuomba msaada, msaada gani, wa kuacha kutumia hivyo vyakula au msaada wa maumivu yako. Tumia hiyo hiyo bircarbonate, ukipata nafuu ndo uache kabisa kutumia takataka.
Mwanzo wa tatizo
Tatizo lilianza mwaka jana August 2018 pale ambapo nilianza kuhisi maumivu yanayokuja kwa kasi na kupungua kifuani karibu na eneo la moyo. Maumivu hayo nilihisi yanahusiana na moyo moja kwa moja. Kadiri muda ulivyoenda ilifika wakati nikawa nashindwa kumeza kitu.

Nilienda hospital ambapo dr. Alinieleza maumivu hayo hayahusiani na moyo bali huenda ni ulcers inaninyemelea. Nilipimwa damu ili kuona kama nina bacteria aitwae H. Pylori ambapo baada ya vipimo nilionekana sina tatizo hilo. Dr. Aliniandikia dawa za kupunguza acid tumboni na dawa nyingine za kutibu UPD.

Nikiwa pale hospital nilimsikia Dr. Akitamka 'heart burn' hivyo nilihamua kwenda ku-google ambambo moja kwa moja ilinileta JF the home of great thinkers nikakutana na uzi wa mdau mmoja akielezea namna alivyotibu heart burn kwa kutumia BICARBONATE OF SODA nikahamua kuachana na zile dawa za hospital na kutumia hio bicarbonate. Nilipata nafuu kubwa na maumivu yalipotea kwa miezi kadhaa.

Hali ilivyo Sasa
Kwanzia mwaka huu 2019 March imekua nikinywa maziwa, bia au kutumia pilipili napata shida sana kwani baada ya hapo nasikia maumivu mithili kwamba kifuani ndani kuna mchubuko flani. Mwezi wa tano nilirudi hospital nikamkuta Dr. Mwingine akaniambia niassume sijawahi kupimwa chochote akachukua vipimo upya lakini hakuona tatizo lolote akaniandikia dawa zilezile za mwanzo na nilizitumia lakini sikupona.

nimefika hapa kuomba msaada kwayeyote mwenye kujua sulihisho
 
mtzedi

mtzedi

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2011
Messages
3,223
Points
2,000
mtzedi

mtzedi

JF-Expert Member
Joined Dec 13, 2011
3,223 2,000
Ukome!
Ulishapata dalili hizo za heartburn, ukashauriwa utumie bircarbonate of soda ukapata nafuu kubwa.
Umeanza tena mchezo wako wa kujitia matakataka mwilini ya Bia, maziwa na pilipili, hujui kwamba hayo ndo yanakudhuru?
Wewe mwenyewe unajua kabisa kuwa vitu hivyo ndo vinakupa shida na wewe unang'ang'ania kuvitumia, si uviache sasa?Watu mnapenda kutumia vitu vyenye kuwadhuru afu unalalamika kuomba msaada, msaada gani, wa kuacha kutumia hivyo vyakula au msaada wa maumivu yako. Tumia hiyo hiyo bircarbonate, ukipata nafuu ndo uache kabisa kutumia takataka.
Tafadhali sana usiite bia matakataka!
 
stunnerjr

stunnerjr

Senior Member
Joined
Jul 17, 2018
Messages
133
Points
250
stunnerjr

stunnerjr

Senior Member
Joined Jul 17, 2018
133 250
Kubaliana na hiyo hali..hilo ni tatizo la acid kujaa tumboni.... Mimi ninailo tatizo yapata miaka 2.... Nimeachana na amaharage, pilipili, mtindi, ndimu.... Na kunywa maji mengi....

Cha kukushauri brother acha hizo bia pamoja na hivyo vitu ambavyo vinakuletea madhara
 
Smart911

Smart911

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2014
Messages
35,393
Points
2,000
Smart911

Smart911

JF-Expert Member
Joined Jan 3, 2014
35,393 2,000
Pole sana...

Sky Eclat ukipata muda pitia hapa...

Cc: mahondaw
 
nacho1

nacho1

Member
Joined
Aug 31, 2014
Messages
38
Points
95
nacho1

nacho1

Member
Joined Aug 31, 2014
38 95
Kubaliana na hiyo hali..hilo ni tatizo la acid kujaa tumboni.... Mimi ninailo tatizo yapata miaka 2.... Nimeachana na amaharage, pilipili, mtindi, ndimu.... Na kunywa maji mengi....

Cha kukushauri brother acha hizo bia pamoja na hivyo vitu ambavyo vinakuletea madhara
Umenitia moyo kwa kweli. Ushauri nitazingatia
 
Forum statistics

Threads 1,342,748
Members 514,784
Posts 32,762,727
Top