Tatizo ni watoa rushwa sio mpokeaji rushwa, labda haijawahi kukukuta

ddcmanesto

Senior Member
Nov 16, 2016
122
39
Rushwa ni janga ambalo kuisha si rahisi amini nakwambia. Kwa mtu ambaye hajakutana na majanga yanayomuhitaji atoe rushwa anaweza kupinga.
Mwaka 2009 nilibahatika kupata binti, mzuri nilimpenda na nikaanza kuishi naye akabahatika kupata ujauzito. Ilipofika miezi sita akapata tatizo la kutokwa na damu usiku nilimpeleka hospitali.

Kwa bahati nzuri tuliwahi mapema walimchunguza na kusema mama na mtoto wako salama ila mgonjwa abaki kwa tahadhari . Nikaondoka nikampa kidogodogo dokta ili amuhudumie vizuri kwa kuwa kazi zangu zilikuwa za kuungaunga nilimwachia mama mkwe wangu kiasi cha pesa kwa ajili ya tahadhari.

Ilipofika kesho yake asubuhi hali ilibadilika, mgonjwa akajifungua kitu ambacho kilimfanya apoteze damu nyingi. Mtoto bahati mbaya alifariki, nilipigiwa simu nikawambia nipo mbali nakuja ila wamcheki damu. Manesi walipewa taarifa hizo lakini walijizungushazungusha huku wakiuliza mume wake anarudi saa ngapi maana waliona mama mkwe wangu hatoi kitu wala haelewi wanachohitaji ili wamuongezee damu.

Nikampa taarifa dada yangu aende, alipofika akawapa kidogo wakaanza kumuhudumia. Wakamwambia akanunue drip n.k. Wakati anatoka kununua nikakutana naye akanipa taarifa mgonjwa yuko vizuri kwa kuwa aliongea naye. Tukawa tunaelekea wodini tulipofika tu tukapewa taarifa mgonjwa amefariki kwa upungufu wa damu.

Niliumia sana nikijua rushwa ndiyo sababu. Kilichonifanya kuandika haya ni baada ya kutoneshwa kidonda cha muda mrefu. Baada ya muda mrefu bila kutamani mahusiano wala kwenda hospital nikabahatika tena kupata mke niliyefunga naye ndoa na kupata ujauzito, na sasa nina mtoto wa siku mbili.

Matukio yaliyojitokeza ni yale yale rushwa mke wangu ananisimulia alipokuwa analalamika hawakumsikiliza hapo wakati huo damu zinamtoka nikampa taarifa dada yangu awe na mkono mrefu kwani nilikuwa mbali natokea Moro kuja Dar alipo yeye.

Baada ya pesa hiyo huku wakikataa kadi ya Bima ambayo serikali inaipigia debe, walimpa huduma na kufanikiwa kujifungua salama lakini hadi hivi sasa siamini.

Kilichoniumiza na kinaniuma hadi sasa leo asubuhi wakati natoka kumtazama mke wangu nilikutana na jirani yangu tukasalimiana akanipongeza na kusema yeye amemleta mtoto wake ambaye ni mjamzito. Nikamtakia kila la heri lakini hadi sasa nipo nyumbani tunasubiri maiti ije kwani mtoto wake amefariki kwa tatizo la upungufu wa damu nyingi wakati anajifungua.

Roho inauma sana nikikumbuka ni zilezile dharau zao mpaka uwape hela. Halafu huwa wanaandika kirahisi tu eti amekufa kwa upungufu wa damu.
Nikatambua tatizo si mpokeaji au muomba rushwa usipotoa wanakupita kama hawakujui au si mgonjwa.

Hakika ni sisi watoaji hata kama hawakwambii toa maana hatuwezi kuwa wajinga kiasi cha kumuacha mgonjwa anakufa na kupeleka taarifa kitengo cha rushwa mkasumbuane huko. Na hata ukipeleka taarifa hawana msaada wowote zaidi hospital nzima itakuchukia mgonjwa.

Inauma sana sana. Nafikiri ili kupambana na rushwa ni kuwaboreshea maisha wahudumu hivyo vita vyenu dhidi ya rushwa kwa kuwauliza wagonjwa kuwataja walioomba rushwa ni kutujengea chuki na wauguzi wetu. Pia nafikiri mtu akifa Kwa upungufu wa damu wakati mgonjwa yupo hospital hatua kali zichukuliwe ni uzembe wa hali ya juu Sana.

Kama unajua mjamzito atajifungua na atatoka damu kwanini usimpime damu mapema kabla ya yote? Subiri yakufike uone kama utatoa au hautatoa rushwa.
 
Mkuu pole na maswahibu na jirani yetu pia zimfikie pole hizi.Amina.

Rushwa ni mtego unaotegwa kwa namna mbaya sana, kiasi kuna wakati kwa kunasa utajihisi ni shujaa na kuna wakati utajihisi kinda la kuku kwenye mvua.

Huwa napenda kuzungumzia rushwa za barabarani, hasa kwa wanaolalamika, kimsingi huwa ni ubwege kukubali kutoa hela maana kwa mtu anayeichukia rushwa kutoka moyoni anazo njia nyingi za kuikwepa rushwa ya namna kama ile.

Lakini kwa mazingira kama hospitali, usaili wa kazi,mahakamani, hata Mungu anaona.hapa haihitaji kuchukua hatua bali pia neema ya Mungu iingilie kati.
Wahusika wanafanya hivyo wakijua kabisa hufurukuti, na ukijifanya mjuaji tu hawana cha kupoteza-ndipo hapa hata mwenye dhamana ya kuzuia rushwa huwa inabidi atoe rushwa.

Hii vita ni kubwa sana, tofauti na tunavyodhania kupambana nayo kwa kuiundia taasisi za kuizuia bila kuchimbua mazingira yake.
 
Back
Top Bottom