Tatizo ni Watanzani Kudanganywa muda mrefu na si Chadema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tatizo ni Watanzani Kudanganywa muda mrefu na si Chadema

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by STEIN, Mar 4, 2011.

 1. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #1
  Mar 4, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ndugu zangu wanaJF na watanzania kwa ujumla, Naomba nitoe ufafanuzi wa mambo kadhaa ambayo yamekuwa yakitokea mara kwa mara nchini kwetu.

  1. Kumekuwa na hali mbaya sana ya maisha kwa wananchi wa kawaida ambao wamefikia hatua ya kukata tamaa na viongozi waliowachagua ili washughulikie matatizo yao wamegeuka na badala yake hao viongozi wamekuwa wanafanya ufisadi wa kutisha hadi taifa linatumbukia kwenye dimbwi la umasikini wa kutupwa na bei ya vitu kupanda mara dufu.

  2. Badala ya Serikali kuwatetea wananchi wake imekuwa ikiwatetea mafisadi wachache ambao mwisho wa siku hawawezi kuisaidia serikali pakianza kuchimbika, watabaki wanakimbilia nje ya nchi mfano haiwezekani Rostam alete kampuni feki ya kuzalisha umeme, na umeme wenyewe haupo na watu wapo gizani then unasema tuilipe hiyo kampuni hewa, hili haliwezekani.
  Sasa wananchi wameshaelewa haki zao na wajibu wa viongozi wa serikali na hasa wa CCM.

  Wasijidanganye kwa kuwatisha wananchi ile hali wao hawachukui hatu yeyote katika kutatua maisha ya watanzania, tunasikia katika nchi za jirani hakuna matatizo ya vitu kupanda bei kiholela hasa Mafuta, umeme, Bei za vyakula lakina hapa kwetu kwa sababu ya monopoly katika biashara watu wanalala wakiamka wanapandisha bei, na serikali ndio yenye jukumu la kuchukua hatua juu ya watu/wafanyabiasha hawa, ndio kwanza inawatetea. Wananchi watafanya nini?

  Badala yake wanafikiria jawabu ni kuwatisha kwa kuifuta CDM na kuwashitaki viongozi wake, wasiwe wavivu wa kufikiria na wajiulize hivi tatizo ni CDM au wananchi wamechoka na CCM na wanataka maisha bora ambayo ameahidi JK wakati wa kampeni na kadiri siku zinavyoenda maisha yanazidi kuwa magumu.

  3. CCM na serikali yake wanataka kuilipa kampuni hewa mabilioni ya shilingi huku wanafunzi wanakosa mikopo, wafanyakazi mishahara haitoshi na hawataki kuiongeza kwa sababu pesa hazipo lakini za kulipia makampuni hewa ya mafisadi wanazo je unafikiri wananchi hawalitambui hilo? Je sulihisho la kuyatatua hayo ni kuifuta CDM na kuwatisha wananchi?, mwanzoni walikuwa wanatishika lakini ukiendelea kuwatisha itafika mahali hawatishiki, wazee wanasema "Ukimkimbiza sana mjusi anageuka kuwa nyoka" je utaendelea kumkimbiza?

  4. Huu ni wakati mgumu ambapo wananchi wote wanataka kuona serikali yao ikiwajibika lakini wao wanabaki kulalamika, mfano Sofia Simba, Wasira, Kilango, Mrema na Cheyo, haya yote ni matokeo ya viongozi kutokutaka kufikiria na kutekeleza wanayotaka wananchi.

  5. Ni wazi kuwa wabunge wengi hawakuchaguliwa na wananchi bali walifanya ujannja ujanja kupita na kuwa wabunge wa wananchi sasa wamegeuka na kuwa watetezi wa mafisa badala ya wananchi, tunawafahamu na wako wengi, na wao wanajifahamu na ndio maana wanayaogopa maandamano ya watanzania kwani wakisema hawakumchagua ataondoka madarakani na hilo ndilo kinachowasumbua wabunge wengi wa CCM.

  5. Juzi bila aibu wanajichukulia mil. 90 kila moja huku wakipaza sauti eti serikali itanunua bajaji kwa ajili ya kuwabeba wajawazito vijijini, je kwa nini magari yao mil. 90 lakini bajaji kwa ajili ya kubebea wagonjwa? hivi katika hili kuna mtanzania atawaunga mkono? Haiwezekani kuendelea kutuaminisha tZ nchi masikini huku wao wakivuna rasilimali za nchi hii na kuwapa wageni bure huku wao wakifaidi sehemu ya pesa hizo.

  Mimi nafikiri kwa tulikofikia waTZ karibu wote wamekuwa kitu kimoja na wanachotaka ni kuona serikali inachukua hatua za makusudi kuwatoa kwenye dimbwi la umasikini na si kwenda kwenye media kuwapiga vijembe wananchi siku uvumilivu ukiwashinda au siku serikali ikiwachokoza ndio itakuwa ni mwisho wa CCM na viongozi wake kuongoza hii nchi.

  Naomba kuwasilisha kwa leo   
 2. MANI

  MANI Platinum Member

  #2
  Mar 4, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,861
  Trophy Points: 280
  Mkuu Stein,

  Usemacho ni kweli ila sisi watanzania tuna woga wa kusema kuwa serekali inakosea. Tumekuwa na nidhamu ya woga kiasi kwamba hata zile haki zetu za msingi tunaona ni kama tunu serekali kututendea. Ni wakati wa mabadilko sasa mungu ibariki Tanzania
   
 3. M

  Marytina JF-Expert Member

  #3
  Mar 4, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Acha usiseme serikali ni mbofumbofu utaambiwa unaleta udini.Maisha magumu+Wadai wa haki ni wadini.
   
 4. DAUDI GEMBE

  DAUDI GEMBE Member

  #4
  Mar 4, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hell is for heroes we must fight 4 ourself and the future generation
   
 5. b

  boybsema Senior Member

  #5
  Mar 4, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 125
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Tumechoka na sasa lazima kieleweke
  hatutishiki tena walizoea enzi hizo...lazima kieleweke!!!
   
 6. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #6
  Mar 4, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Tatizo nikuwa mambuzi yanapigiwa gitaaaa sijui wamelogwa!!
   
 7. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #7
  Mar 4, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  peoples power!!!!!!!!!!
   
 8. Tumaini edson

  Tumaini edson Member

  #8
  Mar 4, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yeah, Hakuna marefu yasiyo Ncha. Kama waliondoka Wakoloni, waliokuwa na nguvu na uwezo wa kila aina, itakuwa CCM!
   
 9. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #9
  Mar 4, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Wakuu,

  Henge, mani,boybsems

  peoples power; TZ bila mafisadi ni lazima siyo hiari
   
 10. sekulu

  sekulu JF-Expert Member

  #10
  Mar 4, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 934
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Ni kupuuza matakwa ya umma,

  Wanadhani chadema inaweza kutushawishi kitu????

  Chadema imeona na Wananchi wanakubali kinachosemwa na Chadema na ndo maana watu wengi wanakisaport chama cha chadema. Sisi tumekua na akili ya kwamba CCM et imetukomboa ni ujinga kuiacha iendelee kuharibu nchi, Mwalimu alifanya kazi mijinga inakuja kuharibu. Puuumbaf!
   
Loading...