Tatizo ni nini?

PHILE1879

JF-Expert Member
May 6, 2013
636
473
Nimekuwa nikifuatilia tawala mbali mbali na viongozi mbali mbali.Ila wote /Zote zina/wana shortcomings.Mfano Mwl.Nyerere wengi wana msifu ila nashangaa eti kuna waliotaka kumpindua.Akastaafu.Rais Mwinyi akafuata,baadae Rais Mkapa na Rais Kikwete na sasa Rais Magufuli.KILA Rais anayetawala watu wanasema bora aliyepita.Hili tatizo liko DUNIA mzima.Tumeona pia Marekani ,Libya,Misri,Syria nk nk.KWA NINI KILA RAIS,KILA CHAMA ,KILA MFUMO UNA MAPUNGUFU? KWA NINI BORA CHAMA KILICHOTAWALA JANA KULIKO HIKI KIPYA? SULUHU NI NINI HASA? au niseme TATIZO NI NINI?
 
Tatizo ni binadamu sio mkamilifu na pia kamwe haridhiki, jambo dogo sana linakuumiza kichwa, it's human nature playing its part brother
 
Hatufanani kama alama za vidole ndio maana
Huyu akiwatetea wanyonge matajiri watamchukia
Na mwingine akiwakumbatia matajiri masikini watamchukia!
 
Kwa hiyo hii hali utakuwa hivi hivi TU? vita baada ya vita, machafuko nk nk?
 
Toka dunia inaumbwa hakujaisha vita, machafuko, kuuana, na mvurugano mwingine, binadamu tumeumbwa tuna pupa na haturidhiki, so hata siku moja binadamu hakamiliki, labda akifuata muongozo wa dini kidogo matatizo yatapungua lakini kwa kutumia akili yake tu basi kamwe itakuwa hivyo until the end of the world
 
Daah hii mitandao hii, wakati mwengine inaboa sana, yaani nilijibu hii post yako vema sana, ikakataa kukufikia, imenisikitisha sana. Ila usijali, kiufupi ni, neno ama maneno Upendo, Upendo, Upendo, nimelirudia mara tatu kwa kuwa lina maana yake kubwa tu. Yesu alisema hata yeye, zipo amri kuu mbili, ila moja ni kuu kuliko zote, 'mpende Mungu wako kwa kila kitu chako (akili, kiroho, kimwili), mpende mwenzio (binadamu) kama unavyojipenda wewe mwenyewe' na ukiangalia hapo, neno Upendo limekaziwa sana. Mtume Paulo nae alisema, 'unaweza ukayafanya yote ya mbinguni na duniani, ila kama hauna Upendo, ni kazi bure'. Hivyo, yalisemwa hayo, kwa kuwa tayari dunia na asili yake ilishaharibika tangu awali na Mungu hakutaka iwe hivi. (sijanukuu namba za maandiko, naamini ujumbe tu hivi unatosha, maana kunukuu kunaweza kuwakwaza wengine), na kama wewe ni Mkristo, basi ushayasikia hayo sana tu.

Nyongeza ni ya Kwangu
( Emphasis is Mine).

Ahsante!
 
Asante kwa ujumbe murua.Nilisoma Mwanzo 1:28 zaeni mjaze DUNIA mtawale samaki,ndege,wanyama.

Je binadamu inawezekana hakuumbwa atawale binadamu mwenzake?
 
So what's the SOLUTION?
Ukitaka solutions ya hayo uyafikiriayo maana yake vitu vyote vitafika mwisho,dunia,dini,mahakama,na vingine vyote vinavyomzunguka na avifanyavyo binadamu,kifupi ni kwamba hakuna solutions,hivyo vyote vikusikitishavyo ndio vinaleta maana halisi ya maisha,na ndio maisha....upo?
 
Back
Top Bottom